Tafuta

Papa Francisko amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dodoma,Tanzania Mhs Padre Wilbroad Henry Kibozi(katikati). Papa Francisko amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dodoma,Tanzania Mhs Padre Wilbroad Henry Kibozi(katikati). 

Padre W.H.Kibozi ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dodoma,Tanzania

Papa amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Tanzania,Mheshimiwa sana Padre Wilbroad Henry Kibozi,wa Jimbo Kuu hilo hilo,ambaye hadi uteuzi alikuwa ni Makamu Gambera na Profesa wa Seminari kuu ya Familia Takatifu,Kahama,kwa kumpatia makao ya Zallata.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 12 Februari 2024 Kanisa nchini Tanzania linayo furaha kubwa kwa kumpata Askofu mwingine mpya, kwa sababu, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma nchini Tanzania, Mheshimiwa sana Padre Wilbroad Henry Kibozi, wa Jimbo Kuu hilo hilo, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Makamu Gambera na Profesa wa Seminari kuu ya Familia Takatifu, Kahama, kwa kumpatia makao ya Zallata.

Wasifu wake

Askofu Mteule, Padre Wilbroad Henry Kibozi alizaliwa mnamo tarehe 30 Aprili 1973 mjini Dodoma. Majiundo yake baada ya sekondari alisoma Falsafa katika Seminari Kuu ya Ntungamo, Jimbo Katoliki la Bukoba na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Kipalapala Jimbo Kuu Katoliki la Tabora. Baada ya kufanya shughuli za kichungaji kwa muda wa mwaka mmoja katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji huko Chalinze (Dodoma), aliendelea na masomo na kupata leseni na Shahada ya Udaktari wa Taalimungu katika Kitivo cha Taalimungu cha Italia ya Kati huko Firenze.

Papa amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki,Dodoma Tanzania,Padre Wilbroad Henry Kibozi
Papa amemteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki,Dodoma Tanzania,Padre Wilbroad Henry Kibozi

Daraja la Upadre

Alipewa daraja takatifu la Upadre  mnamo tarehe 9 Julai 2010 kwa ajili ya Jimbo lake kuu, Dodoma Tanzania.

Nyadhifa

Alishika hata nyadhifa nyingine kama vile: Paroko msaizidi wa Lumuma (2010-2012); Mkurugenzi wa Miito Jimbo Kuu la Dodoma (2012-2014); Muungamishi katika Nyumba ya Malezi huko Livorno, Italia (2017-2019); Mkufunzi wa Waseminari katika Chuo Kikuu cha Jordan, Morogoro (2019-2020); tangu 2020, amekuwa Makamu Gambera na Profesa katika Seminari Kuu ya Familia Takatifu ya Kahama, Tanzania.

Papa amteua Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma Tanzania
12 February 2024, 12:11