Tafuta

Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk Balozi mpya wa Vatican nchini Zimbabwe Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk Balozi mpya wa Vatican nchini Zimbabwe 

Askofu Mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk Balozi Mpya wa Vatican Nchini Zimbabwe

Askofu mkuu mteule Janusz Stanisław Urbańczyk alizaliwa tarehe 19 Mei 1967 huko Kraszewo, Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Juni 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Elbag. Kimasomo alibahatika kupata Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa. Tarehe 25 Januari 2024 Papa Francisko amemteua kuwa Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe na kumpandisha hadi ya kuwa Askofu mkuu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 25 Januari 2024 amemteua Monsinyo Janusz Stanisław Urbańczyk kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zimbabwe na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa ni Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Janusz Stanisław Urbańczyk alikuwa ni Mwakilishi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Vienna, Austria. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Janusz Stanisław Urbańczyk alizaliwa tarehe 19 Mei 1967 huko Kraszewo, Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Juni 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Elbag. Kimasomo alibahatika kupata Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa.

Askofu mkuu Urbanczyk Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe
Askofu mkuu Urbanczyk Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe

Tarehe 1 Julai 1997 alianza kutoa huduma yake katika diplomasia ya Kanisa na hivyo kutumwa nchini Bolvia, Slovakia, New Zealand, Kenya na Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, nchini Marekani. Tarehe 12 Januari 2015 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Tume ya Nguvu za Atomu ya Umoja wa Mataifa, AIEA; Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo Barani Ulaya, OSCE, Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO na hatimaye, Mwakilishi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Vienna, Austria. Askofu mkuu mteule Janusz Stanisław Urbańczyk anatarajiwa kuwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu hapo tarehe 6 Aprili 2024, katika Ibada inayotarajiwa kuongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akisaidiana na Askofu Jacek Jezierski wa Jimbo Katoliki la Elblag.

Uteuzi Zimbabwe
02 February 2024, 14:06