Tafuta

Kardinali  Marengo Msimamizi wa Kitume huko Mongolia Kardinali Marengo Msimamizi wa Kitume huko Mongolia 

Vyombo vya habari vya Vatican vyaongeza Kimongolia kwa lugha 51 zilizokuwapo tayari

Kunzia tarehe 31 Januari 2024, Lugha ya Kimongolia inaongezwa katika lugha 51 zilizokuwapo kwenye vyombo vya habari Vatican na kufanya kuwa lugha ya 52.Sasa Mafundisho ya kawaida ya Mfuasi wa Petro yanawezekana kupatikana katika lugha ya kimongolia.

Vatican News.

Radio Vatican - Vatican News sasa pia inazungumza lugha ya Mongolia. Lugha hiyo imeongezwa kwa lugha 51 ambazo tayari zipo, zilizoandikwa na kuzungumzwa, shukrani kwa ushirikiano na Kanisa mahalia. Kwa hakika, Sala zote za Malaika wa Bwana za kila Dominika na Katekesi za Jumatano zitatafsiriwa na kuchapishwa kwenye kurasa za tovuti ya Vatican. “Tunayo furaha katika uwezekano huo mpya kuweza  kusoma Neno la Baba Mtakatifu katika lugha ya kimongolia, alisisitiza Kardinali Giorgio Malengo Msimamizi wa Kitume wa Ulaanbaatar. Ni moja ya matunda ya ziara katika Nchi hiyo ndani ya anga blu linalogusa moyo wa wakatoliki wa Mongolia, lakini hata watu wengi wanaoishi kwa dini nyingine, wamefurahishwa vyema na ushuhuda mkuu wa kibinadamu na wa kiroho wa Baba Mtakatifu Francisko. Maneno yake yaliingia ndani kwa maoni ya walio wengi kwa kuweka juu thamani za utamaduni wetu,” alisisitiza Kardinali Malengo. Sasa mafundisho ya kawaida ya Mfuasi wa Petro yanawezekana kupatikana katika lugha ya kimongolia.  Zana mpya katika huduma ya uinjilishaji, ambao, ni matarajio ya kueleza ukuu wake wote kwa njia za majukaa ya sasa ya mawasiliano.

Ni jambo dogo wakati huo huo ni kubwa

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk Paulo Ruffini kuhusiana na hilo amesema “ Ni jambo dogo, lakini kwetu linaonekana na ni kubwa kama Mongolia ilivyo. Kuzungumza lugha zote, lugha nyingi iwezekanavyo, ni dhamira yetu, huduma yetu. Kufanya hivyo si peke yake, bali pamoja na wale wanaoishi katika maeneo ambapo neno letu linafika, hutufundisha tena umuhimu wa kukabiliana na changamoto pamoja, kutembea pamoja, kufanya “mambo makubwa” katika pambano la kila siku la mambo yanayoonekana kuwa madogo. Hatua kwa hatua.” Dk. Ruffini aidha aliongeza kusema kuwa Kanisani hakuna mkubwa na hakuna mdogo. Kuzungumza Kimongolia pia kutasaidia Kanisa kwa ujumla kugundua tena umuhimu wa mbegu ndogo, ndogo. Tutakachopokea ni zaidi ya kile tutakachotoa. Papa Francisko anarudia mara nyingi, kusema ufunuo wa Mungu unafanyika katika udogo: “Roho huchagua mdogo, daima; kwa sababu hawezi kuingia ndani ya wakuu, wenye kiburi, wanaojitosheleza.”

Kuhimiza ushirika na ushirikano ambao unafungua ukurasa 

Na kwa upande wa Mkurugenzi wa Uhariri wa vyombo vya habari vya Vatican, Dk. Andrea Tornielli  alibainisha kuwa “ Ziara ya  kwenda Mongolia mnamo Septemba 2023 ilikuwa ya ajabu kwa ushuhuda ambao sote tulipokea kutoka katika Kanisa hilo dogo na ambalo bado limeanza, lililojitolea kwa huduma ya wengine. Picha iliyopigwa na ndege hiyo isiyo na rubani na Mrithi wa Petro pamoja na Wakatoliki wote wa nchi hiyo ambao ni 1,500, ilibaki kuwa ya kihistoria. Kama ishara ya tahadhari kwa jumuiya hii ndogo, ili kuhimiza ushirika, shukrani kwa ushirikiano wa Kardinali Marengo, tumeamua kufungua ukurasa wa Habari wa Vatican kwa lugha ya Kimongolia, na hivyo kufanya lugha zinazotumiwa na mfumo wa vyombo vya habari vya Vatican kufikia 52.. Ni heshima kwa ndugu zetu hawa na ushuhuda wao wa kiinjili huko Mongolia.”

Kufanyia kazi mifao ya umoja na makanisa mahalia

Naye  Dk. Massimiliano Menichetti, Mhusika Mkuu wa Vatican Radio- Vatican News  alisema: “Dhamira yetu ni kueneza Injili ulimwenguni kote, kutoa sauti kwa Makanisa mahalia, kusoma ukweli kupitia lenzi ya mafundisho ya kijamii, tusimwache mtu yeyote peke yake. Tulianza kufanyia kazi mpango huu wakati wa ziara  ya Papa kwenda Mongolia, tukiongozwa na msaada wake kwa jumuiya hii ndogo. Tumeanza kuchapisha kwenye tovuti ya Vatican News, lakini baadaye kunaweza pia kuwa na utayarishaji wa sauti. Tunafanyia kazi mifano ya umoja na Makanisa mahalia, kwa usahihi ili kutoa sauti kubwa zaidi kwa matumaini hayo ambayo yanabadilisha ulimwengu.”

Lugha moya ya Kimongolia katika tovuti za Radio Vatican
31 January 2024, 15:15