Tafuta

“Matumizi ya AI hayabatilishi jukumu la uandishi wa habari katika uwanja huo.Ni kwa kugusa mateso kwanza ndipo tunaweza kuelewa upuuzi wa vita.” “Matumizi ya AI hayabatilishi jukumu la uandishi wa habari katika uwanja huo.Ni kwa kugusa mateso kwanza ndipo tunaweza kuelewa upuuzi wa vita.” 

Dk.Ruffini,Papa anatualika katika Akili Mnemba kutazama kiini bila woga wa uvumbuzi kiteknolojia

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa Mawasiliano alizungumzia juu ya ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 58 ya Mawasiliano Duniani uliochapishwa tarehe 24 Januari 2024.Maoni pia yalitoka kwa Rais wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Laziona Mkuu wa ofisi ya mawasiliano ya Jimbo la Roma.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenyekiti wa  Baraza la  Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini, alianza maoni yake kutoka katika tafakari ya Ujumbe wa Papa ili kufafanua mambo ya kipekee ya ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 58 ya Mawasiliano Duniani. Akizungumza na Telepace, alisema: “Papa anaongeza kipande kuhusiana na maana ya kuwasiliana na moyo kwa kukitumia kwenye mada ya akili Mnemba. Nakala inatufafanulia kuwa akili Mnemba haijatenganishwa na kuwa wanaume na wanawake ambao wana moyo. Kwa msingi wa kwamba  kila kitu daima kina uhusiano kati ya watu ambao teknolojia mpya hazitaweza kuchukua nafasi  hiyo na kuzipunguza. Maono ambayo yanahusiana na wanadamu wetu ni kuepuka kuamini kwamba sisi ni wakuu sana hadi kufikia kuchukua nafasi ya Mungu na mwanadamu na mashine.”

Mkuu wa Mawasiliano Vatican aliendelea kusema kuwa kupitia mafunzo hayo kwa wawasilianaji, Papa Francisko anatualika kuangalia kiini cha suala bila woga wowote wa uvumbuzi wa kiteknolojia.  Akili zetu sio za hesabu tu, lakini ni za upendo na hisia, alisisitiza Dk. Ruffini huku akizingatia kwa  madhubuti yaliyokita  katika waraka wa Kipapa. Ni mfululizo wa maswali juu ya mazungumzo na matumizi ya akili Mnemba kama vile ushirikiano wa majukwaa, wajibu wa uhariri wa mwandishi na ufuatiliaji wa vyanzo.” Papa: Mwanadamu hapaswi kuwa chakula cha kukimbizwa na habari , mawasiliano yanabaki kuwa ya kibinadamu. Katika ujumbe wa Siku ya 58 ya Mawasiliano Duniani, Papa Francisko anaakisi  fursa na hatari za akili Mnemba na teknolojia mpya. Na kwa hiyo Ujumbe wa Papa Francisko pia unatukumbusha kutowezekana kutoa habari bila waandishi wa habari katika uwanja ambao hukutana na watu na kuanzisha uhusiano.

Rais wa Chama cha Waandishi wa habari Lazio

Kwa upande wake Guido D'Ubaldo, rais wa chama cha waandishi wa habari cha Mkoa wa  Lazio, Italia, alisema: “Tuna wajibu na jukumu la kusikiliza kabla ya kueleza ukweli. Ni kupitia taaluma yetu​​ tutaweza kudhibiti changamoto ya akili Mnemba kwa kuendelea kusaidia watu kutofautisha kati ya ukweli na habari za kugushi.” Siku zote tunasikiliza sana maudhui  ambayo Papa anahutubia kundi letu” aliongeza D'Ubaldo tena, akikumbuka misa ya Wanahabari iliyoandaliwa kwa mwaka wa tatu mfululizo pamoja na Ofisi ya Mawasiliano ya Kijamii ya Jimbo la ya Roma kwenye hafla hiyo ya kumbukumbu ya Mtakatifu Francis wa Sales. Sherehe hiyo, iliyoongozwa na Monsinyo Baldo Reina, makamu wa Vicariate, iliyofanyika asubuhi tarehe 24 Januari 2024 katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi huko Clivo Argentario juu ya Gereza la Mamertine na kumalizika kwa ziara ya kuongozwa na walinzi wa magereza.

Padre Giulio Abanese ni fursa ya kuomba mtakatifu mlinzi wetu

Kuhusiana na maadhimisho ya Mtakatifu Francis wa Sales ambaye ni msimamizi wa Waandishi wa habari na waariri, viziwi na vipofu, Padre Giulio Abanese mhusika wa muundo wa Mawasiliano, jimbo la Roma alisema kuwa: “ Ni Fursa ya kuomba kwa maombezi ya mtakatifu mlinzi wetu. Zaidi ya hayo, tumethibitisha dhana thabiti ya uwajibikaji katika kutoa sauti kwa wale ambao hawana sauti na kusimama na wale ambao mara nyingi ni waathiriwa wa dhuluma na ukandamizaji katika karibu pande zote. Ni wazi kwamba hatuzungumzii juu ya taaluma rahisi. Kama Papa Francisko hivi karibuni alivyokumbuka, kuwa huu ni wito wa maandamano ili kuthibitisha ukweli kwa ajili ya ujenzi wa wema wa wote.”

Maoni Kutoka kwa Dk Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican
25 January 2024, 16:33