Tafuta

Kanisa la Huruma ya Mungu huko China. Kanisa la Huruma ya Mungu huko China. 

China:Askofu wa Jimbo jipya la Weifang amewekwa wakfu wa kiaskofu

Padre Antonio Sun Venjun aliteuliwa na Papa Francisko tarehe 20 Aprili 2023 na Papa alikuwa amechagua jimbo jipya baada ya kuondoa usimamizi wa kitume huko Yiduxian.Na maamuzi yote mawili yamewekwa wazi 29 Januari 2024 katika siku ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu wa Askofu huyo.

Vatican News

Jimbo jipya la Weifang lilianzishwa nchini China na Jumatatu tarehe 29 Januari, 2024 mchungaji wake mpya aliwekwa wakfu, Askofu Antonio Sun Venjun. Maamuzi yote mawili kuhusu Jimbo Jipya na uteuzi wa mchungaji wake wa kwanza ni wa mwezi Aprili 2023, lakini taarifa imejulikana  katika siku ya kuwekwa wakfu kwa askofu huyo. Uteuzi huo ulifanyika ndani ya mfumo wa Makubaliano ya Muda kati ya Vatican  na Jamhuri ya Watu wa China. Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, tunasoma kuwa: “Katika nia ya kuendeleza uchungaji wa kundi la Bwana na kuhudhuria kwa ufanisi zaidi kwa manufaa yake ya kiroho tarehe 20 Aprili 2023, Papa Francisko aliamua kuondoa China usimamizi wa kitume wa Yiduxian, ambalo lilichaguliwa tarehe 16 Juni 1931 na Papa Pio XI kwa kupata eneo kutoka katika Usimamizi wa kitume wa Zhif (Leo hii ni jimbo la Yantai) na wakati huo huo kuweka hadhi ya  Jimbo jipya  la Weifang, linalopakana na  Jinan, Walaya ya Shandong, lenye makao ya  uaskofu katika Kanisa Kuu la Kristo Mfalme, lililoko Quinngzhou, mji wa Weifang.”

Askofu Mpya alizaliwa 1970

Askofu mpya Antonio Sun Wenjun aliyewekwa wakfu Jumatatu tarehe 29 Januari, alizaliwa Novemba 1970. Alisoma katika Seminari ya Sheshan mjini Shanghai kuanzia mwaka 1989 hadi 1994. Alipewa daraja la Upadre mnamo mwaka 1995 katika parokia ya Xishiku mjini Beijing. Baadaye alifanya huduma ya kichungaji huko Shandong kuanzia 2005 hadi 2007. Kati ya 2007 na 2008 alibaki Ireland kuendelea na mafunzo yake. Baadaye alirudi Weifang na kuendelea na huduma yake hapo.

Katika taarifa tunasoma kuwa: “Mipaka ya kikanisa ya Jimbo jipya itajumuisha maeneo yafuatayo: vitongoji vya Weicheng, Hanting, Fangzi na Kuiwen; kanda nne za maendeleo ya manispaa; kata za Linju na Changle; miji ya Qingzhou, Zhucheng, Shouguang, Anqiu, Gaomi na Changyi. Badala yake, sehemu ya mashariki ya vitongoji vya Laiwu imeunganishwa kuwa jimbo kuu la Jinan; huku vitongoji vya Boshane ya Linzi, wilaya ya Guangrao, Ndondi na Gaoquing vikiunganishwa kuwa Jimbo la  Zhoucun.” Ndivy tunasoma katika taarifa iliyotolewa. Eneo la Jimbo jipya Weifang linalingana na lile la mji mkuu wa Weifang, lenye jumla ya eneo la 16,167.23 km na wakazi 9,386,705, ambao takriban elfu 6 ni Wakatoliki, wanaohudumiwa na mapadre 10 na watawa 6.

Misa ya kuwekwa wakfu

Askofu Giovanni Fang Xingyao wa Linyi, aliongoza Ibada ya Misa ya kuwekwa wakfu kwa Askofu huyo ambapo Maaskofu wengine wanne wa Kichina, mapadre 44 na waamini zaidi ya 330 na walei walishiriki katika liturujia hiyo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides, limebanisha kuwa waamini wakatoliki wa jimbo jipya la Waifang walishukuru. Aidha Fides inasisitiza kwamba historia ya Jimbo la Weifang, Jimbo la Kitume la zamani la Yiduxian tangu 1931, linahusishwa na utume wa uinjilishaji unaofanywa katika nchi hiyo na Wafransiskani  wa Ufaransa. Jimbo hilo halikuwa na askofu tangu 2008. Katika kipindi cha miaka ya nafasi ya kiti cha uaskofu, jumuiya ya kikanisa ya kijimbo iliendelea kutembea kwa umoja na kudhihirisha ufuasi wake wa Kristo na shauku ya kutangaza Injili, kwa ushirika na Papa na Kanisa la  Roma.

Watawa wanajikita na uchungaji na uhuishaji wa kijamii

Katika jimbo hilo  Masista wa Shirika la Mkingiwa linafanya kazi na wapo na kujikita sana katika uchungaji wa parokia na katika uhuishaji wa kazi za kijamii. Mnamo mwaka 2005 baadhi yao walishiriki katika Mkutano wa Tume ya Kikatoliki ya China katika  Kazi za Hisani na Huduma za Kijamii, yenye kauli mbiu: “Kujali Jamii.” Katika hafla hiyo Sr  Zong Huaiying alikuwa amesisitiza kwamba licha ya ugumu na uhaba wa rasilimali, bado ilikuwa inawezekana kufanya kazi nzuri ya usaidizi wa kijamii, kwa neema za Mungu.” Taarifa kutoka Fides inahitisha.

Jimbo jipya nchini Jipya na kuwa na Askofu Mpya
29 January 2024, 15:33