Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 27 Januari 2024 ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 27 Januari 2024 ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba la kutaka kung’atuka kutoka madarakani.  

Askofu Msaidizi Methodius Kilaini Ameng'atuka Kutoka Madarakani Bukoba

Askofu Msaidizi Methodius Kilaini alizaliwa kunako tarehe 30 Machi, 1948 huko Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, alipewa daraja takatifu ya Upadre kunako tarehe 18 Mach 1972 na Kardinali Agnelo Rossi. Na kunako tarehe 22 Desemba, 1999, Mtakatifu Yohane Paulo wa pili, alimteuwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam na hivyo kuwekwa wakfu kunako tarehe 18 Machi, 2000 na Kardinali Polycarp Pengo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 27 Januari 2024 ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu Msaidizi Methodius Kilaini alizaliwa kunako tarehe 30 Machi, 1948 huko Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, alipewa daraja takatifu ya Upadre kunako tarehe 18 Mach 1972 na Kardinali Agnelo Rossi. Na kunako tarehe 22 Desemba, 1999, Mtakatifu Yohane Paulo wa pili, alimteuwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam na hivyo kuwekwa wakfu kunako tarehe 18 Machi, 2000 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam. Kabla ya uteuzi wake kuwa Askofu msaidizi, alikuwa ni Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na amewahi kufundisha Historia ya Kanisa, Seminari kuu ya Falsafa, Ntungamo, Bukoba.

Askofu Methodius Kilaini ang'atuka kutoka madarakani
Askofu Methodius Kilaini ang'atuka kutoka madarakani

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, tarehe 5 Desemba, 2009, alimhamisha Askofu msaidizi Metodius Kilaini kutoka Jimbo kuu la Dar es Salaam kwenda kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Tanzania.Tarehe 1 Oktoba 2022 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Bukoba, utume ambao umefikia ukomo wake tarehe 27 Januari 2024, siku ambayo Askofu Jovitus Francis Mwijage wa Jimbo Katoliki la Bukoba, alipowekwa wakfu na kusimikwa rasmi kuwa ni Mchungaji mkuu wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Askofu mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga wa Jimbo kuu la Mbeya, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ametumia maadhimisho haya kuwatangazia watu wa Mungu nchini Tanzania juu ya kung’atuka kwa Askofu msaidizi Kilaini kutoka madarakani. Kimsingi, Askofu Methodius Kilaini amelitumikia Kanisa katika kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu kama Padre kwa miaka 51 na kama Askofu miaka 23!

Askofu Kilaini
27 January 2024, 14:04