Tafuta

2023.12.07 Waliomba katika Tamasha la Shule ya Magnificat ya Yerusalemu katika Kanisa la Bikira Maria huko Trastevere,Roma. 2023.12.07 Waliomba katika Tamasha la Shule ya Magnificat ya Yerusalemu katika Kanisa la Bikira Maria huko Trastevere,Roma. 

Wanafunzi wa Magnificat katika “Usiku wa Amani:”tunaweza kuishi pamoja katika Nchi Takatifu

Tamasha la amani katika Mashariki ya Kati,miezi miwili baada ya kuzuka kwa mzozo wa kivita kati ya Israel na Hamas,katika Basilica ya Mtakatifu Maria,Trastevere,Roma iliyohamasishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.Wahusika wakuu walikuwa ni wanafunzi na walimu saba wa Shule ya Muziki ya Yerusalemu,Wayahudi,Waislamu na Wakristo.Patriaki Pizzaballa:kusikiliza pamoja kitu kizuri,kilichofanywa pamoja ni mchango wa kuokoa nuru.

Alessandro Di Bussolo na Angella Rwezaula – Vatican

Maombi ya ushuhuda katika muziki kwamba inawezekana kuishi pamoja katika nchi yenye mateso, Wayahudi, Waislamu na Wakristo. Na hakuna mawasiliano bora kuliko ushuhuda. Kusikiliza kwa pamoja jambo zuri, lililofanywa pamoja, ambalo ni mchango katika kuokoa taa ya nchi iliyogawanyika, Israel na Palestina, katika vita ambayo imezidisha migawanyiko zaidi, na kuomba kitendo cha matumaini usitishaji mpya wa mapigano, ambapo ni kukomesha vifo na uharibifu. Ni mawaidha yaliyosikika wakati wa Tamasha la Muziki lenye kauli mbiu: “Usiku wa Amani wa Shule ya Magnificat ya Yerusalemu,” Nchi Takatifu. Tukio hilo lilifanyika katika mkesha wa Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, jioni tarehe 7 Desemba  2023, miezi miwili baada ya kuzuka kwa vita Nchi Takatifu, ambalo tamasha lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Chuo cha Kipapa cha Maisha, kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, katika Basilica ya Mtakatifu Maria, Trastevere jijini Roma.

Wakati wa kuimba katika Tamasha la Magnificat, kikundi kutoka Yerusalemu
Wakati wa kuimba katika Tamasha la Magnificat, kikundi kutoka Yerusalemu

Sauti zilisikiza za Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriki wa Kilatini wa Yerusalemu na Padre Gabriele Romanelli, paroko wa Kanisa la Kilatini la Familia Takatifu huko Gaza . Shule hiyo, inayoendeshwa na Usimamizi wa Nchi Takatifu na kuongozwa na Ndugu Mdogo Alberto Iuan Pari, ilitoa tamasha huko Jijini Roma kama sehemu ya mpango wa amani kati ya miji hiyo mawili inayokinzana. Shule hiyo iliyounganishwa na Chuo cha Muziki cha Vicenza nchini Italia, imejengwa katika Jiji la Kale la Yerusalemu tangu 1995 na inatoa kila mwaka fursa ya kutambulishwa kwa muziki na kuwasindikiza hadi wafikie diploma ya Muziki, kwa wanafunzi vijana wa Kiyahudi, Waislamu na Wakristo, wakiongozwa na walimu wengi wa Kiyahudi, pamoja na baadhi ya Wakristo. Na inakuwa, pamoja na wanafunzi wake 220, Wakristo asilimia 70, Waislamu 20 na Wayahudi 10, fursa yenye matunda kwa majadiliano na mazungumzo kati ya dini za Ibrahimu katika Nchi Mtakatifu.

Wanafunzi wakicheza ala zao (Violini)
Wanafunzi wakicheza ala zao (Violini)

Tamasha hilo lilifunguliwa kwa usomaji wa Zaburi ya 122, inayojikita kutazama  jiji la Yerusalemu, ambalo sote tunaalikwa kuomba  amani, iliyosomwa na Andrea Monda, mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano na kumalizika kwa Wimbo wa Magnificat. Salamu za kwanza zilikuja kupitia video kutoka kutoka Nchi  Takatifu kwa  Patriaki  wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, ambaye alikumbuka jinsi mzozo mpya katika Mashariki ya Kati umeongeza hisia za umbali, za uadui kati ya Waisraeli na Wapalestina kwa njia ya kina sana, labda hata alisema  chuki katika hali fulani. Ni ngumu sana kuongea sisi kwa sisi, hatusikilizani. Katika usiku wa wakati huu, hata hivyo, kuna uhaba wa nuru kwa watu, taasisi, harakati na vyama ambao hujaribu kufuata namna ya  kusuluhisha migogoro lakini, licha ya matatizo makubwa, wanafanya kitu kizuri.” Na muziki, ambao hauitaji tafsiri, kila mtu anauelewa, ni njia rahisi, nzuri, thabiti ya kufanya kitu pamoja, hasa katika wakati huu ambao uhusiano wetu unateswa na vurugu nyingi.” Alisema Patriaki. Kwa njia hiyo  Noeli inayokaribia ilimtia moyo Kardinali Pizzaballa kwa uhakika kwamba “tutaweza kuanza tena, na hapa pia, katika jumuiya ya Wakristo, kati ya Wayahudi, kati ya Waislamu, kati ya Waisraeli na Wapalestina, kutakuwa na watu wengi ambao tutakuwa pamoja nao kuweza kuungana tena kwa njia mpya, kwa mitazamo mipya na mizuri, mahusiano yetu.”

Ndugu wadogo katika Tamasha la Shule ya Magnificat
Ndugu wadogo katika Tamasha la Shule ya Magnificat

Baada ya wimbo wa kwanza ulioongozwa na mkurugenzi wa shule, Ndugu Mdogo Alberto Iuan Pari,  wa: “Ave Maria” katika Masifu ya  kwanza ya Maadhimisho ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa wa Dhambi ya Asili, naye Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini, aliwashukuru wanafunzi saba waliohudhuria, pamoja na mapadre wawili walioandamana nao, kwa sababu wao ni  nuru. “Tunatembea kwenye bonde lenye giza. Na ushuhuda wenu, wa kuimba kwenu, pamoja ni nuru. Ni wimbo mpya. Unatayarisha njia ya amani jangwani.” Alisisitza Mkuu wa baraza la Kipapa la Mawasiliano kuwa  ni wimbo mpya kwa sababu “katika ulimwengu uliogawanyika unashuhudia kuwa wimbo, katika umoja wa sauti, uwezekano wa umoja wa mioyo. Uwezekano wa kugundua tena, licha ya kila kitu, ukweli unaotuunganisha, ule wa kuwa sisi sote ni kaka na dada. Na pia thamani ya ukimya na kusitisha, bila  kufanya hivyo kusingekuwa na muziki, kusingekuwa na mazungumzo. Na Mungu anajua ni kiasi gani kuna haja ya mapumziko leo katika dini ya silaha, maneno, na mawazo ya kuchanganyikiwa. Mungu huongea hata kwa kutulia. Na katika mapumziko wimbo mpya unaibuka.” Kwa kuhimtimisha, Dk. Ruffi alisema: “Wimbo wenu huwatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao. Unatukumbusha umuhimu wa umoja. Unawasha matumaini. Tutawaombea ninyi  na kwa ajili ya amani.”

Nyimbo za  tamasha

Tamasha hilo liliendelea na kipande kingine cha  muziki wa Bach kwa ala mbili (violini) na mchango wa Ilaria Della Bidia, mwimbaji wa sauti ya juu wa pop, akisindikizwa na Mwalimu Attilio Di Giovanni, ambaye wasikilizaji wa radio ya "Il roarito del coniglio" wanamfahamu vyema na wimbo wa Kiyahudi, Kiarabu na “Dolce è sentire” yaani "Usikivu mtamu" wa Mtakatifu Francis wa Asisisi. Baada ya  wimbo wa "Panis Angelicum", wimbo wa mwisho ulikuwa kutoka Zaburi 18: "Mbingu kubwa zinaimba" na Benedetto Marcello. Pia katika viti vya mbele alikuwapo Kadinali Fernando Filoni, Mkuu wa Shirika la Kaburi Takatifu.

Ushuhuda wa Paglia 

Salamu zingine zilizopishana na vipande vya muziki wa  tamasha, zilikuwa kama  vile kutoka kwa Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, ambaye alikumbuka jinsi ambavyo Basilica ya Mtakatifu Maria huko Trastevere, ni mahali pa kwanza pa ibada zote zinazojitolea kwa ajili ya  Maria, hapo Roma, kijana wa miaka 14 “umri wao zaidi au chini, ambaye aliondoka huko Nazareti na kujiunga na binamu yake Elizabeth na kuimba wimbo Magnificat yaani wa sifa ya Kumtukuza Mungu. “Tunajiunga katika ndoto ya kikundi cha vijana kuimba Magnificat kwa ajili ya  amani na kukutana,”aliongeza.  

Ushuhuda wa Marco Impagliazzo

Kisha kulikuwa na  ushuhuda wa Bwana Marco Impagliazzo, rais wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambaye alisisitiza jinsi ambavyo tunahitaji ishara za amani, upatanisho na siku zijazo, ambazo haziwezi kuonekana katika giza la vita na ugaidi. “Tukikutana hapa ambapo huwa tunaomba amani hutuambia kwamba kuna dalili ya amani, hata ikiwa bado tunaona mateso mengi. Ishara ya urafiki wenu, ya ushirikiano wenu, inatugusa na inatupa matumaini.” Alisema.

Tamasha la Shule ya Magnificat
13 December 2023, 14:39