Tafuta

Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher 

Askofu Mkuu Gallagher,Vita katika Mashariki ya Kati:mazungumzo yanahitajika haraka iwezekanavyo

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa katika mahojiano na gazeti, la Sette kila Juma,anaakisi mzozo unaoendelea Nchi Takatifu na masuala ya kimataifa ya sasa hasa kuaniza mzozo wa Ukraine hadi mzozo wa UN na jukumu la China.

Vatican News

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa katika mahojiano maalum yaliyochapishwa tarehe  23 Desemba 2023  na gazeti la kila Juma la Jimbo la Roma,( la Sette) kwenye kiambatisho cha Gazeti la Avvenire, alisema: “Tulishuhudia ukatili wa kutisha wa Oktoba 7, ambao hakuna uhalali wowote, lakini pia tulishuhudia kilichotokea baadaye. Mazungumzo ni muhimu haraka iwezekanavyo. Tunatumaini kuwa vita hivi havitazua migogoro mingine ya kidini na havitarefushwa kwani maisha ni sehemu nyingine za dunia.” Askofu Mkuu alibanisha hayo kwa kuakisi mzozo unaoendelea wa Mashariki ya Kati na masuala motomoto zaidi katika anga la kimataifa, kuanzia vita vya Ukraine, mgogoro wa Umoja wa Mataifa hadi jukumu la China.

Kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine kwa takriban miaka miwili, Askofu Mkuu Gallagher alieleza wasiwasi mkubwa kuwa: “ni mkwamo huku kukiwa na wahanga wa pande zote mbili. Tunaendelea kupatikana ili kuwezesha upatanishio. Tunachoweza kufanya ni kusaidia misaada ya kibinadamu. Tunaendelea kutumia ofisi zetu nzuri kwa ajili ya kubadilishana wafungwa na kujaribu kuwezesha mpango wa kuwarejesha makwao watoto wa Kiukraine. Ni lazima tukubali kwamba matokeo ya jitihada hizi ni ya kawaida hata kama ni ngumu. Lakini tunaendelea kufanya kazi.” Kuhusu uwezekano wa ziara ya Papa Francisko, Askofu Mkuu Gallagher alisema kwamba: “Papa bado yuko wazi sana kwenda Ukraine na Urussi. Itakuwa ishara ya hatua ya mbele katika kutuliza. Kwa bahati mbaya, hatufikirii itakuwa lini, lakini tunatumaini kuwa inaweza kufikiwa. Ni wazi, inategemea pia pande zinazozozana. Ninaamini kwamba ziara ya Papa ingethaminiwa na wote wawili.” Alisema

Askofu mkuu Gallger  pia alisisitiza juu ya mgogoro mkubwa wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa. Mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yanatoa mchango muhimu katika maeneo ya vita lakini katika ngazi ya kisiasa na kidiplomasia mgogoro huo ni mkubwa. Marekebisho yanahitajika, ambayo yamezungumzwa kwa miaka mingi hasa wa Baraza la Usalama, na sasa kuna imani kubwa zaidi. Pengine ni suala la kuimarisha jukumu la Baraza Kuu, la kupanua wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza, na pengine kubadilisha kanuni zake. Vatican inaamini kwamba vyombo hivi vinapaswa kushughulikia zaidi masuala muhimu ambayo yanahusu ubinadamu kweli.

Askofu Mkuu Gallagher na suala la mzozo wa Mashariki ya Kati na pia Ukraine
23 December 2023, 18:18