Tafuta

2023.12.27  Kardinali Krajewski akiwa Nazareth hawa ni mamonaki wa Nazareth. 2023.12.27 Kardinali Krajewski akiwa Nazareth hawa ni mamonaki wa Nazareth. 

Vatican,Kard.Krajewski amehitimisha utume Nchi Takatifu

Kardinali Konrad Krajewski,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapapa la Huduma ya Upendo amehitimish Utume wa Vatican Nchi Takatifu.Baba Mtakatifu Francisko alimtuma,huko ili kuwasindikiza Wakristo wa Jumuiya ya Nchi Takatifu kuadhimisha Siku Kuu ya Noeli katika kipindi hiki ambacho inajikuta ndani ya mgogoro wa kivita kati ya Israel na Palestina.

Konrad Krajewski

Akirejea kutoka katika utume wake katika Nchi Takatifu, kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, Kardinali Krajewski ameandika tafakari yake akiakisi juu ya uzoefu alioishi kwenye mipaka ya vita huko Gaza ambapo anasema katika Baba Yetu, Yesu anasema: “Mapenzi yako yatimizwe na Ufalme wako ufike,” wakati mwanadamu anafuata  mapenzi yake na malengo yake tu mateso na migogoro mara nyingi hutokea." Ifuatayo ni tafakari ya uzoezo huo na ushuhuda wa Kardinali Krajewski kuwa: "Nilikwenda kwenye Nchi Takatifu kwa imani na sala, mahali ambapo vita vinaendelea, ambapo kuna chuki, kuna kulipiza kisasi, mahali ambapo mtu anaua mwingine, ambako kuna ukosefu wa maji, chakula, na ambapo hakuna umeme.

Kardinali Krajewski na Patriaki Pizzaballa wakati wa Noeli 25 Desemba
Kardinali Krajewski na Patriaki Pizzaballa wakati wa Noeli 25 Desemba

Hata wakati wa Noeli, siku takatifu zaidi kwetu, hawakuacha kupigana, kuua, huko Ukraine kama hata  Ukanda wa Gaza. Nilifika katika nchi hii nikiwa na silaha za hali ya juu zaidi ulimwenguni, yaani, imani na sala, ambazo zinaweza kufanya isogee milima kila wakati na kwa hivyo kumaliza migogoro ... Lakini kwa nini sio hivvyo?


Nimekwenda sehemu zote ambapo Yesu aliishi. Nimekuwa Nazareti, Bethlehemu, nimefika mahali aliposulubishwa, akauawa kisha alipofufuliwa, ninajiuliza: “Bwana, mbona hakuna amani? Unataka amani.” Nimefikiria kila mara juu ya sala hii: “Utuokoe, Bwana, kutoka katika maovu yote, utupatie amani katika siku zetu” ... Basi kwa nini usitupatie amani katika siku zetu?

Kardinali Krajewski wakati wa misa tarehe 26 Desemba huko Nazareth
Kardinali Krajewski wakati wa misa tarehe 26 Desemba huko Nazareth

Sisi watu labda tumejiweka mahali pa Mungu na tunataka kuamuru, kulaani lakini tunafanya bila huruma, bila upendo. Labda hii ndiyo sababu hakuna amani, kwa sababu hatusujudu tena mbele za Mungu, mbele ya fumbo. Jana ilikuwa sikukuu ya Mtakatifu Yohane Mtume, alifika kwenye kaburi la Yesu na akainama ili aweze kuingia, aweze kuona kuwa mwili wake haupo, kwamba amefufuka. Lakini leo hatuinami tena, hata kama milango ya hapa katika Nchi Takatifu inatuambia kwamba tunapaswa kufanya hivyo ili kuelewa siri ya Mungu, kuelewa upendo wake, huruma yake, kuishi sawasawa na mantiki ya mafundisho ya Yesu, yaani kwa mantiki ya Injili.

Kardinali Karajewski akiwa katika kituo cha watoto Yatima huko Betlehemu
Kardinali Karajewski akiwa katika kituo cha watoto Yatima huko Betlehemu

Ninamshukuru Bwana kwa kuishi siku hizi katika Nchi Takatifu na kuanza kuelewa siri ya Mungu, sala ya Baba yetu, sala ambayo Yesu alitufundisha, inasema, “Mapenzi yako yatimizwe, Bwana”", sio yangu, kwa sababu tangu  mapenzi yangu kuna vita, kuna vifo vingi.” Ufalme wako uje,” si wetu, ufalme wa uharibifu ni wetu. “Jina lako litukuzwe, sio langu, jina langu linapotakaswa mimi ni hatari kwa wengine. Baada ya Baba Yetu, kuhani anasema: |Ee Bwana, utuokoe na mabaya yote, utupatie amani siku zetu.” Matumaini yangu ni kwamba amani istawi kweli katika mioyo ya wanadamu.

28 December 2023, 15:59