Tafuta

Papa na Wajumbe wa Tume ya Papa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto . Papa na Wajumbe wa Tume ya Papa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto .  (Vatican Media)

Ulinzi wa watoto,ufadhili wa mipango ya ulinzi Kusini mwa ulimwengu

Tume ya Kipapa imetangaza kutenga kiasi cha euro elfu 230 kusaidia mipango mbalimbali ya ulinzi katika maeneo yaliyo hatarini zaidi.Rasilimali zinatokana na Mfuko wa Kumbukumbu,ulioanzishwa na shirika la Vatican mwaka 2023.O'Malley:ni muhimu kwamba kila mahali katika Kanisa kuna rasilimali na wafanyakazi muhimu kutekeleza na kudumisha ulinzi imara katika ngazi zote."

Vatican News

Katika hafla ya mkutano wa hivi karibuni wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, Euro elfu 230 zilitengwa kusaidia mipango mbalimbali ya ulinzi katika nchi maskini zaidi. Rasilimali hizo zinatoka katika  Mfuko wa Kumbukumbu, ulioanzishwa na Tume hiyo mnamo 2023 ili kujenga uwezo wa ulinzi katika Kanisa la Kusini mwa Ulimwengu.

Mpango wa mfuko wa Kumbukumbu

Madhumuni ya  Kumbukumbu ya Mpango  huko ni kusaidia na kushirikiana na Makanisa mahalia ulimwenguni kote katika mafunzo na kuimarisha uwezo wa kinga na ulinzi kwa watoto na watu wazima walio katika mazingira magumu. Usaidizi huo unazingatia maeneo matatu: kusindikiza waathirika na walionusurika, utekelezaji wa sera za kuzuia kupitia uundaji wa programu za kuzuia, utekelezaji wa sera za uzuiaji kupitia uundaji wa miongozo na kanuni za maadili, na kujibu ipasavyo na kwa haraka tuhuma za unyanyasaji kwa mujibu wa sheria za Kanisa.

Baadhi ya mipango ya ulinzi

Mfuko wa Kumbukumbu unasimamiwa na Tume kwa msaada mkubwa wa Baraza la Maaskofu wa Italia. Miongoni mwa mipango iliyoidhinishwa kusaidia ulinzi: Nchini Paraguay, fedha zitaruhusu Kituo kipya cha Ulinzi huko Asuncion kwa kuajiri mtu aliyeteuliwa kufanya uhakiki wa kimfumo wa sera na desturi zinazotumika sasa katika Kanisa lote, ikijumuisha huduma za kuripoti na usaidizi, ili kuona ni wapi maboresho yanapaswa kufanywa. Nchini Panama, fedha hizo zitatoa programu ya mafunzo kwa viongozi wa makanisa kusasisha miongozo yao na kulinda na kuunda mfumo wa kusindikiza waathiriwa na walionusurika.

Kard.O'Malley: muhimu kuhakikisha rasilimali na wafanyakazi

Kisha kuna fedha nyingine kwa ajili ya Jumuiya ya Wanachama wa Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki (Amecea), ambayo inashughulikia nchi 13 za Afrika Magharibi na ambayo itatoa mfululizo wa warsha katika kipindi cha miaka miwili ijayo kwa uongozi wa Kanisa na watendaji. Pia nchini Mauritius kuna fedha ya kufadhili semina ya kwanza ya ulinzi kwa uongozi katika Kanisa la Afrika linalozozungumza Kifaransa. Semina hiyo itajumuisha warsha kuhusu masasisho ya hivi karibuni ya kanuni za kanisa, jukumu na wajibu wa uongozi katika kuwasaidia waathiriwa na uundaji wa mifumo ya ulinzi na miundo ndani ya makanisa mahalia. Kardinali Seán O'Malley, rais wa Tume, hiyo alisema: “Ni muhimu kwamba sehemu zote za Kanisa ziwe na rasilimali na wafanyakazi muhimu ili kutekeleza na kudumisha ulinzi thabiti katika ngazi zote za Kanisa.”

22 December 2023, 11:05