Tafuta

Patriaki Bartolomeo wa kwanza katika ujumbe wake kwa Sherehe za Noeli kwa Mwaka 2023 anakazia kuhusu: Umuhimu wa kupambana kufa na kupona ili kutafuta, kulinda na kudumisha amani duniani. Patriaki Bartolomeo wa kwanza katika ujumbe wake kwa Sherehe za Noeli kwa Mwaka 2023 anakazia kuhusu: Umuhimu wa kupambana kufa na kupona ili kutafuta, kulinda na kudumisha amani duniani.  

Ujumbe wa Patriaki Bartolomeo wa Kwanza Kwa Noeli 2023: Amani Duniani

Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli katika ujumbe wake kwa Sherehe za Noeli kwa Mwaka 2023 anakazia kuhusu: Umuhimu wa kupambana kufa na kupona ili kutafuta, kulinda na kudumisha amani duniani. Wakristo katika Sherehe ya Noeli wanakumbuka kuzaliwa kwa Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, Mkombozi na Mfalme wa Amani. Kimsingi dini Ulimwenguni zinapaswa kuwa ni chombo cha umoja, upendo na mshikamano wa kweli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mtakatifu Yohane XXIII katika Waraka wake wa Kitume “Pacem in terris” yaani “Amani Duniani.” Kuhusu kuimarisha amani kati ya watu wote katika ukweli, haki, upendo na uhuru” anasema amani duniani, ambayo watu wa nyakati zote waliitamani kwa hamu kubwa sana, haiwezi kujengwa wala kuimarishwa isipokuwa kwa kulinda kitakatifu utaratibu uliowekwa na Mungu. Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli katika ujumbe wake kwa Sherehe za Noeli kwa Mwaka 2023 anakazia kuhusu: Umuhimu wa kupambana kufa na kupona ili kutafuta, kulinda na kudumisha amani duniani. Wakristo katika Sherehe ya Noeli wanakumbuka kuzaliwa kwa Kristo Yesu, Mwana wa Mungu, Mkombozi na Mfalme wa Amani.Kuna hatari kwamba, binadamu daima anateleza na kuangukia kwenye vita, migogoro na mipasuko ya kijamii, changamoto na mwaliko kwa watu wa Mungu, kukesha na kuendelea kuwa macho, ili matatizo na changamoto za ulimwengu mamboleo ziweze kupatiwa ufumbuzi wake kwa njia ya majadiliano katika ukweli na uwazi. Hii ndiyo dhamana na wajibu mkubwa wa dini yoyote duniani ni kuhakikisha kwamba, inalinda na kudumisha: haki, amani na maridhiano duniani.

Amani Duniani kwa watu wenye mapenzi mema!
Amani Duniani kwa watu wenye mapenzi mema!

Inasikitisha kuona kwamba, baadhi ya dini zinashutumiwa kuwachochea waamini wake kuwa na misimamo mikali ya kidini na kiimani, kuanzisha vita na ghasia kwa jina la Mwenyezi Mungu. Kimsingi dini ulimwenguni zinapaswa kujikita katika nguvu ya amani, upendo na mshikamano; haki na upatanisho. Haya ni mambo muhimu sana yanayoitambulisha dini sehemu mbalimbali za dunia. Kumbe, misimamo mikali ya kidini ni kinyume kabisa cha asili ya dini ambazo zinapaswa kuwa ni kiungo cha umoja na ushirika kati ya binadamu, ili kwa pamoja waweze kusimama kidete kupambana kutafuta na kudumisha: haki, amani na maridhiano sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. Wakristo waendelee kujitambulisha kuwa ni wadau wakuu katika huduma ya maendeleo fungamani ya mazingira. Uelewa wa Kikristo katika changamoto hizi uwasaidie Wakristo kuwa na uelewa mpana kuhusu amani kama zawadi kutoka kwa Kristo Mfufuka inayowataka watu wa Mungu kushiriki kikamilifu. “Yesu akawaambia tena, “Amani kwenu! Kama vile Baba alivyonituma mimi, nami nawatuma nyinyi.” Yn 20:21. Upendo kwa adui ndio upya wa mafundisho ya Kristo Yesu.

Kumbukizi ya Miaka  75 ya Tamko la Haki za Binadamu Duniani
Kumbukizi ya Miaka 75 ya Tamko la Haki za Binadamu Duniani

Kuwapenda adui na kuwaombea ni njia ya amani na wala si vita na kinzani. Kumbe, amani inapatikana kwa njia ya amani na wala si “Jicho kwa jicho wala jino kwa jino; bali majadiliano katika ukweli na uwazi; upendo, msamaha na upatanisho. Haya ni mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele cha kwanza, sanjari na kulinda pamoja na kudumisha haki msingi za binadamu. Tamko la Haki za Binadamu Duniani (The Universal Declaration of Human Rights, 1948, UDHR) lilitiwa mkwaju tarehe 10 Desemba 1948 na Mataifa yalikubaliana kulinda haki msingi za binadamu hasa haki ya kuishi ambayo ndiyo msingi wa haki nyingine zote. Tamko hili la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2023 linaadhimisha Miaka 78 tangu kuridhiwa kwake na Jumuiya ya Kimataifa. Tamko hili ni matokeo ya tafakari ya kina iliyofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa kuhusu: Athari zilizokuwa zimesababishwa na Vita kuu ya kwanza na ile ya Pili ya dunia; ambapo kuna watu wengi walipoteza maisha na mali; utu na heshima yao vikawekwa rehani. Walitaka kuweka kanuni msingi ambazo zimengefuatwa na Jumuiya ya Kimataifa. Hizi ni haki ambazo zinafumbatwa katika uhuru, haki na amani duniani. Huu ni urithi wa binadamu wa nyakati zote na mahali pote bila ubaguzi, kwani zinapata chimbuko lake kutoka kwa binadamu mwenyewe aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na kwamba ni sehemu ya asili ya binadamu.

Kristo Yesu ni Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu
Kristo Yesu ni Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu

Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli anakaza kusema, amani ya kweli inasimikwa katika uhuru na haki msingi za binadamu. Ni katika muktadha huu, dini zina mchango mkubwa katika kutafuta, kukuza na kuimarisha amani duniani. Hii ni changamoto inayojikita katika ujenzi wa utamaduni wa amani, mshikamano wa upendo na ujenzi wa udugu wa kibinadamu, unaowasukuma watu wote kuheshimiana na kuthaminiana kwa sababu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na kamwe binadamu asiwe ni tishio kwa binadamu mwenzake wala adui!

Ujumbe wa Noel 2023
26 December 2023, 11:24