Tafuta

Papa wakati wa ziara yake ya kitume huko Ureno katika fursa ya Siku ya XXXVIII ya Vijana alikutana na Vijana wa Scholas Occurrentes. Papa wakati wa ziara yake ya kitume huko Ureno katika fursa ya Siku ya XXXVIII ya Vijana alikutana na Vijana wa Scholas Occurrentes.  (Vatican Media)

Scholas Occurrentes tuzo kwa kujitolea kwa ajili ya haki za binadamu

Harakati ya Elimu iliyoundwa na Papa Francisko imepokea Tuzo ya“Juan Antonio Carrillo Salcedo,”Chuo Kikuu cha Seville kwa ajili ya ulinzi wa haki za binadamu. Tangu kuundwa kwake,imezindua mipango ulimwenguni kote ya kupambana na unyanyasaji,uonevu,unyanyasaji mtandaoni,ufisadi na unyonyaji.Corral,Rais wake alisema:“Wasomi wanatetea ukweli kuwa na maisha yenye maana ni haki ya binadamu ambayo hayawezi kukiukwa.”

Vatican News

Scholas Occurrentes ni Harakati la Kimataifa la Elimu lililoundwa na Papa Francisko ambalo, limepokea Tuzo ya “Juan Antonio Carrillo Salcedo” kutoka Chuo Kikuu cha Seville kwa ajili ya kulinda haki za binadamu. Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila baada ya miaka miwili, inawatambua watu au taasisi ambazo zimejipambanua kwa utetezi wa haki za binadamu, iwe katika nyanja za kisiasa, kijamii au kielimu. Hapo awali, ni Malkia Sofia wa Hispania, Federico Moyor  Zaragoza, Marcelino Oreja na Adela Cortina pekee ndio walikuwa wametunukiwa tuzo hiyo. Jopo la  uamuzi la  Chuo Kikuu cha Seville, mojawapo ya taasisi kongwe zaidi za kitaaluma nchini Hispania, lilichagua Scholas Occurrentes, ambayo kwa bahati linaadhimisha mwaka wake wa kumi,  mwaka huu 2023, kutoa tuzo hii maarufu. Kazi ya Harakati ya Scholas Occurrentes katika kutetea haki za binadamu za vijana duniani kote na mazoea yake madhubuti na ya kibunifu, ili kila mtoto na kijana awe na maisha yenye maana, haijapita bila kutambuliwa.

Del Corral: kushiriki katika changamoto nyingi

José María del Corral, rais wa Harakati ya Scholas Occurrentes kimataifa, alitoa maoni yake kuhusu utambuzi huo kuwa: “Scholas inatetea ukweli kwamba kuwa na maisha yenye maana ni haki ya binadamu ambayo haiwezi kukiukwa, na ili kufikia hili tunashughulikia masuala tofauti latika kuzuia kujiua katika sehemu nyingi za ulimwengu, tunashughulikia afya ya akili ya vijana na vijana katika nchi zaidi ya 30 wakati wa janga hili, na tunapambana na shida kama vile magenge ya kiharifu huko Panama, Mafia huko Napoli , Italia  na unyanyasaji wa watoto nchini Ureno, Mexico na Hispania.: Kwa kufafanua zaidi alisema: “Wengi wetu tunazungumza kuhusu haki za binadamu, lakini linapokuja suala la kuona kazi, wachache wanaifanya kwenye matope, au kuacha” alisema del Corral. Kwa hiyo Scholas Occurrentes iliwasili Hispania mnamo mwaka 2015 na tangu wakati huo amekuwa akishirikiana kikamilifu na Kanisa mahalia na madhehebu mengine, a Wizara ya Elimu, Vijana na Masuala ya Kijamii, huko wakifanya shughuli mbalimbali katika mikoa mbalimbali ya nchi, kama vile Jumuiya ya Madrid, Catalonia, Galicia, Valencia, Andalusia na Cantabria. Kwa upande wake, amesema matawi ya chuo kikuu cha Scholas yamefunguliwa huko Madrid, Granada, Valencia na Barcelona, ​​​​miongoni mwa zingine.

Uzoefu wa kielimu ulimwenguni kote

Tangu kuanzishwa kwake, Scholas imeunda uzoefu wa kielimu ambao umewaleta pamoja vijana kutoka Israel na Palestina, kutoka Cuba na Marekani, kutoka tamaduni na dini mbalimbali, na kuunda maprofesa katika vyuo vikuu vya umma na vya kibinafsi; kujenga shule za michezo nchini Msumbiji, Iraq na Amerika Kusini. Vijana wa Scholas hufanya kazi kila siku kutoka Haiti ili kurejesha utu kupitia elimu. Zaidi ya hayo, kutoka Los Angeles, Miami, New York na Washington, walimu wa Scholas hutafuta kumsaidia kila kijana kupata maana na kusaidia mazungumzo ili kushinda chuki na migogoro. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Harakati hiyo  tunasoma kuwa: “Kila siku  waalimu vijana  wa Scholas hukutana na shida halisi za watoto na vijana kama vile :ukosefu wa afya ya akili, ongezeko kubwa la watu wanaojiua, ukosefu wa usalama, ongezeko la kutumia madawa ya kulevya na ufisadi, unyanyasaji, unyonyaji  wa watoto, uonevu kwenye mtandao na maumivu mengine mengi yanayohitaji kusikilizwa, kufanyiwa ubunifu na jamii. Vile vile  Wanachuo wanaamini kwamba mfumo wa elimu unaweza kubadilishwa, kutoka chini na kwa kujitolea kwa kila mtu. Wanatetea haki za binadamu kwa vijana kwa vitendo madhubuti, bila kujali ni wa imani na dini gani  au ile au wa ngazi hii au ile ya kijamii au kiuchumi, kwa sababu anaamini kuwa jambo muhimu ni mkutano na utofauti huo ndio unaotuunganisha. Tuzo hiyo, kwa waanzilishi wake, ni ya vijana wanaojitolea muda na shauku yao kila siku ili kuwafikia vijana wengi zaidi ulimwenguni na kwa Papa Francisko kwa kuwa na imani katika uvumbuzi huu mtakatifu.”

Tuzo kwa Harakati ya Kimataifa ya Scholas Occurrentes
19 December 2023, 16:12