Tafuta

2023.12.29 Picha ya Madonna Lactans yaani Mama anayenyonyesha,itawekwa kwenye sherehe za Kipapa mwishoni na mwanzo wa mwaka 2024 Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. 2023.12.29 Picha ya Madonna Lactans yaani Mama anayenyonyesha,itawekwa kwenye sherehe za Kipapa mwishoni na mwanzo wa mwaka 2024 Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. 

Picha ya Mama anayenyonyesha itakuwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Picha ya karne ya 12,inayotoka katika Madhabahu ya Montevergine,itawekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya sherehe za kipapa za Desemba 31 na Januari 1,2024.Tamaduni ya zamani inabainisha kuwa Picha ya kwanza ya Maria kuheshimiwa na Mtakatifu William wa Vercelli,mwanzilishi wa Abasia ya Virginia,ambapo wanaadhimisha miaka yake 900.

Riccardo Luca Guariglia, o.s.b.

Kwa jumuiya nzima ya watawa ya Montevergine ni furaha kubwa sana kuwezesha Baba Mtakatifu na waamini wote watakaokuwapo katika Kanisa kuu la Vatican kwenye Maadhimisho ya Siku kuu ya Mama Mtakatifu wa Mungu kuheshimu picha hiyo ya  Bikira na Mtoto anayenyonyeshwa na ambayo imehifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Abasia. Tafiti zilizofanywa kwenye sanaa hiyo zimeruhusu kuakisi picha huyo ya Madonna Lactans yaani Mama anayenyonyesha kuwa ni ya mwanzoni mwa karne ya 12 na utamaduni wake unasimulia jinsi ilivyokuwa kitu cha ibada ya kwanza ya mwanzilishi wetu Mtakatifu William wa Vercelli na wafuasi wake wa kwanza na  wote waliofuata,  yaani sisi watawa wa Kibenediktini wa Virginia ambao tunajisikia kuwakilishwa ipasavyo na ndugu yetu wa kale aliyeoneshwa kwenye miguu ya Mama Maria aliyeketi kwenye kiti cha enzi, na kuomba kutoka kwao nuru ya neema, uimarishwaji wa imani na faraja ya tumaini katika kufuata kanuni za kimungu za Mwana wake. Mama anayenyonyesha mtoto wake ni picha halisi ya huruma: katika kila zama, katika kila ustaarabu na  katika kila upande. Hata zaidi kwetu sisi Wakristo, wakati tunapoishi siku za ukumbusho wa kuzaliwa kwa Mwokozi, wa ukweli wa ajabu na wa kushtua wa umwilisho, ule wa Mungu aliyefanyika mwanadamu kwa upendo.

Hii picha ya ‘Madonna del latte’ – yaani ‘Mama wa maziwa’ inajidhihirisha kwa macho yetu kama picha ya uzuri wa kupendeza na maarufu licha ya utukufu wa pozi na utajiri wa mapambo na ina uwezo wa kutafsiri kwa ajili yetu, kama ilivyokuwa kwa babu zetu wote, lugha ya haraka na ya ulimwengu wote kutoweza kupenyeka kwa mafundisho makuu. Ni picha ya muujiza wa kila siku na wa pamoja, ule wa kuzaliwa na kukua, uliojaa hisia na mshangao, lakini hauko huru dhidi ya hatari na hatarishi, kama vile ujio wa ulimwengu na utoto wa Bwana. Tunaweza kufikiria, tukimtazama kwamba ni macho ngapi ya akina mama yenye shukrani au ya kusihi kwa karne nyingi yatakuwa yameinuliwa kuelekea kwake na mikono mingapi inayotetemeka itawainua watoto wachanga waliovalia nguo za kitoto mbele yake na kuwaomba kwa ulinzi wa kimungu.

Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.”( Lk 11, 27 ): ni sifa ambayo mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia mama wa Yesu anayeonyeshwa waziwazi na mwandishi asiyejulikana kutoka kijijini katika picha ya Mama wa Mungu kwa ajili ya matunda tele ya kiroho tunayopewa siku baada ya siku. Kwa njia hiyo tunafurahi kumletea Baba Mtakatifu Francisko Picha hii ya Bikira Maria Mtakatifu, anayembariki nafsi yake na dunia nzima kwa kumuonesha Mwana wake wa Mungu, “mkuu wa amani” (Isa 9, 5). Kwa ujasiri wa furaha wakati huo huo, kutoka juu ya mlima ambapo Abasia yetu ipo hadi Madhabahu ya Kuungama ya Basilika ya Vatican, tunaomba maombezi yake yenye nguvu, ili familia ya binadamu, ijifungue kwa ujumbe wa Kiinjili. Na Baba Mtakatifu anayetangaza bila kuchoka, anaweza kupitia mwaka mpya unaoanza kwa udugu na amani. Ni maneno yake mwenyewe ambayo yanatuongoza katika kuinuliwa na kusifiwa kwa Theotokos (Mama wa Munguu) wakati, kama wachungaji, tunatafakari Picha ya Mtoto mikononi mwa Mama yake, tukihisi hisia za shukrani nyingi ambazo hukua mioyoni mwetu kuelekea Yeye aliyemtoa Mwokozi wa ulimwengu:

“Asante, Mama Mtakatifu wa Mwana wa Mungu Yesu, Mama Mtakatifu wa Mungu! Asante kwa unyenyekevu wako uliovutia macho ya Mungu; asante kwa imani uliyopokea Neno lake; asante kwa ujasiri ambao ulisema: “Tazama mimi hapa”, kwa kujisahau mwenyewe, ukivutiwa na Upendo Mtakatifu, ulifanywa kuwa na tumaini lake. Asante, Mama Mtakatifu wa Mungu! Utuombee, mahujaji kwa wakati; utusaidie tutembee katika njia ya amani. Amina.” (Papa Francisko, Malaika wa Bwana, tarehe 1 Januari 2017).

Mama Maria anayenyonyesha
30 December 2023, 15:01