Tafuta

Kusomwa kwa hukumu ya kesi ya usimamizi wa fedha za Vatican. Kusomwa kwa hukumu ya kesi ya usimamizi wa fedha za Vatican.  (ANSA) Tahariri

Mchakato ambao ulihakikisha haki za wote

Maoni kando ya uamuzi kuhusu uuzaji wa mali kwenye Barabara ya Sloane

Andrea Tornielli

Kwa hakika haifai kuuita “mchakato wa karne,” hata kama kile ambacho kimehitimishwa mapema katika chumba cha madhumuni mbalimbali cha Makumbusho ya Vatican bila shaka kilikuwa mchakato muhimu. Wa kwanza kwa upeo na ukubwa huu tangu serikali ya Jiji la Vatican kuwepo, yaani, tangu wakati wa Mkataba wa Lateran ya 1929. Ulikuwa ni mchakato mrefu na wenye kutaabisha, ambao uliingia katika "mwili hai" wa usimamizi wa fedha za Vatican, na ambao uliweka hadharani njia zote mbili ambazo katika baadhi ya kesi fedha zilisimamiwa na jaribio la baadhi ya watendaji wa nje kuchukua rasilimali za Kanisa. Njia ya uwazi na ya lazima ya mchakato wa kawaida ilifanywa ili kujibu malalamiko yaliyowasilishwa na vipengele vilivyojitokeza wakati wa uchunguzi na awamu ya uchunguzi wa awali.

Usimamizi wa fedha za ng'ambo umekuwa mada ya uandishi wa habari na wakati mwingine hata uchunguzi wa mahakama kwa zaidi ya nusu karne. Njia ya uwazi ilianzishwa kwa ujasiri na Papa Benedikto XVI na kuendelezwa kwa dhamira ya mageuzi ya Papa Francisko. Papa, akikabiliwa na kasoro zilizoripotiwa kwa mamlaka za mahakama sio na mahakama ya nchi nyingine bali na vyombo vya ndani ya Vatican, aliruhusu haki kufuata mkondo wake wa kawaida na wa kitaasisi. Zaidi ya misisitizo iliyowakilishwa na baadhi ya watu, ile  inayohusu uwekezaji katika jengo kaitka Barabaya ya Sloane na masuala yanayohusiana nayo ilikuwa kesi ya haki, ambayo ilichezwa kabisa katika kikao cha mjadala wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, kwa kufuata kikamilifu dhamana kwa washtakiwa: hii haioneshwa tu na idadi ya mashauri, nyaraka na mashahidi waliochunguzwa, lakini pia ukweli kwamba mashahidi ambao walionekana kuwa wa msingi hapo mwanzo baadaye haukuwa na maana kutokana na ulinganisho katika chumba cha mahakama na ushahidi wa maandishi.

Lakini matokeo ya kesi hii pia yanatuambia kwamba mahakimu wa Mahakama, kama ilivyokuwa sawa, walijadiliana kwa uhuru kamili kwa msingi wa ushahidi wa maandishi na ushahidi uliosikilizwa, si kwa nadharia zilizowekwa awali. Na waliacha nafasi ya kutosha kwa ajili ya  mjadala. Kwa hiyo hukumu hiyo ilifikiwa kwa kuzingatia dhamana zote za washtakiwa, kwa kuzingatia ipasavyo maombi ya watetezi wao na zaidi ya yote bila kuunda kanuni ili kuendana na urahisi wa mashitaka. Hii inadhihirishwa, kwa mfano, na uamuzi wa Mahakama wa kuzingatia kauli zilizotolewa wakati wa kuhojiwa na Mlinzi wa Vatican Gianluigi Torzi kuwa zisizoweza kutumika. Maelezo ambayo yaliwashtaki washtakiwa wengine, lakini ambayo hayakukubaliwa kwa vile Torzi mwenyewe hakufika katika chumba cha mahakama kuyarudia na kuyathibitisha.

Baba Mtakatifu Francisko mnamo Februari mwaka jana alisema, wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Kimahakama: “Hapa tunahitaji kuwa wazi na kuepuka hatari ya kuchanganya kidole na mwezi”: tatizo si taratibu ya michakato, lakini ukweli na tabia ambazo zinazoazimia kuzifanya kwa uchungu ziwe muhimu sana.” Sheria za uwazi, udhibiti mkali wa usimamizi wa fedha, ikiwa ni pamoja na wasimamizi wa nje, na ufahamu kwamba hakuna maeneo huru, itachangia kuenea kwa usimamizi wa mali za kikanisa ambazo zinazidi kufanana na moja ya busara wa baba wa familia. Mwanzo wa mchakato huu ulionesha kwamba Vatican na Serikali ya mji wa Vatican wanamiliki “kingamwili” zinazohitajika ili kubaini madai ya unyanyasaji au mambo yasiyofaa. Mchakato wa kesi yake unathibitisha kwamba haki inasimamiwa bila njia za mkato, kwa kufuata kanuni za utaratibu, kuheshimu haki za kila mtu na kudhaniwa kuwa kwa hasiye na hatia.

Kardinali Becciu kuhukumiwa kifungo jela kwa miaka 5 na faini juu
17 December 2023, 10:22