Tafuta

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP28 kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi huko Dubai Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP28 kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi huko Dubai  (AFP or licensors)

Kardinali Parolin:kuna ishara chanya za kutia moyo kutoka Cop28

Mwishoni mwa kikao alichoshiriki,Katibu wa Vatican alitoa tathimini ya Mkutano wa tabianchi huko Dubai hasa kufuatia na kuunda mfuko wa Fidia ya Hara na uharibifu kwa nchi zinazokablisha na athari mbaya za tabianchi,kwamba anaamini ni moja ya ishara kuu za matumaini kuruhusu kufanya tathimini hata kama njia bado ni ndefu.

Na Stefano Leszczynski - Dubai

Mwishoni mwa kazi ya siku ya tarehe 2, Disemba 2023,ambayo ilimwona akitoa hotuba iliyotiwa saini na Papa Francisko mbele ya mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali,Katibu wa Vatican,Kardinali  Pietro Parolin alielezea tathmini ya awali ya kazi hiyo inayoendelea katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa COP28, juu ya mabadiliko ya tabianchi huko Dubai kuanzia tarehe Mosi hadi 12 Desemba 2023.

Kardinali Parolin Katibu wa Vatican wakati wa kutoa Mkutano wa COP28
Kardinali Parolin Katibu wa Vatican wakati wa kutoa Mkutano wa COP28

Miongoni mwa mada kumi zilizojitokeza katika hotuba za viongozi wa dunia waliokusanyika huko Dubai,na moja ambayo inachochewa zaidi na maneno ya Papa ni mada ya uwajibikaji wa kimaadili wa nchi zilizoendelea zaidi kuelekea nchi zenye uchumi dhaifu na ambayo mara nyingi huteseka kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Kwa upande wa Kardinali Parolin alisema hii,"ilikuwa mojawapo ya mambo makuu ya uingiliaji kati uliofuatana wakati wa mchana,hasa kutokana na mbinu ambayo hasa ni ya Papa Francisko. Kipengele cha maadili ambacho ni muhimu sana kwa sababu kinahusisha ukumbusho wa nguvu wa kila mtu kuwajibika kwa viongozi waliopo hapa, hasa wale kutoka nchi zilizoendelea zaidi." Kwa  upnde wa Kadinali,Parolini alisema “siku hii ya tatu ya mkutano ilikuwa kali sana na pia tajiri sana katika maudhui.”

Mji wa EXPO  Dubai wakati wa COP28
Mji wa EXPO Dubai wakati wa COP28

"Hata wito uliozinduliwa na Papa Fransisko kwa viongozi wa dunia kutojifungia nje kwa maslahi binafsi, ili kuwa kwa maslahi ya kikundi, kwa maslahi ya kitaifa inaonekana kukubalika kwa niaba ya manufaa ya wote,"alisisitiza Katibu waVatican. Kigezo pekee ambacho kinaweza kuturuhusu kweli kushughulikia hali ya mabadiliko ya tabianchi   na yenye matunda."

Watu wakizunguma katika jengo la Mkutano wa COP28
Watu wakizunguma katika jengo la Mkutano wa COP28

Miongoni mwa matokeo ya kwanza kukaribishwa ni hakika utekelezaji wa Mfuko wa Fidia ya Hasara na Uharibifu inayokusudiwa kusaidia nchi zinazokabiliwa na athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi. "Ninaamini kwamba hii ni moja ya ishara kuu za matumaini,ambayo inaruhusu angalau hadi sasa kufanya tathmini chanya ya Mkutano huo, hata ikiwa bado kuna njia ndefu,"alielezea Kardinali Parolin.

Tathimini ya Kardinali Parolin kuhusu COP28
04 December 2023, 15:36