Tafuta

2023.12.22 Kardinali Parolin wakati wa kubariki watoto wadogo wagonjwa katika hospitali ya kipapa ya Bambino Gesù 2023.12.22 Kardinali Parolin wakati wa kubariki watoto wadogo wagonjwa katika hospitali ya kipapa ya Bambino Gesù 

Kard.Parolin kati ya wagonjwa wadogo wa Bambino Gesù na madaktari

Katibu wa Vatican alitembelea wagonjwa wa hospitali ya watoto ya Vatican ili kuwapelekea salamu za Papa kwa kuzingatia Noeli inayokaribia.Kati ya utani,picha,salamu,kupeana mikono na mtoto kutoka Puglia ambaye anamwuliza:"Je,wewe ni Padre Pio?"Kadinali alisalia Salamu Maria katika kila chumba cha kitengo cha Gastroenterology na kutoa baraka na zawadi za Papa.

Vatican News

“Je,wewe ni Padre Pio? Kardinali Pietro Parolin aliangua kicheko, chini ya Barakoa yake, mara baada ya swali la Angelo. “Angelino,” mwenye umri wa miaka 7, “Malaika kwa jina na ukweli,”alisema baba yake - anayetokea huko Lecce, italia wa mtoto huyo aliyepandikizwa ini katika siku za hivi karibuni na ni mmoja wa watoto wapatao ishirini ambao Katibu wa Vatican alikutana nao alasiri tarehe 22 Desemba 2023, katika Kitengo cha Gastroenterology ya Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù. Kwa njia hiyo katika hospitali ya Vatican, madaktari bingwa barani Ulaya wanaojulikana duniani kote, ndipo Kardinali alikwenda kupeleka matashi na Heri za siku kuu ya Noeli na zawadi bora ikiwa ni pamoja na zile za upendo na ukaribu wa Papa Francisko. “Ninakuletea salamu za Papa, unajua?”, alimwambia Andrea, ambaye pia amelazwa hospitalini baada ya kupandikizwa ini. “Alifanya vizuri vya  kutosha kuchukua cheti cha shule ya Msingi  hapa na sisi”, walielezea madaktari, “kwa sababu alifanya mtihani hospitalini”. Kardinali Parolin alishangaa na kiusema: “Vizuri sana,” “Ninataka kuanza chuo kikuu lakini kwa fujo nimekuwa nayo...”  alisema mvulana, mwingine huku akidhamiria kutazama mfululizo kwenye kompyuta. Mama yake idha alimwonesha Katibu wa Vatican vitabu vilivyowekwa kwenye dirisha, vitabu vya maandalizi kwa ajili ya majaribio ya kuingia.  Kardinali alijibu: “Sawa, tayari unatazama mbele.”

Kardinali na wauguzi na madaktari wa Hospitali ya kipapa ya Bambin Gesu
Kardinali na wauguzi na madaktari wa Hospitali ya kipapa ya Bambin Gesu

Ni mazungumzo mafupi ambayo yalilenga kupunguza mateso ya wagonjwa lakini zaidi ya wazazi wote, ambao baadhi yao wamekuwa karibu na watoto wao kwa siku, miezi au miaka, hata kwa miaka kumi. Kama baba na mama wa Sveva, ambaye tangu kuzaliwa “amekuwa na mambo mengi madogo ya kutatua”, alisema daktari anayemfuatilia. “Hakuna Mtakatifu Sveva, labda atakuwa mmoja,” mama yake alitabasamu.  Kwa kujibu  Kardinali Parolin alisema: “hata ninyi wazazi,” Vile vile  Kardinali aliwapelekea watoto na familia nyingine picha ndogo ya Papa na kutoa msalaba wa plastiki wenye uso wa Kristo. Kinachoonekana katika wengi wa wagonjwa hawa, ambao wakati wa Noeli  watakuwa hospitalini  kwa sauti ya kuendelea ya kufuatilia moyo ambayo hupima vigezo vyao, kati ya taa na vyumba na harufu kali ya za usafi, pia viliyopambwa kwa michoro, vinyago au pango la kuzaliwa, miti midogo iliyopambwa na  wafanyakazi wa uuguzi. Kardinali Parolin alitembea kuzunguka wadi kwa karibu saa moja, akiwasalimu kila mtu. Katika kila chumba, mwishoni, baada ya kupeana mikono au maombi, aliuliza, kama "kuna yeyote anayetaka kuongoza  sala ya Salamu Maria. Kardinali alizunguka katika vyumba kumi alivyongia huku akisali rosari, isipokuwa chumba cha mwisho cha wagonjwa mahututi. Huko alibaki nje lakini aliweza kutuma baraka yake.

Akiwa na rais  wa Hospitali ya Watoto Bambin Gesu, Tiziano Onesti na mkurugenzi wa afya Massimiliano Raponi pembeni yake, Kadinali Parolin alimtania Valeria, mwenye umri wa miaka 15, mwenye ugonjwa wa Wilson kutokana na sumu ya shaba: “Kukaa hapa kunasumbua kidogo”?  “Lakini ni mafunzo ya maisha,” alijibu. Kisha kwa Luca aliyemgusa shavu, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, ambaye kutokana na kulazwa hospitalini yuko mbali na ndugu wengine. Aliwatia moyo Cosimo na Vincenzo, mapacha wawili kutoka Bari(“Vijana wawili!”), ambao walifanyiwa upasuaji wa ini kwa ajili ya ugonjwa wa kimetaboliki: “Kabla ya hapo hawakuweza kula vyakula,  alieleza daktari kutoka timu ya matibabu, “walikuwa wanahudhuria shule ya hoteli na baada ya upasuaji, waliweza kuhudumiwa na kula vitu vile vile." Sasa wanataka kuwa wapishi: “Ni taaluma maarufu sana ... Mmerudi katika maisha ya kawaida, ujasiri!"alisema Kardinali Parolin.

Kardinali Parolin aliwatembelea watoto hospitalini
Kardinali Parolin aliwatembelea watoto hospitalini

Kwa kila mmoja tunajijulisha kuhusu matibabu na vyanzo vya magonjwa, ahueni; alisema ili kuwafariji baadhi ya akina mama: “wewe ni jasiri, mama! Ni katika kuelezea Mtoto mwingine Cristian mwenye umri wa miaka 2, ambaye alitoka Albania, pia atakuwa na ini jipya kwa siku chache zijazo. Kulikuwa na mtoto mwingine wa Kosovo ambaye alilia kwa uchungu akiwa na mirija iliyounganishwa: Watoto maskini ambao hawajui jinsi ya kujieleza. Wakati Giosué, ambaye alieleza kwa sauti ya uchovu kwamba amefanyiwa operesheni 18-20, alimhakikishia kwamba atatambua ndoto yake ya kuondoka hospitalini.

Kardinali Parolin alionekana kuguswa na pia alishiriki hisia hizi na madaktari, wauguzi, watawala na watawa wa kujitolea aliokutana nao katika Jumba la Salviati, lililopewa jina la familia ya mwanzilishi wa Hospitali ya Bambino Gesù na hasa kukutana na wagonjwa wadogo. Inagusa,” alisema na  wale waliokuwapo, huku madaktari wengine wengi na wauguzi wakiunganishwa kupitia utiririshaji, kwani wasingeweza kuondoka mahali pao pa kazi. Kardinali Parolin alisema alivyostaajabishwa kuona kukaribishwa kwa watoto lakini pia kwa wazazi: “Ni furaha kubwa kukutana na Padre na kusali pamoja na kupokea baraka za Baba Mtakatifu. Daima ni wakati mzuri na wa kugusa." Aliongeza kuwa inagusa moyo jinsi gani kukutana na wale wanaofanya kazi hospitalini: “Singependa kusema nijisikie kama maofisa wa Kiti Kitakatifu, labda ingekuwa nyingi sana, lakini mna wajibu mkubwa kama wahudumu wa afya, wauguzi, madaktari, watawala, kila mtu ana nafasi yake. Ninyi kwa maana fulani ni mawakala wa Kiti Kitakatifu."

Kardinali Parolini na watoto wagonjwa kwa Baraka ya Noeli
Kardinali Parolini na watoto wagonjwa kwa Baraka ya Noeli

Kwahiyo katika maneno ya Kardinali kuna"asante" peke yake kwa huduma ambayo"wanatoa sababu ya watoto wagonjwa ambao ni jumuiya maalum sana lakini pia sababu ya Uinjilishaji, kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Aliwaambia wahudumu wa hospitali kuwa waowasihubiri lakini kwa kazi yao wanatoa ushuhuda wa utume huu ambao Yesu aliwakabidhi wanafunzi". Kwa hivyo kutiwa moyo kusonga mbele kwa "shauku" na  ari lakini juu ya yote kukaa karibu na familia; "Leo tunajua kuwa kuna haja ya kusaidia familia wakati wa hali dhaifu, shida na matatizo ni kuwa sababu ya matumaini kwa wagonjwa na familia zao."

Kardinali na watoto wa Hospitali ya Kipapa ya Bambin Gesu

 

23 December 2023, 18:12