Kard.Parolin aongoza Misa katika Hospitali ya Kisayansi ya(IDI)
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Jumamosi taarehe 23 Desemba 2023, Kardinali Parolin Katibu wa Vatican ameadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya Wagonjwa na wahudumu wa kiafya, katika fursa ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana 2023. Misa hiyo imefanyika katika Hospitali ya Kisayansi na matibabu ya Immacolata, Roma. Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Hospitali hiyo inabainisha kuwa "Mkutano kwa ajili ya kutakiana heri za Noeli, unajikita katika utamaduni muhimu na wenye thamani ya wakati wa kukutana kati ya wafanyakazi wahudumu na wagonjwa wakiungania katika tumaini na katika jitihada kwa ajili ya mchakato wa safari daima yenye umakini na utunzaji wa mtu mgonjwa:
Ibada ya Misa Takatifu kwa Wagonjwa na wahudumu wa Kiafya(IDI - IRCCS), iliudhuriwa na idadi kubwa ya wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo. Kwa namna hiyo jumuiya ya Hospitali imependelea kwa mara nyingine tana kukusanyika pamoja katika wakati wa kushirikishana na kwa maombi.
Kwa njia hiyo “mazungumzo kati ya madaktari, wafanyakazi wa hospitalini na wagonjwa ambao ni sehemu ya historia na utamaduni wa Taasisi hiyo unajikita katika hatua ya mbele kwa manufaa ya wote. Katika maadhimisho ya Ibada ya misa walioshikiriki ni pamoja na Mwenyekiti wa Hosptiali hiyo, Padre Padre Giuseppe Pusceddu, wanashirika wenzake ambao wanatoa huduma katika Hospitali hiyo na ndugu wengine walioshiriki pamoja na Baraza la Ushauri, Alessandro Zurzolo na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.