Kard.Krajewski:hali halisi ya Gaza ni ngumu
Vatican News
Inahitajika kuwa na moyo mkuu wa kutoa nafasi ya maumivu na kuyafunika kwa tumaini wakati kila kitu, nyumba, mapenzi, maisha yamepoteza haki ya joto na hali ya hatari iliyojaa hofu kuwa kawaida. Baada ya ziara nyingi katika eneo la vita katika kambi za vita vya Kiukraine, wakati umefika kwa Kadinali Konrad Krajewski kupeleka mkumbatio wa Papa na usaidizi wa Noeli kwenye eneo jingine ambalo ni Ukanda wa Gaza na Nchi Takatifu ambapo tangu 7 Oktoba 2023 wamefunikwa na giza la mkasa mwingine. Habari za mwakilishi wa Papa Francisko kwenye vyombo vya habari vya Vatican, zinaanzia Bethlehem, ambapo alifika huko asubuhi 22 Desemba na kujikuta amepiga magoti katika Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana, mapema asubuhi na mara baada ya kuanza ziara ya mji huo na Padre wa Parokia ya Gaza.
Katika kueleza siku yake alisema "Tulikwenda kwenye vituo vitatu vya watoto yatima, ambako hata watoto wachanga wanaotolewa nje ya barabara wanatunzwa, na watoto wawili walioletwa hivi karibuni tu na watawa.” Alisema Kardinali na kwamba alikaa nao kwa muda ili kusali pamoja na kwamba: “Pia niliwaachia msaada wa Baba Mtakatifu aliowatumia kwa sababu wanaishi kwa shida sana.” Kisha alibaki kwa chakula cha mchana katika seminari ya Upatriaki wa Bethlehemu, ambapo waseminari 38 wanaishi. Alasiri ndiyo wakati wa mkutano mgumu sana. Kardinali Krajewski alizungumza kuhusu watu wanne, vijana kabisa, waliokuja kuzungumza naye. Walipata bahati ya kuondoka Gaza kabla ya kuanza mikasa. Kwa sababu hiyo, alisisitiza. “Wanafamilia wao wote walibaki, ila msichana alipoteza wanafamilia 12. Walikuja kueleza jinsi mambo yalivyo, kuweza kumwambia Baba Mtakatifu hali ngumu yote iliyopo, kwamba hakuna maji, hakuna umeme, kwamba watu wanaozunguka kanisa ni karibu watu 600. Tulisali pamoja, kwa hakika tulihuzunishwa sana lakini hatukukosa tumaini”.
Kardinali aliendelea kusema kuwa "Siku nzima nilipitia katika nchi ambayo Yesu alizaliwa na ambapo leo hii tunapitia polepole na chini ya udhibiti mkali. Tungeweza kuingia kutoka upande mmoja, mlango pekee, kwa sababu Wapalestina hawawezi kuondoka Bethlehemu, wanapaswa kukaa mjini. Kesho, tutaona ni wapi tunaweza kwenda kusaidia jumuiya mbalimbali za kidini, mapadre wanaofanya kazi katika hali hii ngumu sana.” Kardinali Krajewski alisema pia kuwa alikutana na Askofu wa Kikatoliki wa Ugiriki na kwamba: “Tulizungumza kuhusu jinsi tunaweza kuongeza misaada. Kwa sababu katika Noeli ya mwaka huu bila taa mwanga unaopasha joto na kuonesha mwelekeo ni ule wa ukaribu tu."