Tafuta

2023.12.14 Waamini wa Kanisa Katoliki la Gaza  wakiwa wanasali 2023.12.14 Waamini wa Kanisa Katoliki la Gaza wakiwa wanasali  (© KIRCHE IN NOT)

Kard.Krajewski ametumwa na Papa kwenda Nchi Takatifu

Baba Mtakatifu Francisko amemtuma mwakilishi wake,Kadinali Konrad Krajewski,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo katika Nchi Takatifu kama ishara ya mshikamano wakati wa janga la vita.Kardinali wa Poland atakuwa huko Nchi Takatifu katika Noeli wakati huo huo Patriaki wa Kilatini ya Yerusalemu amewaalika kila mtu kuombea amani.

Vatican News

Amani ni zawadi ambayo Papa, hasa katika kipindi hiki cha Noeli, ameomba mara kadhaa katika miito mingi iliyotolewa ili kumaliza mzozo kati ya Israeli na Hamas, lakini pia kwa Ukraine inayoteseka ambayo imekuwa ikiteseka kwa karibu miaka miwili.  "Katika vita hii ya tatu ya dunia iliyosambaratika, sala inakuwa kazi na kuwa utume kupitia kwa Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekitin wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambaye Papa Francisko amemtuma katika Nchi Takatifu, kama ishara halisi  ya ushiriki wake kwa Kanisa la mateso wanayopata matokeo ya vita moja kwa moja.” Ndivyo tunsoma katika taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo. “Kwa hakika ni matakwa ya Baba Mtakatifu kwamba safari hii iambatane na sala ili kupata zawadi ya amani katika maeneo ambayo kelele za silaha bado zinasikika. Amani ambayo itatolewa katika sala kuu ambayo Almoner wa Papa atafanya pamoja na Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa na Kanisa zima la mahali, "kusherehekea siku kuu ya kuzaliwa kwa Yesu, mkuu wa amani na tumaini pekee la Dunia."

Mwakilishi wa Papa alikuwa Ukraine katika Noeli ya 2023

Kwa Kardinali Krajewski kwa mara nyingine tena Atakuwambali na Roma katika Noeli hii. Mwaka 2022, kiukweli, alikwenda Ukraine kupeleka masweta kwa ajili ya  joto kwa idadi ya watu, iliyotolewa na maelfu ya watu pia na  kupitia usajili wa mtandaoni, lakini pia kupeleka jenereta za nishati. Usaidizi wa kimwili na wa kiroho ni njia mbili ambazo Almoner hutekeleza wajibu wake. Hata wakati wa Pasaka, wakati mwingine muhimu kwa Kanisa, ukaribu wa Papa na idadi ya watu wa Ukraine ulionekana, na picha zenye kugusa za sala yake mbele ya makaburi ya halaiki ya Borodjanka, moja ya maeneo yaliyoharibiwa zaidi na vita.

Maombi ya Papa

Kardinali atawasili katika Nchi Takatifu akiwa na sala moyoni, ileile aliyosali Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Juni 2014, katika bustani ya Vatican mbele ya Rais wa Israel Shimon Peres na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Sala iliyokumbukwa katika taarifa kwa vyombo vya habari vya Almoners na bado inafaa sana kurudia leo hii: “Eee Bwana Mungu wa amani, usikie maombi yetu! Utupe amani, tufundishe amani, tuongoze kuelekea amani. Fungua macho yetu na mioyo yetu na utupe ujasiri wa kusema: “wala tusipigane tena!; kwa vita kila kitu kinaharibiwa. Uweka ndani mwetu  ujasiri wa kufanya ishara thabiti ili kujenga amani. Na maneno haya yafukuzwe kutoka kwa moyo wa kila mtu yaani mgawanyiko, chuki, na vita! Bwana, ondoa silaha za ulimi na mikono, ufanye upya mioyo na akili, ili neno linalotuleta pamoja daima ni ndugu, na mtindo wa maisha yetu unakuwa: shalom, amani, salamu.”

22 December 2023, 11:16