Tafuta

2023.12.14  Banda la Imani katika COP28 limehitimishwa kwa mafanikio ya shughuli zake:Vipindi 70 vya mazungumzo na zaidi ya watoa mada 300 kutoka ulimwenguni kote. 2023.12.14 Banda la Imani katika COP28 limehitimishwa kwa mafanikio ya shughuli zake:Vipindi 70 vya mazungumzo na zaidi ya watoa mada 300 kutoka ulimwenguni kote.  

COP28,Kard.Czerny:Uongofu ni mabadiliko ya mtazamo na mwelekeo

Miongoni mwa mada zilizojitokeza katika hotuba za viongozi wa dunia katika Cop28,moja inayopata msukumo mkubwa kutoka kwa maneno ya Papa ni ile ya uwajibikaji wa kimaadili wa nchi zilizoendelea zaidi kuelekea nchi zenye uchumi dhaifu ambao mara nyingi huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.Amesema Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Katika Mkutano wa COP28 ambao ulianza mnamo tarehe 30 Novemba na kumalizika tarehe 12 Desemba 2023, mengi bado yanazungumza juu yake hasa wasi wasi kuu inayoibuka kuhusu hukosefu wa utekelezaji wa makubaliano yaliyowekwa kwenye Hati ya mwisho, kwa kufikiria maazimio ya mkutano iliyotangulia hadi sasa. Ni katika muktadha huo ambapo hata Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu anatoa maoni yake. Kwa upande wake Kardinali Czerny katika Gazeti la Osservatore Romano ameandika  kuwa: “Uwepo uliotangazwa wa Papa Francisko katika COP28 unaashiria hatua ya mabadiliko, iliyohisiwa na wengi, kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua juu ya tabianchi. Kutofika kwake kwa sababu za kiafya kunawakilisha kipengele kisicho na maamuzi, kwa sababu msisitizo ambao umekuwa wazi kwa wakati huu ni kwamba leo kutunza mazingira sio msimamo wa kisiasa sana, lakini ni jukumu kubwa la maadili la kila mtu.”

COP28
COP28

Kwa maana hii, “ukweli kwamba, miaka minane baada ya waraka wa kihistoria wa Laudato si', Papa mzee anaweka mamlaka yake ya kimaadili tena katika utendaji ili kuwasukuma wawakilishi wa COP28 kuwa wajasiri, na kuhamasisha jumuiya ya kiraia, jambo la msingi la  kutorudi nyuma. Mabilioni ya wanadamu wanahimizwa na uongozi huu wa kiroho kufufua dhamiri zao na kushiriki katika mabadiliko makubwa katika wazo la maendeleo.” Mkuu hiyo wa  baraza la Huduma ya Maendeleo ya Binadamu aanasisitiza kuwa “Kutunza nyumba yetu ya pamoja kumekuwa kipaumbele cha mara kwa mara cha Papa Francisko, kama inavyooneshwa na hatua zake nyingi na juhudi nyingine nyingi katika kukuza hatua ya mabadiliko katika kukabiliana na hatari ya mabadiliko ya tabianchi na dhuluma zinazoteseka na jamii zilizo hatarini zaidi. Katika upeo wa ikolojia  fungamani, suala la mazingira si matakwa ya wanamazingira, lakini kwanza kabisa ni “tatizo la kijamii la kimataifa”, ambalo haliwezi kupunguzwa au hata kudhihakiwa, ikizingatiwa kuwa changamoto ya mazingira, ya kijani ya  mapendeleo.” Papa anapinga ukanushaji wowote na upunguzaji, akibainisha mabadiliko ya tabianchi kama ‘tatizo la kibinadamu na kijamii kwa maana pana na katika viwango mbalimbali" ambalo “linahitaji ushiriki wa kila mtu.”

Utekelezaji wa Makuabaliano ya COP28 ndiyo unaohitajika kuliko maneno
Utekelezaji wa Makuabaliano ya COP28 ndiyo unaohitajika kuliko maneno

Kardinali Czerny anaadika kuwa “Mnamo Oktoba 4 iliyopita, miezi miwili kabla ya  kuanza kwa Cop28, Baba Mtakatifu alichapisha Waraka wa  Kitume wa Laudate Deum, wenye sura mbili zilizojitolea kwa ajili ya  Kilele cha Mkutano wa Umoja wa Mataifa, bila kuacha ukosoaji mkali wa matoleo yaliyopita, lakini wakati huo huo akiongeza uaminifu kwa njia ya kimataifa, kama chombo muhimu cha utawala wa mienendo ya kimataifa. Kama inavyojulikana, kiwango cha juu cha muunganiko wa diplomasia wa tabianchi ilikuwa COP21, ambayo ilizaa “Makubaliano ya Paris”, yaliyoidhinishwa hivi karibuni pia na Vatican. Kuna haja ya "kuzindua upya safari" na Kanisa - kuwa mwaminifu kwa kile kinachoamini na kutangaza,  lazima lihimize kwa kila njia kushinda kuganda na migawanyiko iliyopatikana katika mikutano  ambayo yalikuwa ya kukatisha tamaa katika mambo mengi. Katika ujumbe wake kwa COP28, Papa Francisko alitutaka tuepuke vikwazo vya ubinafsi na utaifa ambavyo ni mifumo ya zamani na ambavyo vimewakilisha, mara nyingi, kikwazo cha kukomesha uchoyo, unyonyaji na ukosefu wa haki.”

Mandhari huko Dubai ilikuwa inavutia
Mandhari huko Dubai ilikuwa inavutia

Kardinali Czerny aidha anaandika kuwa “akitoa hotuba huko Dubai, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican katika ujumbe wa Papa Francisko ulikuwa ni mpana na umejaa mawaidha na mialiko mingi. Maneno yake kuhusu hatua kali ya mataifa yaliyosababisha mzozo wa sasa wa kiikolojia, na ambayo yana rasilimali za kulipia athari za sera zisizo endelevu, yanafikia moja kwa moja kwenye kiini cha mjadala mkuu wa mazungumzo haya: "Sio kosa la maskini, kwa sababu karibu nusu ya dunia, maskini zaidi, inawajibika kwa asilimia 10 tu ya hewa chafuzi, wakati pengo kati ya matajiri wachache na wengi wasiojiweza halijawahi kuwa mbaya sana.” “Kwa mantiki hiyo, miongoni mwa mada zilizojitokeza katika hotuba za viongozi wa dunia katika Cop28, moja inayopata msukumo mkubwa kutoka kwa maneno ya Papa ni ile ya uwajibikaji wa kimaadili wa nchi zilizoendelea zaidi kuelekea nchi zenye uchumi dhaifu, ambao mara nyingi huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.”

Mazingira yalivutia wakati wa Mkutano wa COP28
Mazingira yalivutia wakati wa Mkutano wa COP28

Kardinali Czerny aidha alisisitiza kuwa “ikumbukwe pia kwamba Waraka wa Kitume wa Laudate Deum, unataka hatua za haraka na za lazima juu ya tabianchi na onyo lisilo la kawaida dhidi ya kutumia zana za kiteknolojia kushughulikia suala hilo. Katika ujumbe uliotumwa huko Dubai, Papa Francisko anashutumu “misimamo migumu ikiwa sio isiyobadilika, na uwajibikaji wa mara kwa mara: na anaomba kukumbatia “maono mbadala, ya kawaida” ambayo “yataruhusu uongofu wa kiikolojia,” kwa sababu “hakuna kudumu mabadiliko bila mabadiliko ya kiutamaduni.” Ni katika kiwango hicho ambapo masimulizi makuu huhesabiwa, yenye uwezo wa kuhamasisha mawazo ya jumuiya za wanadamu, na hata zaidi rasilimali za kiroho zinazohitajika kuingia katika mchakato wa uongofu. Usemi huu, katika chimbuko na kiini cha ujumbe wa kiinjili, unahamasisha “kujitolea na msaada wa Kanisa Katoliki” ambao Papa anawahakikishia viongozi wa dunia na wanadamu wote. Uongofu ni mabadiliko ya mtazamo na mwelekeo. Kuhubiriwa kwa Ufalme kunadokeza kwamba hatua hii ya badiliko inatukia hapa chini, kati ya mambo ya kila siku, kuweka upya kila mtu katika uhusiano unaofaa na viumbe na pamoja na muumba.”

Katika COP28 kwa mara ya kwanza kulikuwa na Banda la Imani
Katika COP28 kwa mara ya kwanza kulikuwa na Banda la Imani

Kardinali Czerny aidha anaandika kwamba: “Kwa mara ya kwanza katika COP28, kulikuwa na  maonesho ya “Banda la Imani,” ambapo ilikuwa ni nafasi ya mikutano ya kidini na mazungumzo ambayo kila mtu ana jukumu la kufanya unabii na uwezo wa athari ya kweli ya kiutamaduni. Ingawa haikuzungumzwa mara nyingi, jukumu la imani, lakini limekuwa muhimu katika mazungumzo ya tabianchi. Mara nyingi jumuiya za kidini ndizo zinazounga mkono makundi maskini zaidi na yaliyo hatarini zaidi katika nchi zao na kuzihimiza serikali zao kuchukua hatua kubwa zaidi. Matumaini ni kwamba watu wengi watatiwa moyo na kutiwa moyo na imani kufanya maendeleo makubwa katika suala hilo. Ikumbukwe kwa kweli kwamba, katika hali ya sasa na takwimu inayokuja kwetu kutoka kwa jumuiya ya wanasayansi, Cop28 inaonekana, ikiwa sio habari ya mwisho, kwa hakika kama mojawapo ya madirisha machache ya fursa  ambazo bado zinapatikana.” Kwa maana hiyo aliongeza kuandika kuwa “Matumaini ni kwamba, ujumbe wenye nguvu wa Papa na mwaliko wa kushinda maslahi na mitazamo inayogawanyika unaweza kutoa msukumo mpya katika mazungumzo ya kiufundi ya siku hizi, ili kufikia makubaliano ya mwisho ya kupitishwa kwa kauli moja. Hizi ni hatua muhimu za uratibu wa hatua kuhusu tabianchi, zikiongozwa na umuhimu wa kutoa sayari inayoweza kuishi na kukaribisha kwa vizazi vya sasa na vijavyo.”

Kardinali Czerny na maoni yake kuhusu COP28
14 December 2023, 15:07