Tafuta

2023.11.27 Maaskofu na Mkutano wa Mawasiliano ya Kikatoliki huko Bangkok,Thailand. 2023.11.27 Maaskofu na Mkutano wa Mawasiliano ya Kikatoliki huko Bangkok,Thailand. 

Bangkok,Maaskofu wapyaisha utume wa mawasiliano ya Kanisa

Wataalam wa Vyombo vya Habari wa Kikatoliki wa Asia walikusanyika katika mji mkuu wa Thailand huko Bangok,katika Mkutano wa 28 wa Mwaka wa Maaskofu ili kushirikisha nia yao ya kusaidia Kanisa katika kuwasilisha huruma na furaha ya Injili.Dk.Ruffini:"Wakristo wameitwa kuwa wamisionari katika enzi ya kidijitali."

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Maaskofu, mapadre na walei kutoka Bara la Asia yote  walikusanyika huko Bangkok katika siku za hivi karibuni ili kuainisha njia za mbele katika utume wa Kanisa wa kuwasilisha Injili kwa ufanisi na kwa ujasiri kwa njia zote za kisasa za mawasiliano. Takriban wajumbe 30 walikutana kuanzia tarehe 20 hadi 24 Novemba katika Jumba la Don Bosco katika mji mkuu wa Thailand kwa ajili ya mkutano wa 28 wa kila mwaka wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa FABC-OSC.

Mkutano kuhusu mawasiliani ya kijamii huko Thailand
Mkutano kuhusu mawasiliani ya kijamii huko Thailand

Kati ya walioudhuria Mkutano huo ni pamoja na Dk. Paolo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano akiambatana na Nataša Govekar, mkurugenzi Kitaalimungu-kichungaji wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano , ambao walijiunga na wawakilishi wa Kanisa la Asia kwa siku tano za tukio hilo. Pia walioshiriki katika tukio hilo ni Kardinali Charles Bo, Askofu Mkuu wa Yangon na rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Asia (FABC), na Kadinali Francis Xavier Kriengsak, Askofu Mkuu wa Bangkok.

Washiriki wa Mkutano huko Bangkok
Washiriki wa Mkutano huko Bangkok

Akizungumzia  juu ya mada ya “Mawasiliano katika Kanisa la Sinodi”,  Dk. Ruffini alionesha nia ya Vatican kushiriki katika kusaidiana na Makanisa mahalia na akakumbusha kwamba Kanisa la Sinodi linahusu zaidi kujenga uhusiano kuliko kusambaza mawasiliano tu: Kanisa ni jumuiya ya wanafunzi wanaoinjilisha, hivyo Wakristo wameitwa kuwa wamisionari katika zama za kidijitali na wawasilianaji wa Kanisa ili kutangamana na mitandao ya kijamii kwa matumaini ya kujenga mikutano ya kibinafsi. Siku zote ni vyema kukutana ana kwa ana na kupata muda wa kubadilishana mawazo,wasiwasi na ndoto, alieleza Dk.Ruffini anaelezea akizungumza na Vatican News. "Nilichoelewa katika siku za hivi karibuni ni kwamba kutoka Asia Mashariki, tunaweza kujifunza somo: kwamba utamaduni wa mashariki unajua jinsi ya kuelewa kwamba kila kitu ni umoja,unajua jinsi ya kuangalia zaidi ya kuonekana".

Tukio la Mkutano wa mawasiliano ya Kijamii huko Thailand
Tukio la Mkutano wa mawasiliano ya Kijamii huko Thailand

Katika siku ya kwanza ya hafla hiyo ilishuhudia vijana wengi wa mawasiliano kutoka sehemu mbalimbali za bara la Asia wakikusanyika kwa ajili ya kikao cha mtandaoni kuhusu "Imani ya Kuwasiliana katika Ulimwengu wa Dijitali", mpango unaosimamiwa na  Baraza la Kipapa la Mawasiliano ili kuwatayarisha vijana kwa ajili ya  changamoto za mawasiliano watakazokabiliana nazo.  Hawa walikuwa ni Wavulana na wasichana walioshiriki walitoka Ufilipino, Malaysia, Myanmar, Singapore, Vietnam, India, Timor Mashariki, Pakistan na Thailand yenyewe. Lengo lilikuwa ni kwamba, kwa msaada wa baadhi ya miongozo, wapate ufahamu wa utambulisho wao ili kuwasiliana vyema katika utamaduni wa heshima,mazungumzo na urafiki.

 Nataša Govekar katika tukio la Thailand
Nataša Govekar katika tukio la Thailand

Nataša Govekar aliwasilisha hati ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuelekea uwepo kamili - Tafakari ya kichungaji juu ya kujihusisha na mitandao ya kijamii.Verso una piena presenza - Riflessione pastorale sul coinvolgimento con i social media. Haya ni maandishi ya kurasa 34, yaliyochapishwa mnamo mwezi Mei 2023, ambayo yanawaalika Wakatoliki "kuishi katika ulimwengu wa kidijitali kama 'majirani wanaopendana' ambao wapo kiukweli na wanaosikilizana katika safari yetu ya pamoja kwenye 'barabara kuu za kidijitali'.

Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakati wa kutoa hotuba yake
Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakati wa kutoa hotuba yake

Kwa upande wake, Kardinali Sebastian Francis, Askofu wa Penang nchini Malaysia na rais wa Ofisi ya Mawasiliano ya Jamii ya  Baraza la Maaskofu Asia (FABC,) alibainisha  kuwa mkutano wa Bankok ulikuwa  wa kwanza wa ana kwa ana wa FABC-OSC kwa miaka kadhaa.  "Mawasiliano ni njia yetu ya maisha, njia yetu ya kuhusiana," alisema na kuongeza kwamba Waasia ni "wasimulizi wa historia. Na tuna historia ya kusimulia." Kardinali alionesha imani kwamba wamisionari vijana wa kidijitali wataweza kusimulia historia ya Injili ya huruma na furaha. "Kuna vijana wengi sana, hasa katika bara la Asia,ambao wanakuwa sehemu ya utume huu na sehemu ya historia  hii na wanaosonga mbele,hata mbele yetu katika kuinjilisha,katika kushirikisha historia  hii ya Injili na Asia."

01 December 2023, 14:31