Tafuta

Padre Vincent Cosma Mwagala kutoka Jimbo Katoliki la Iringa  ameteuliwa kuwa Askofu  wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Mafinga. Padre Vincent Cosma Mwagala kutoka Jimbo Katoliki la Iringa ameteuliwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Mafinga.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Askofu Vincent Cosmas Mwagala Jimbo Katoliki la Mafinga, Tanzania

Askofu mteule Vincent Cosmas Mwagala alizaliwa tarehe 11 Desemba 1973 huko Makungu, mkoani Iringa. Baada ya masomo yake ya Kikasisi toka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino, Peramiho, iliyoko Jimbo kuu la Songea kwa Falsafa aliendelezwa kwa masomo ya Taalimungu na akajipatia Shahada ya Uzamili kutoka katika Kitivo cha Kipapa cha Taalimungu, Sicilia, huko Palermo. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 11 Julai 2007 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Iringa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 22 Desemba 2023 ameunda Jimbo jipya la Mafinga, Tanzania kwa kulimega Jimbo Katoliki la Iringa na kwamba, Jimbo Katoliki la Mafinga litakuwa chini ya Jimbo kuu la Mbeya. Jimbo Katoliki la Mafinga “Mafingensis" limeundwa baada ya kumega Jimbo Katoliki la Iringa na Jimbo kuu la Mbeya na Makao makuu ya Jimbo yatakuwa mjini Mafinga na Kanisa kuu la Jimbo ni Kanisa la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, Mafinga.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa sana Padre Vincent Cosmas Mwagala kutoka Jimbo Katoliki la Iringa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Mafinga. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Vincent Cosmas Mwagala alikuwa ni Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Iringa na Paroko wa Ifunda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Vincent Cosmas Mwagala alizaliwa tarehe 11 Desemba 1973 huko Makungu, Wilaya ya Mufinndi, mkoani Iringa. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi toka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino, Peramiho, iliyoko Jimbo kuu la Songea kwa Falsafa aliendelezwa kwa masomo ya Taalimungu na hatimaye akajipatia Shahada ya Uzamili kutoka katika Kitivo cha Kipapa cha Taalimungu, Sicilia, huko Palermo, Kusini mwa Italia. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 11 Julai 2007 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Iringa.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wakati wa "Ad Limina 2023"
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wakati wa "Ad Limina 2023"

Tangu wakati huo, kama Padre amebahatika kutekeleza dhamana na utume wake kama: Paroko-usu huko San Gerlando, Lampedusa, Italia kati ya Mwaka 2007 – 2011, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Usokami kati ya Mwaka 2011-2018. Akateuliwa kuwa ni Msaidizi wa Askofu upande wa Watawa. Kuanzia mwaka 2015 akateuliwa kuwa Makamu wa Askofu Jimbo Katoliki la Iringa na Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo Parokia ya Ifunda kuanzia mwaka 2018. Kuanzia Mwaka 2019 aliteuliwa kuwa ni mjumbe wa Baraza la Washauri wa Askofu. Jimbo Katoliki la Mafinga “Mafingensis lina jumla ya Parokia 17 zitakazokuwa zinahudumiwa na Mapadre wa Jimbo 30, Mapadre Watawa 11. Lina watawa wa kiume ni 5 na watawa wa kike ni 136. Waseminari walioko Seminari kuu ni 52, lakini Jimbo lina utajiri mkubwa wa Makatekista wapatao 350.

Jimbo Katoliki la Mafinga linaundwa na Parokia za: Mafinga, Sadani, Mdabulo, Mgololo, Kibao, Ikwega, Nyakipambo, Nyololo, Itengule, Usokami, Mapanda, Ibwanzi, Igowole, Nadibira, Ujewa, Chosi na parokia ya Mbarali. Askofu mteule Vincenti Cosmas Mwagala atawekwa wakfu na hatimaye kusimikwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Mafinga hapo tarehe 19 Machi 2024, Sherehe ya Mtakatifu Yosefu, Mume wake Bikira Maria.

Jimbo Katoliki Mafinga
22 December 2023, 11:54