Tafuta

Askofu mkuu Vincenzo Turturro, Balozi wa Vatican nchini Paraguay Askofu mkuu Vincenzo Turturro, Balozi wa Vatican nchini Paraguay 

Askofu Mkuu Vincenzo Turturro Balozi wa Vatican Nchini Paraguay

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Eliseo Antonio Ariotti, Balozi wa Vatican nchini Paraguay la kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshiwa sana Monsinyo Vincenzo Turturro kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Paraguay na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1978. Upadrisho tarehe 31 Oktoba 2003 na uteuzi wa ubalozi umefanyika 29 Desemba.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Eliseo Antonio Ariotti, Balozi wa Vatican nchini Paraguay la kung’atuka kutoka madarakani. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mstaafu Eliseo Antonio Ariotti alizaliwa tarehe 17 Novemba 1948, Jimboni Cremona, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, tarehe 7 Mei 1975 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 17 Julai 2003 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Cameroon na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, tarehe 5 Oktoba 2003 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. Tarehe 5 Agosti 2003 aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Equatorial Guinea. Baba Mtakatifu Benedikto XV1, tarehe 5 Novemba 2009 akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Paraguay na kung’atuka kutoka madarakani tarehe 29 Desemba 2023.

Viongozi wa Serikali ya Paruay walipokutana na Papa Francisko.
Viongozi wa Serikali ya Paruay walipokutana na Papa Francisko.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshiwa sana Monsinyo Vincenzo Turturro kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Paraguay na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Vincenzo Turturro alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1978 huko Bisceglie, Bari. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 31 Oktoba 2003 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuingizwa Jimbo Katoliki la Molfetta nchini Italia. Amesoma na kujipatia Shahada ya uzamili katika masomo ya Taalimungu. Tarehe 1 Julai 2009 akaingia kwenye Diplomasia ya Kanisa na kufanikiwa kutoa huduma nchini Zimbabwe, Nicaragua na Argentina. Mwishoni hapa alihamishiwa mjini Vatican kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican na kupangiwa kufanya utume wake kitengo cha Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Na tarehe 29 Desemba 2023 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Paraguay.

Uteuzi Paraguay
29 December 2023, 14:37