Seoul,Askofu Mkuu Peña Parra kwa waseminari:ikumbatieni imani kw
Osservatore Romano
Mapadre wanaitwa kwanza kabisa kuleta furaha ya Injili kwa kila mtu, si kwa maneno tu bali zaidi ya yote kwa kutoa maisha yao yenyewe. Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Sekretarieti Vatican, aliyasema hayo katika salamu zake Jumamosi tarehe 18 Novemba 2023, kwa jumuiya ya seminari kuu ya Seoul wakati wa kuhitimisha misa aliyoiadhimisha. Hiki kilikuwa ni kitendo cha mwisho cha ziara yake nchini Jamhuri ya Korea iliyoanza tarehe 17 Novemba 2023, ambapo Askofu Mkuu Parra alishiriki katika matukio mbalimbali ya Kanisa la mahali hapo, akikutana pamoja na mambo mengine, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Korea (CBCK) , Askofu Matthias Ri Iong-hoon, wa Suwon, na kisha Baraza la Kudumu la Baraza hilo hilo.
Akiendelea Askofu Mkuu alisema kuwa, “Zawadi ya thamani ya wito wa ukuhani, ni kukumbuka historia yenu, ya mashahidi wengi ambao wameikubali imani kwa ujasiri, ya safari ile ya watu ambayo wito wa ukuhani ulizaliwa na kukomaa. Mzizi huu katika ukweli halisi utawasaidia kuwa wachungaji waliofanyika mwili katika maisha ya watu na makuhani ambao, kwa shauku juu ya utangazaji wa Injili, wazi, furaha na kupatikana, wanajua jinsi ya kuwa wachungaji wenye huruma kama Yesu, wanaoweza kuwa na ukaribu na ubinadamu."
Askofu Mkuu Peña Parra akikumbuka maneno ya Papa Francisko, kuhusu Mtakatifu Andrew Kim alisema "alikuwa na anabakia kuwa shuhuda fasaha wa bidii kwa ajili ya kutangaza Injili." Kiukweli, "hata ndani ya usiku wa giza wa mateso ambayo Peninsula ya Korea imepitia furaha ya Injili imetiririka kama mto uliojaa wa maji safi na imerutubisha ardhi hii, ikizalisha jumuiya ya Kikristo yenye bidii katika imani na yenye kutia moyo katika mioyo ya vijana wengi kama nyinyi ni wito wa kumfuata Bwana katika njia ya kuwekwa wakfu maalum.