Tafuta

2023.11.24 Papa Francisko amekutana na Bwana Nikos Christodoulides,Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Cyprus. 2023.11.24 Papa Francisko amekutana na Bwana Nikos Christodoulides,Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Cyprus.  (Vatican Media)

Papa amekutana na Rais Nikos wa Cyprus

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa 24 Novemba 2023 alikutana na Rais Nikos Christodoulides ambaye mara baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican akisindikizana na Monsinyo Pacho.Uhamiaji na hali za kimataifa zilikuwa mada msingi zilizogusiwa katika mazungumzo.

Vatican News

Tarehe 24 Novemba 2023, Baba Mtakatifu Francisko alikutana mjini Vatican katika nyumba ya Kitume na Bwana Nikos Christodoulides, Rais wa Jamhuri ya Cyprus, ambaye baadaye alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican  akifuatana na Monsinyo Daniel Pacho, Katibu Msaidizi  wa Vatican wa  Sekta ya Kimataifa ya Kitengo cha Mahusiano na mataifa na mashirika ya kimataifa.

Papa na Rais wa Cyprus wakibadilishana zawadi
Papa na Rais wa Cyprus wakibadilishana zawadi

Wakati wa majadiliano ya ukarimu katika Sekretarieti ya Serikali, shukrani ilioneshwa kwa mahusiano mazuri kati ya  nchi mbili, pia kutaja baadhi ya masuala ya wazi katika mahusiano ya Kanisa na  Vatican. Kisha waliakisi  baadhi ya changamoto za sasa za nchi, zikiwemo za wahamiaji. Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, kulikuwa na kubadilishana mawazo kuhusu hali ya kimataifa, kwa kuzingatia hasa migogoro inayoendelea, ikiwemo ya Israel na Palestina.

Papa na rais wa Cyprus
24 November 2023, 15:42