Tafuta

2023.11.23 Maswali ya Waandishi wa Habari kwa Kardinali Parolin nje ya Kanisa la Mtakatifu  Andrea wa Valle, Roma. 2023.11.23 Maswali ya Waandishi wa Habari kwa Kardinali Parolin nje ya Kanisa la Mtakatifu Andrea wa Valle, Roma. 

Kard.Parolin, Vatican haifutilii mbali kuaaniwa kwa vitendo

Katibu wa Vatican akiwa kando ya Misa ya kumbu kumbu ya miaka 90 ya mauaji ya kimbari alisisitizia msimamo wa Papa wa ukaribu na Waisraeli na Wapalestina.

Vatican News

Papa na Vatican kwa ujumla wako karibu na mateso ya kila mtu: hapakuwa na "kupuuzwa" katika kulaani shambulio baya la Hamas mnamo 7 Oktoba 2023; wakati huo huo hatuwezi "kupuuza" kile kinachotokea Gaza, "ambapo kumekuwa na vifo vingi, majeraha mengi, uharibifu mwingi". Ni maneno ya  Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, aliyesisitiza tena msimamo huo wa usawa ambao umekuwa mtindo wa Vatican  tangu wakati wa  Papa Benedikto XV, ambaye pia alishambuliwa pande zote mbili wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, kwa kuwa alidumisha msimamo wa kutoegemea upande wowote, bila kutambua ,  kulingana na washtaki - mchokozi na aliyeshambuliwa. Hatima ambayo sasa inaonekana pia kumuathiri Papa Francisko, ambaye maneno yake ya mwisho wakati wa Katekesi yake Jumatano 22 Novemba 2023 yalizua mabishano kutoka kwa baadhi ya wawakilishi wa ulimwengu wa Kiyahudi, ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Kiyahudi wa Italia  Alhamisi asubuhi 23 Novemba 2023 ambapo katika barua analalamika kwamba  Papa angeweza kuweka katika ngazi moja kwa kuzungumzia ugaidi kwa pande zote mbili.

Alipoulizwa kuhusu hili na waandishi wa habari nje ya Kanisa la Mtakatifu Andrea wa Valle, ambapo aliadhimisha Misa alasiri  kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 90 ya Mauaji ya kimbali ya Holodomor, ambayo yalikuwa ni  maangamizi makubwa na njaa ya mamilioni ya Ukraine mnamo  mwaka 1932-33, Katibu wa Vatican  alizungumzia shutuma ambazo hazina maana kwa Papa na alisisitiza kwamba matukio ya hivi karibuni hakika hayatilii shaka katika uhusiano na ulimwengu wa Kiyahudi na "mafanikio ya miaka hii, kuanzia  Hati ya Nostra Aetate. (Tamko la Nostra aetate (yaani Katika wakati Wetu) ni moja ya hati za Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican unaohusu mada ya maana ya kidini na uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na dini zisizo za Kikristo.) kwa hiyo Kardinali hakika, aliseama kuwa,"tuna wasiwasi sana na wimbi hili la chuki dhidi ya Wayahudi ambalo linazuka kila mahali.

Msimamo wazi dhidi ya shambulio la Israel

Kulingana na Kardinali Parolin, kwa upande wa Vatican  kumekuwa na msimamo wa wazi kabisa kuelekea mashambulizi ya Hamas, sio kwamba tumepuuza. Wa kwanza alikuwa yeye mwenyewe, kando ya tukio la Chuo Kikuu cha Gregorian, baada ya shambulio la wanamgambo nchini Israeli, kuzungumza juu ya shambulio mbaya na "la kudharauliwa. Kisha Papa, ambaye katika kila tamko la hadhara hajawahi kuacha kunyanyapaa vurugu na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa kwa mateka wa Israel.  Kwa njia hiyo Kardinali alisisitiza kuwa, Inaonekana kwangu kwamba Vatican inajaribu kwa kila njia kuwa wa haki, kuzingatia mateso ya kila mtu. Pia katika kesi hii inapaswa kuhukumiwa kwa mambo mabaya ambayo Israeli imeteseka, alisisitiza Kardinali. Wakati huo huo hatuwezi hata kupuuza kile kinachotokea upande mwingine, yaani, katika Ukanda wa Gaza, ambapo kumekuwa na vifo vingi, majeraha mengi, uharibifu mkubwa. Papa - aliongeza kadinali, akikumbuka taarifa ya kutangaza hadhira ya jana kwa familia za mateka na kundi la Wapalestina - anataka kuwa karibu na mateso ya wale wote wanaoteseka".

Kwa wale miongoni mwa waandishi wa habari walioeleza kuwa ukosoaji wa Marabi leo ni sawa na ule uliojitokeza wakati wa vita kati ya Ukraine na Urusi kwa madai ya kutokuwepo tofauti kati ya wachokozi na walioshambuliwa, Parolin alijibu: Tayari tumekwisha. alijibu, kwa wakati wake. Papa na Holy See wanaeleza waziwazi: kwa upande wa Ukraine tulisema 'ni vita vya uchokozi. Je, tunaweza kusema nini zaidi ya hayo? Pia unahitaji kusoma maneno kwa uangalifu na kuelewa maana yake. Halafu ikiwa mtu anataka zaidi, sisi pia tuna msimamo wetu, tunazingatia, tunafanya maamuzi yetu." "Hata hivyo, haionekani kwangu - alimhakikishia kardinali - kwamba kuna usawa. Kabisa. Tumesema kila mara yale ya kusema, hata kama kwa njia zinazolingana na Kiti Kitakatifu. Na “anachosema Papa, anasema waziwazi. Kwa kweli, sio jinsi wanavyotaka."

Njia za Vatican

Mivutano, shutuma, ugumu katika kuzungumza juu ya amani, kwa vyovyote vile, si jambo jipya. "Sio mara ya kwanza hii kutokea ... Ikiwa unakumbuka wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia Papa Benedikto", Kardinali  alikumbuka.  Aidha alisema “Kwa hiyo samahani, lakini sishangai. Ni hatima ya kujua jinsi ya kumwambia kila mtu kile kinachohitajika kusemwa lakini ninarudi kusema kwa njia ambazo Jimbo Takatifu hulifanya."

Suala la mateka

Kuhusu njia za mazungumzo ambayo diplomasia ya Vatican inafuatiliwa huko Mashariki ya Kati, Katibu wa Vatican alieleza kwamba “jambo linaloweza kufanywa ni kuendelea na suala la mateka. Kwa sasa hakuna uwezekano mwingine mwingi." Kitendo cha Papa cha kukaribisha familia mjini Vatican, kwa mujibu wa kadinali huyo, "inaweza kutumika kwa maana hii kusaidia kupata suluhu la tatizo". akati huo huo, kazi mbele ya Kiukreni inaendelea kwa kurudi kwa watoto waliochukuliwa kwa nguvu kwenda Urussi. Taratibu ni kazi, yaani, utaratibu ulioanzishwa baada ya ziara ya Kardinali Zuppi huko Moscow na Kyiv. Na ilitoa matokeo fulani." Walakini, Kardinali Parolin alifafanua, kuwa "hata hapa hatupaswi kutarajia matokeo ya kushangaza, ambayo ni kwamba mamia na mamia yao wataachiliwa ...". Takwimu ambazo, zaidi ya hayo, "hakuna makubaliano: kwa upande mmoja wanasema jambo moja, kwa upande mmoja wanasema jambo lingine. Lakini kuna kazi ambayo inafanywa na ambayo imezaa matunda."

Mwisho wa vita nchini Ukraine na makubaliano ya Israel-Hamas

Swali kwa Kadinali huyo pia kuhusu kauli za Rais Vladimir Putin wa Urussi katika G20 kuhusu ukweli kwamba Urussi iko tayari kwa mazungumzo kukomesha janga la vita nchini Ukraine. Je, Putin anaaminika anapotarajia kumalizika kwa mzozo aliouanzisha mwenyewe?

Kardinali Parolin alitoa maoni kuwa, "Natumaini inaaminika kwa sababu ndivyo sote tunatumaini." Huku akisema anasikitishwa na kuahirishwa kwa makubaliano kati ya Hamas na Israel kwa ajili ya mapatano ya muda na kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina. Jana, juu ya mada hiyo, kadinali huyo alitoa maoni kwamba ilikuwa hatua muhimu ambayo iliangaza mwanga wa matumaini. Leo, hata hivyo, uchunguzi wa uchungu: "Hii si ishara nzurilakini waliniambia kwamba hatua ya mwisho ilikuwa ya Mahakama au Mahakama Kuu ambayo ilipaswa kutoa mwanga wa kijani, sijui. kujua kama hii ndiyo sababu kwa hivyo hakuna makubaliano... Tunatumai kweli kwamba tunaweza kufikia makubaliano, angalau usitishaji wa mapigano”.

Mismamamo wa Vatican

 

25 November 2023, 11:33