Tafuta

2023.11.20 Askofu Mkuu Gallagher na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje nchini Korea Kusini. 2023.11.20 Askofu Mkuu Gallagher na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje nchini Korea Kusini. 

Gallagher,yuko Korea Kusini kwa maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano kati ya Vatican

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya kimataifa yuko Barani Asia kuanzia tarehe 20 hadi 23 Novemba 2023 katika fursa ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Korea Kusini.

Vatican News

Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican  wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, yupo  safari ya  Korea Kusini kuanzia tarehe 20 Novemba hadi tarehe 23 Novemba 2023, katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hiyo na Vatican, kama ilivyofahamishwa na Sekretarieti ya tajwa na chapisho lililowasilishwa na(Segreteria di Stato con un post su X.) Hii ni safari ya kitaasisi lakini inaashiria, kwa mara nyingine tena, usikivu wa Kanisa kwa Bara la Asia, lenye utajiri wa nguvu mpya, na ambayo, pamoja na utamaduni na mapokeo yake ya kutafuta usawa, inaweza kuchangia katika kutafuta njia mpya za amani katika ulimwengu huu uliosambaratika na vita vya kindugu.

Kuzungumza na washiriki wa kongamano la walinzi wa kumbu kumbu na wa matumaini

Pamoja na mikutano ya kitaasisi na Waziri Mkuu wa Korea na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Askofu Mkuu  Gallagher atazungumza katika Kongamano lililoandaliwa katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka huu, juu ya mada iliyooneshwa na Papa Francisko wakati wa ziara yake huko Seul 2014(rej. viaggio a Seul, nell’agosto del 2014:) "Kuwa walinzi wa kumbukumbu na walinzi wa matumaini", na atakutana kwa njia isiyo rasmi na  baadhi ya wanachama wa Kikosi cha Wanadiplomasia.

Ziara ya kudumisha na kuendeleza njia kidiplomasia

Miongoni mwa matukio mbalimbali ya kidini, katibu wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ataadhimisha Misa Takatifu katika eneo la Madhabahu ya Seosomun, mahali ambapo wakristo wa kwanza wa Korea, mnamo tarehe 6 Mei 1984 walitangazwa kuwa Watakatifu na MtakatifuYohane  Paulo II(rej. primi cristiani coreani che, il 6 maggio 1984, furono canonizzati da San Giovanni Paolo II.) Ziara hiyo inakusudia kuwa ishara madhubuti ya kuendeleza njia iliyosafiri katika miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kwa ujasiri wa kufuatilia njia mpya za amani, hivyo basi kama alivyoomba Papa FRanciskoko mnamo Septemba iliyopita (rej. come  chiesto da Papa Francesco, il 16 settembre scorso,) akikutana na kikundi cha waamini wa Kikorea kwamba: "Ningependa kuwaalika kugundua tena wito wenu kama "mitume wa amani" katika kila eneo la maisha kwa kuwa mashuhuda wasafiri na mashuhuda ya upatanisho; ni ushuhuda wa kuaminika kwamba siku zijazo hazijengwi kwa nguvu kali za silaha, bali kwa nguvu ya upole ya ukaribu."

Askofu Mkuu Gallagher yuko Korea Kusini
20 November 2023, 17:30