Tafuta

2023.10.06 utoaji wa habari fupi kuhusu Sinodi. 2023.10.06 utoaji wa habari fupi kuhusu Sinodi.  (Vatican Media)

Uzoefu wa Kisinodi uwe wa kusikiliza na kujumuisha!

Sio mahali pa kueleza maoni ya kibinafsi,bali ni mahali pa kusikiliza,kutambua na kutembea pamoja kuelekea ufukwe ambapo Bwana anatungoja.Ndiyo muhtasari wa Sinodi ya kisinodi kwa mujibu wa kile kilichojitokeza wakati wa taarifa ya sasisho alasiri Oktoba 7,katika Chumba cha Waandishi wa Habari Vatican mwishoni mwa kazi ya vikundi vidogo.

Na Paolo Ondarza na Angella Rwezaula –Vatican.  

Yesu, Kanisa, familia, sinodi, kusikiliza, ushirika, maskini, vijana, jumuiya, upendo. Haya ni baadhi tu ya maneno yanayojirudia mara kwa mara katika siku hizi za kwanza za kazi ya Sinodi ya kisinodi, ambayo imefikia mwisho wa uchunguzi wa sehemu ya kwanza ya Instrumentum Laboris au  kitendea kazi. Katika siku hizi za kwanza, kwa mujibu wa ripoti ya rais wa Tume ya Habari, Dk. Paolo Ruffini, na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, wakati wa mkutano wa sasisho la  alasiri tarehe 7 Oktoba 2023 kwamba washiriki  wa Sinodi walitoa shukrani kwa Papa kwa uzuri wa wakati huu ambao wanapitia mabadiliko ya Kanisa Katoliki ulimwenguni.

Wanahabari wakichukua video na picha wakati wa ripoti fupi ya Sinodi
Wanahabari wakichukua video na picha wakati wa ripoti fupi ya Sinodi

Ripoti ya vikundi vidogo

Baada ya mkutano mkuu wa tatu uliofanyika Oktoba 6 alasiri, kikao cha tatu cha vikundi vidogo kilifanyika asubuhi Oktoba 7, 2023 kwa ukamilishaji wa taarifa ya kazi iliyofanyika katika vikundi hivyo vya kazi vinavyoundwa na takriban watu 10-12, wakiwemo ndugu wajumbe ambao hata hivyo hawashiriki katika kura. Taarifa hizo, zilizoidhinishwa na kila kundi kwa idadi kubwa, ziliwasilishwa kwa Sekretarieti Kuu ya Sinodi ambayo inazikubali kuzirejesha kwenye mkutano wakati hati ya muhtasari itakapojadiliwa.

Masuala ya uhusiano

Miongoni mwa mada zilizojitokeza katika ripoti za kila kikundi cha mduara: mafunzo katika kila ngazi, ya mapadre,  waseminari, katika familia; wajibu wa pamoja kati ya wote waliobatizwa; njia ambayo uongozi unaweza kujiweka ndani ya ushirika; washiriki waliombwa kuzama kwa kina zaidi kuhusu neno kisinodi kutoka katika mtazamo wa kileksika katika lugha mbalimbali. Tatizo lililosisitizwa sio tu kutenguliwa kwa ukiritimba wa miundo ya kikanisa, lakini ni hitaji la kuweka nguvu katika kufikiria upya aina mpya na maeneo mapya ya kushiriki katika ushirika na katika historia ya miaka elfu moja ya Kanisa.

Vijana na ukweli wa kidijitali

Haja ya kuwashirikisha vijana iliawekwa bayana, kwa mfano kwa kuzingatia uhalisia wa kidijitali, kuhama kutoka katika dhana ya mamlaka hadi ile ya huduma, kuepuka aina yoyote ya ukleri au maagizo bila kuhusika. Pia walijiuliza kuhusu jukumu la walei na wanawake ndani ya ushirika wa kikanisa na jinsi gani Kanisa linaweza kujiweka katika huduma ya maskini na wahamiaji. Kazi ya sinodi pia ililenga uhusiano kati ya mapafu mawili ya Kanisa, ya Mashariki na Magharibi.

Waandishi wa habari wakiwa wanapata ripoti ya Sinodi
Waandishi wa habari wakiwa wanapata ripoti ya Sinodi

Papa Francisko, mchungaji anayeongoza Sinodi

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa Dk. Ruffini alisema,  Papa pia alikuwepo katika mkutano mkuu wa Oktoba 6 alasiri na kwa ujumla ni miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika ukumbi huo. Papa Francisko alitoa shukrani za pekee kwa jinsi wafanyakazi wa vyombo vya habari wanavyoelezea acontecimiento, au tukio, la Sinodi. Mkutano huo mfupi ulihudhuriwa na Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (Secam); Sr. Leticia Salazar, ODN, shuhuda wa mchakato mzima wa sinodi kutoka Jimbo la Mtakatifu Bernardino nchini Marekani na kama kawaida Sheila Leocádia Pires, Katibu wa Tume ya Habari ya Sinodi.

Kutafuta mapenzi ya Mungu kwa Kanisa leo hii

Kardinali Ambongo, katika mang’amuzi yake ya nne ya Sinodi, alikumbusha tofauti za Sinodi hii ikilinganishwa na zile zilizotangulia kuwa: “Katika tukio hili, umuhimu mkubwa unazingatiwa katika kutafuta mapenzi ya Mungu kwa wakati huu wa kihistoria wa maisha ya Kanisa. Hakuna aliyekuja na ajenda ya kulazimisha. Sisi ni kaka na dada tunasikiliza mapenzi ya Mungu kwa ajili ya  Kanisa lake na yale yatakayotokana  na Sinodi hii yatazaa matunda mema na yatakaribishwa kama mapenzi ya Mungu." Ni muhimu kumsikiliza Roho: lengo la safari hii hadi 2024 ni kutafuta majibu bora kwa ajili ya matatizo fulani na matokeo, shukrani kwa maombi na majadiliano, yatakuwa "kitu karibu na kile tunachoweza kuzingatia kuwa mapenzi ya Mungu."Alisema Rais wa SECAM.

Maombi

Kwa hakika, hakuna sinodi bila sala. "Kama Kanisa siku zote tuko katika utambuzi na hakuna hatua ya kuwasili," Alisema. Aidha Rais wa SECAM, alihojiwa na waandishi wa habari, kisha akaeleza kwamba ripoti za vikundi vidogo vya mduara hazitachapishwa ili kuheshimu "utaratibu wa sinodi uliowekwa" na kutakuwa na muhtasari wa ripoti zote. Kwa kuzingatia moja tu kunaweza kumaanisha kuachana na sinodi.

Rais na Katibu wa Tume ya Habari za  Sinodi 2023
Rais na Katibu wa Tume ya Habari za Sinodi 2023

"Sio sekretarieti ya Sinodi inayoamua au kutekeleza Sinodi," alisema: kuna mwingiliano kati ya midura midogo na sekretarieti kuu. Zaidi ya hayo, mamlaka ya washiriki binafsi haitolewi kwa uteuzi wa Papa, bali kwa ubatizo. Katika suala hilo, Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Ruffini alikumbusha kuwa wajumbe waliopendekezwa ni 52 kati ya jumla ya wajumbe 364.

Njia mpya ya kutatua shida

Alipoulizwa kuhusu masuala yanayohusiana na masuala ya LGBT au Jinsia moja  na jinsi haya yatakavyo karibishwa na maaskofu wa Afrika, Kardinali Ambongo Besungu alisema: "tuko hapa kwa ajili ya Sinodi ya kisinodi. Sitaki kutoka nje ya mada. Sinodi haimaanishi kueleza maoni ya kibinafsi, bali kutembea pamoja kuelekea ufukwe ambapo Bwana anatungoja. Kuhusu suala la LGBT, au jinsia Bwana mwenyewe atatuonesha mwelekeo kupitia utambuzi wa pamoja." Zaidi ya hayo, rais wa SECAM alitoa ushauri kwa waandishi kupunguza matarajio yaliyotiwa chumvi kutoka katika Sinodi hii, ambayo hupekee wake ni kufafanua njia mpya ya kufanya mambo na kushughulikia matatizo kwa upande wa Kanisa.

Sio wazo, lakini uzoefu

"Sinodi si dhana, lakini ni uzoefu wa kusikilizwa, ikiwa ni pamoja "alisema Sr. Leticia Salazar, akionesha shukrani kubwa kwa uwezekano wa kushiriki katika tukio ambalo Kanisa zima la ulimwengu linahusika. Kisha aliweka bayana mada ya uhamiaji katikati ya utambuzi wa sinodi. “Nikiwa na umri wa miaka 17, nilihamia California pamoja na familia yangu na Kanisa lilinikaribisha mara moja.”

Matukio nje ya ukumbi

Sheila Leocádia Pires pia aliunganisha mada hiyo, akikumbusha kwamba uhamiaji una athari kwa muundo wa familia na ni mada pana sana ambayo inahusisha wengine kuanzia na mabadiliko ya tabianchi, migogoro, vita, na mengine.  Katibu wa Tume ya Habari ya Sinodi baadaye  alikumbusha matukio yanayohusiana na kazi hiyo inayoendela kwamba, Alhamisi ijayo washiriki wote wanaalikwa kwenda hija katika  Catacombs ya Mtakatifu  Domitilla na Mtakatifu Sebastiano; Matukio ya sala kama vile rozari yaliyopangwa katika Kanisa Kuu la Vatican, pia ndani ya bustani za Vatican na kuabudu Ekaristi. Hata katika ukumbi nafasi ya  maombi  ni jukumu msingi. Hii ni kwa sababu kati ya maingiliano, kiukweli, wote wanakusanyika kila wakati katika sala na ukimya ili kutafakari kwa undani na kutafakari yaliyomo.

Kuanza tena  siku ya Jumatatu Oktoba 9

Hakuna kazi iliyopangwa Alasiri 7 Oktoba  na Dominika 8 Oktoba. Kwa njia hiyo: Tutarejea ukumbini Jumatatu asubuhi mara baada ya misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro pamoja na mkutano mkuu wa nne ambao, utatangazwa kwa utiririshaji, na utakaoshughulikia hoja mpya ya Instrumentum Laboris  yaani kitendea kazi juu ya mada "Ushirika unaong'aa. Je tunawezaje kuwa ishara kamili zaidi na chombo cha muungano na Mungu na umoja wa wanadamu?” Baadaye, uchaguzi wa wajumbe wa tume ya ripoti ya muhtasari na tume ya habari utafanyika.

 

07 October 2023, 18:30