Tafuta

2023.10.07 Sr  Simona Brambla, M.C., mmisionari wa Consolata amechaguliwa na Papa Francisko kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume. 2023.10.07 Sr Simona Brambla, M.C., mmisionari wa Consolata amechaguliwa na Papa Francisko kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume. 

Papa amemteua Sr. Brambilla,M.C kuwa Katibu wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Wakfu!

Jumamosi tarehe 7 Okotba 2023,Baba Mtakatifu Francisko,ameteua Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume ,Mheshimiwa Sr. Simona Brambilla, M.C., wa Shirika la Wamisonari wa Consolata.Aliwahi kuwa Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Consolata Duniani.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 7 Oktoba 2023, amemteua Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume, Mheshimiwa Sr. Simona Brambilla, M.C., aliyewahi kuwa hata Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Consolata duniani.

Curriculum vitae - Wasifu wake

Sr. Simona Brambilla alizaliwa huko Monza nchini Italia mnamo tarehe 27 Machi 1965. Baada ya kupata stashahada ya kitaaluma ya uuguzi mnamo mwaka 1986, mwaka 1988 alijiunga katika Taasisi ya Masista Wamisionari wa Consolata, ambapo mnamo mwaka 1991 alifunga nadhiri za kwanza za kitawa. Mnamo mwaka 1998 alipata leseni ya saikolojia katika Taasisi ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma.

Baada ya taaluma yake ya mwisho, mnamo mwaka 1999, alikwenda Msumbiji, ambako alijishughulisha na Idara ya Kichungaji ya vijana katika Kituo cha Masomo cha Macua Xirima huko Maua. Kuanzia mwaka 2002 hadi 2006 alikuwa Profesa katika Taasisi ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana. Mnamo mwaka 2005 hadi 2011 alikuwa Mshauri wa Taasisi ya Masista Wamisionari wa Consolata. Mnamo Mwaka 2008 alipata Shahada ya Uzamivu katika Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma. Mwaka 2011 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Masista Wamisionari wa Consolata, na alichaguliwa tena hawamu ya pili mnamo mwaka 2017, hadi Mei 2023. Na tangu mnamo mwaka 2019 amekuwa mshiriki wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume.

Papa amteua Sr Brambilla kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitwa na vyama vya kitume
07 October 2023, 18:11