Tafuta

2023.10.07  makundi madogo madogo wakizungumza katika Sinodi 2023.10.07 makundi madogo madogo wakizungumza katika Sinodi  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Sinodi,Ruffini:wanawake,maskini,wahamiaji wamekuwa kitovu

Katika mrejesho wa pili kuhusu sinodi inayoendelea rais wa Tume ya Habari alionesha masuala yaliyoshughulikiwa kati tarehe 5 na 6 na katika mikutano midogo na uingiliaji wa sinodi.Miongoni mwa hayo ni marekebisho ya miundo ya Kanisa,matumizi mabaya,mazungumzo ya kidini,chaguo kwa maskini. “Umuhimu wa kujivua kisichoendana na Injili ulisisitizwa.

Vatican News

Mafunzo "ya wote", kuanzia seminari, kisha ya mapadre, walei, makatekista; wajibu wa wanawake,  huduma zilizowekwa rasmi na zisizowekwa rasmi; kiini cha Ekaristi;na  umuhimu wa maskini "kama chaguo kwa Kanisa". Na tena, majanga ya kuhama, ya kunyanyaswa, ya Wakristo wanaoishi katika hali ya mateso na dhuluma. Kuanzia na Waukraine ambao walipigiwa makofi pia katika Ukumbi wa Paulo VI. Hizi ndizo mada ambazo kazi ya Sinodi ilijikita nazo kati ya tarehe 5 alasiri na asubuhi tarehe 6 Oktoba kwa wajumbe 351 wa Mkutano Mkuu wa Sinodi kuhusu sinodi, iliyogawanywa katika makundi madogo ya wajumbe 35. Hayo yalisemwa, katika taarifa fupi tarehe 6 Oktoba 2023, katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, na Rais wa Tume ya Habari, Dk. Paolo Ruffini, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawasiliano, ambaye alifungua mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kwa kuwahakikishia kuwa : "Tutafanya kila siku kwa bidii yetu kuwapatia kila kitu tulicho nacho."

Kwa mujibu wa Dk, Ruffini alieleza, kuwa mkutano uliendelea katika Miduara midogo ambayo jioni "ilihitimisha sehemu ya kwanza ya majadiliano yao". Kikao cha asubuhi tarehe 6 Oktoba ambacho Papa Francisko alikuwepo, kiligawanywa katika sehemu mbili: ya kwanza ikiwa na ripoti 18 kutoka kwa wasemaji (waitwao "waandishi") wa vikundi tofauti katika mkutano huo; muda wa pili na watu 22 waliozungumza. Kila mmoja alipewa Dakika tatu tu  katika awamu hii "iliyobanwa zaidi kuliko nykati nyingine zinazofuata ambapo muda wa kila kuingilia kati utakuwa dakika 4".  Kwa hiyo tarehe  hiyo kila hotuba ya nne kulikuwa na kutulia  kwa ukimya na sala.

Kitabu juu ya hatua za Papa kwa wajumbe

Alasiri kazi iliendelea na sehemu kuu ya tatu. Na tena alasiri hiyo kwa mujibu wa Ruffini alitangaza kuwa, kila mmoja wa washiriki angepewa kitabu kilichochapishwa na LEV (kwa lugha ya Kiitaliano lakini chenye tafsiri za Kiingereza na Kihispania) ambacho kinakusanya maingiliano mawili: moja ya Papa na moja ya Kadinali Bergoglio wa wakati huo kinachohusu  utakatifu na ufisadi, pamoja na (utangulizi). Kanisa la "Watakatifu, sio la kidunia", tafakari mbili zilizomo kwenye kitabu hicho Bergoglio Francesco ambacho walipatiwa washiriki wa Sinodi kilichotolewa na  Nyumba ya Uchapishaji la Vatican na  kinakusanya  hatua zake mbili, na makala ya  '91 inaelezea juu ya "Rushwa na dhambi". .

Sheila Pires: Kuna utofauti na hamu ya kutembea pamoja

Miduara  tofauti ya mkao  ilikutana tena katika mazingira ya "mtangamano sana,  kama alivyosema  Sheila Pires, katibu wa Tume ya Habari, kwenye mkutano huo kwamba, "Watu wanaanza kufahamiana... Tunatembea pamoja kweli kweli." Mazingira, juu ya yote, ni ya  "furaha" hata kama, kwa kawaida, "pia hakukosekani kuwa na mvutano". Kipengele cha kuvutia zaidi, kilichomulikwa na kijana wa Afrika Kusini, ni ukweli kwamba katika kila kundi kuna watu kutoka mabara tofauti: "Kwa mfano, katika kundi langu kuna watu wanaotoka Asia, Afrika, Amerika ya Kusini /Kaskazini na kutoka Ulaya, kuna utofauti, kuna roho ya udugu, kuna hamu ya kutembea pamoja.

Pires, kama alivyokuwa Dk. Ruffini, pia aliorodhesha baadhi ya mada kwa waandishi wa habari zilizojitokeza katika vikao hivi viwili vilivyopita, akisisitiza hasa tafakari ya "Kanisa, kama familia inayokaribisha kila mtu". "Hii - alisema - ilikuwa moja ya mada zinazojirudia". Kisha, pia uekumeni na mazungumzo ya kidini, pamoja na utambuzi wa vijana na umuhimu wa ushiriki wa wanawake. Kuhusiana na hili, asubuhi tarehe 6 Oktoba Kusanyiko hilo lilifunguliwa na mtawa mmoja ambaye alisisitza "Tunajaribu kujumuisha iwezekanavyo." Kila kitu ni sehemu ya "mchakato" huu ambapo "kipaumbele ni kusikiliza", kama Papa alisema katika ufunguzi. Kusikiliza lakini pia "kujifunza kusikiliza" ni miongozo ya siku hizi za mwanzo za Sinodi juu ya sinodi, iliyoingiliwa na nyakati mbalimbali za sala na kupumzika, ambayo yanasaidia  katika kutafakari na utambuzi, alisema Sheila.

Na pia kuimarisha "vifungo vya urafiki", aliunga mkono Dk. Ruffini kwamba: "Kuna urafiki uliozaliwa katika vikundi, tulikutana na tulijitolea kujaribu kuelewa kile ambacho Kanisa linahitaji". Ilisemwa kwamba hakika kumekuwa daima na matatizo lakini vizuizi vingi vitaanguka kwa sababu marejeo yatakuwa mwili wa Kristo unaoteseka," aliongeza. Papa Fransisko  alifungua Mkutano Mkuu wa kwanza wa Sinodi ya kiinodi katika Ukumbu wa Paulo VI akiwakumbusha washiriki wote waliokusanyika katika Ukumbi huo kwamba mkutano huo “sio bunge, wala... na hivyo ni katika kusikiliza na waandishi hawana budi kumsaidia.

Mada zilizojadiliwa

Hata kwa undani zaidi, msimamizi wa Mawasiliano alieleza kuwa katika Mduara wa  mazungumzo ulimulika "mapitio ya miundo ya Kanisa kama vile Kanuni za Sheria ya Kanoni, mwelekeo wa Curia na tena, mafunzo." Ulizingatia pia mada ya uhusiano wa Mashariki na Magharibi, ukimnukuu Mtakatifu Yohane  Paulo II na kifungu chake cha kihistoria juu ya Kanisa ambalo lazima lipumue kwa "mapafu mawili". Kuhusu hali ya uhamiaji, kuna hitaji la kusindikiza wahamiaji na huduma ya askofu kama mchungaji, "msingi katika ufuataji huu", ulisisitizwa tena. Wakati juu ya nafasi na jukumu la  wanawake  na umuhimu wa kukuza sura ya kike katika Kanisa na ushiriki wake katika michakato mbalimbali ulizinduliwa tena. Wasiwasi huo huo pia ulitolewa kwa vijana na maskini, ambao walihimizwa kuondokana na  hali fulani  za  kufanya "polepole."

"Kukarabati Kanisa"

Miongoni mwa uingiliaji kati mbalimbali, pia kulikiwa na nukuu kutoka katika Msalaba wa Mtakatifu Damiano, nakala ya picha ilioko kwenye Ukumbi wa Paulo VI. Kwa hiyo “mada ya kukarabati Kanisa iliibuka.  Yaani kukarabati ni kusema tazama mimi hapa, niko katika huduma. Wale wanaojiweka kwenye huduma hurekebisha Kanisa, hutumikia utambuzi na ubashiri na kusoma alama za nyakati kwa moyo safi", alifafanua Dk. Ruffini. Zaidi ya hayo,  kuna "umuhimu wa kujivua kila kitu kisichofanana na Kristo, kama Kanisa na kama waamini" na wa kila kitu "kisichopatana na Injili" ulisisitizwa. Kwa hivyo, "kati ya mambo muhimu" ilioneshwa hatari ya "kulimbikiza madaraka badala ya hitaji la kuishi huduma". Washiriki wa Sinodi walikubaliana kwa kusema kwamba “Sinodi ni sehemu ya Kinasaba DNA ya Kanisa” na kusanyiko lote lilishughulikia wazo “kwa wale ambao hawakuweza kushiriki katika Sinodi, kwa sababu waliteswa au kwa sababu kubwa za mgogoro katika Dunia".

Zaidi ya yote, mawazo yalikwenda kwa "Kanisa linaloteseka" huko Ukraine: "Kutikisa vichwa kulifanywa na kuibua kupiga makofi", alisema Dk. Ruffini, huku akielezea kwamba hii ilikuwa njia ya "kujisikia katika ushirika" na "watu wa Ukraine walio vitani na Wakristo” wanaoteseka mfululizo. Mzunguko mwingine wa makofi,  lakini kwa sababu tofauti ulitolewa kwa Sr. Letizia Salazar ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa  na Askofu Mkuu Charles Scicluna, kwa kumbukumbu ya ukumbusho wake wa uaskofu. Ishara, hizi pia, zilirejesha hali nzuri ya kukumbuka na ambayo inaundwa katika mkutano huo.

Mahojiano na Kardinali Müller

Maswali kadhaa yaliulizwa kwa zaidi ya moja kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuhusu ushiriki wa Kardinali Gherard Ludwig Müller, aliyekuwa Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa la  Mafundisho Tanzu ya Kanisa  wakati wa mkutano huo katika kipindi cha televisheni cha Marekani tarehe 5 Oktoba kuzungumzia kazi ya sinodi. Kulingana na baadhi ya waandishi wa habari, mahojiano hayo yatapingana na maelekezo ya  Papa kwa wajumbe wa Sinodi ya kuzingatia "kufunga maneno kwa umma" katika majuma ya  hivi karibuni. Mtu mwingine  pia aliuliza ikiwa kuna "adhabu" zilizopangwa. Dk. Ruffini alijibu kwa utani: "Kutoka kwa nani, kutoka kwangu?", Baadaye akaelezea kwamba kuna "utambuzi katika ukimya. Hakuna polisi anayeadhibu... Ni mkusanyiko wa kaka na dada ambao wamejipatia muda wa kusimamia kazi. Kuna utambuzi wa kibinafsi ulioombwa  na Papa kutoka kwa washiriki na pia kutoka kwao katika kuelezea ni nini  tunachozungumza." Na "utambuzi huu huachiwa kila mtu."

DK RUFFINI HABARI ZA SINODI
07 October 2023, 14:28