Ufunguzi wa Sinodi,Papa anasema Sinodi sio bunge!
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Hatuhitaji mtazamo wa karibu, unaoundwa na mikakati ya kibinadamu, hesabu za kisiasa au vita vya kiitikadi ambavyo wanajisingizia wenyewe, na ikiwa Sinodi itatoa ruhusa hii, kufungua mlango huu, mwingine ... hii haitakuwa na faida. Hatuko hapa kutekeleza mkutano wa bunge au mpango wa mageuzi. Sinodi, ndugu wapendwa, sio bunge, mhusika mkuu ni Roho Mtakatifu. Hatupo hapa kushikilia bunge, hapana: tuko hapa kutembea pamoja na macho ya Yesu, aliyembarikiwa na Baba na kuwakaribisha wale waliochoka na kukandamizwa. Kwa hiyo na tuanze kutoka katika mtazamo wa Yesu, ambao ni mtazamo wa baraka na ukaribishaji.
Ni maneno mazito yaliyosikika katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kufungua Sonodi ya XVI ya Kawaida ya Maaskofu Jumatano tarehe 4 Oktoba ambayo itaendelea hadi 29 Oktoba 2023. Kabla ya kuanza, washiriki 464 wamekuwa kwenye mafungo ya kiroho tangu Jumamosi jioni tarehe 30 Septemba 2023 hadi tarehe 3 Septemba 2023.
Katika mombi kwa lugha mbali mbali kulikuwa na sala ya Kiswahili iliyosomwa na Padre Mtui, OSA: Kwake Yeye anayewafunulia watoto wachanga mafumbo ya ufalme wake, amjalie anayeshiriki shughuli za kisinodi, roho iliyo wazi kwa maongozi ya Roho Mtakatifu, katika kusikiliza ndugu, wenye kuhitaji wa Kanisa katika ulimwengu wa leo.
Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo umjalie Papa Francisko kuongozwa kwa hekima ya kiinjili katika safari ya Kanisa lililotawanyika ulimwenguni ili liwe ishara ya Udugu na Matumaini kwa wote.
Ee Mungu wa Kila faraja uwajalie makardinali wapya na ndani ya Baraza la makardinali kuhamasishana kwa ushirikiano katika huduma ya kitume ya Papa, katika kuwatunza wale ambao wamechoka na waliokandamizwa.
Mara baada ya misa Takatifu, Radio Vatican ilizungumza na baadhi ya watanzania waliokuwapo kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro ambao walionesha furaha kubwa ya ushiriki na kuguswa sana. Katika maelezo yao wanaelezea hisia zao za siku ya leo, mahubiri ya Papa kuhusu Sinodi kama kiini na pia furaha ya kuwa na Kardinali mpya Protase Rugambwa, Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora Tanzania.