Kila Jumamosi ya Oktoba ni Rosari aux flambeaux katika Uwanja wa Mt.Petro
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Mwezi wa kumi kama ilivyo mwezi wa tano wa kila mwaka ni mwezi wa Mama Maria, mwezi wa kusali Rosari, kumuomba Mama Maria, Mama wa Yes una Mama wa Mungu amani ya dunina na kwa watoto wake, wanahohitaji ulinzi wake. Ni katika muktadha huo ambapo Jumamosi tarehe 7 Oktoba 2023 katika kumbukizi ya Bikira Maria wa Rosari, Matendo ya Rosari aux flambeaux na maandamano na mishumaa mikubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro itafanyika kuanzia saa 3.00 kamili usiku ambayo ni moja ya mipango wa sala ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika kipindi chote cha mkutano Mkuu wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu ulioanza tarehe 4 Oktoba na utahitimishwa tarehe 29 Oktoba 2023.
Washiriki mkutano huo wanaalikwa kushiriki sala hiyo na watu wotr wenye mapenzi mema. Hata hivyo taarifa inabainisha kuwa kila Jumamosi, usiku kwa mwezi wote wa Oktoba, sala ya Rosari itafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Atakayeongoza Rosari ya Jumamosi 7 Oktoba 2023 ni Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi.
Nyote mnaalikwa kushiriki kiroho au kimwili kusali.