Tafuta

Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswiss. Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswiss.  (BENEDETTA BARBANTI)

Vatican:inasikitisha baada miaka 75 ya haki za binadamu bado udugu unakanyagwa

Badala ya roho ya udugu ambayo jumuiya ya kimataifa ilijitolea,mara nyingi sana leo mtu yeyote anayeonekana kuwa dhaifu,maskini au asiye na thamani kulingana na kanuni fulani za kiutamaduni hupuuzwa,hutengwa au hata kuchukuliwa kuwa tishio kwa kuondolewa.Ni katika hotuba ya mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika mkutano kuhusu haki za binadamu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Katika hotuba ya Askofu Mkuu Ettore Balestrero  Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, katika mjadala  mkuu wa 53 wa Baraza kwa ajili ya Haki za Binadamu, tarehe 13 Septemba 2023 alisema kuwa baaadaye mwaka huu, Jumuiya ya Kimataifa na Baraza hilo litaadhimisha Miaka 75 ya kupitishwa kwa Tamko la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (UDHR). Jiwe hili la msingi la mfumo wa kimataifa wa leo hii limejengwa juu ya imani kwamba Binadamu wote wamezaliwa huru na sawa katika utu na haki. Wamejaliwa kuwa na akili na dhamiri na wanapaswa kutendeana wao kwa wao kwa roho ya udugu. Ni ukweli wa kusikitisha wa historia kwamba imani hii iliwekwa ndani ya UDHR baada tu ya uharibifu na hasara ya mamilioni ya maisha katika Ulimwengu wa vita vya Pili.   

Kwa upande wa Vatican hata hivyo, amebainisha kuwa inasikitisha zaidi kwamba miaka 75 baadaye, wengi wa kaka na dada zetu bado wanateseka kwa sababu ya vita, migogoro, njaa, ubaguzi na unyanyasaji. Badala ya "roho ya udugu" ambayo jumuiya ya kimataifa ilijitolea bila shaka, mara nyingi sana leo, mtu yeyote anayeonekana kuwa dhaifu, maskini au asiye na "thamani" kulingana na kanuni fulani za kiutamaduni hupuuzwa, hutengwa au hata kuchukuliwa kuwa tishio kwa kuondolewa. Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican alisema kwa kuzingatia ukiukwaji wa mara kwa mara wa haki za binadamu unaotokea duniani leo, maadhimisho ya miaka 75 ya kupitishwa kwa UDHR yanatoa fursa muhimu ya kutafakari kanuni hizo za kimsingi zinazozuia ulinzi wa haki za binadamu. UDHR, kwanza kabisa, ni ya ulimwengu wote. Watu wote, bila ya utofauti wa aina yoyote, kimaumbile na bila kutengwa wana utu wa kibinadamu. Hii haimaanishi tu kwamba kila mtu anapaswa kuheshimiwa, lakini pia inamaanisha kwamba kila mtu anapaswa kuthaminiwa kwa mchango wake wa kipekee anaoleta kwa jamii. Kwa bahati mbaya, mara nyingi ni watu walio katika mazingira magumu zaidi ambao wanabaguliwa na kutengwa.

Mwakilishi wa Vatican aliendelea kukazia kuwa Wahamiaji na wakimbizi, wazee, wagonjwa, wasiozaliwa na maskini, kwa kutaja wachache tu, mara nyingi huwekwa kando ya jamii au hata kutupwa. Ili kupambana na mielekeo hii, ni muhimu kupitisha chaguo la upendeleo kwa maskini na waliotengwa, kudumisha haki zao za ulimwengu wote na kuwawezesha kustawi na kuchangia kwa manufaa ya wote. Kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosema, “mara nyingi watu dhaifu zaidi wanatupwa, wanachukuliwa kuwa hawana maana na ni muhimu kupambana na utamaduni wa kutupa na kukumbusha kila mtu kwamba utofauti ni utajiri ambao haupaswi kamwe kuwa sababu ya kutengwa au ubaguzi.” Haki za binadamu zilizoainishwa katika UDHR hazijatolewa kwa mtu yeyote, bali zinakuwepo hati yoyote.

Tamko la Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, Kifungu cha 1. 2 linawakilisha utambuzi wa pamoja na jumuiya ya kimataifa wa maadili ambayo hayatenganishwi na maana ya kuwa binadamu. Kwa hivyo, bila kujali kama kuna majukumu maalum ya kisheria au la katika mahali na wakati fulani, maadili ya UDHR lazima yaheshimiwe kwa watu wote wakati wote. Kwa kuzingatia hadhi na utu wa binadamu, haki za binadamu si tu upendeleo unaotolewa na maafikiano ya jumuiya ya kimataifa kwa watu binafsi. Badala yake, zinawakilisha maadili hayo yenye malengo, yasiyo na wakati ambayo ni muhimu kwa ajili ya kusitawi kwa mwanadamu. Hii ina maana kwamba hata kama jamii au jumuiya ya kimataifa itakataa kutambua haki moja au zaidi zilizojumuishwa katika UDHR, hilo halitapunguza uhalali wa haki hiyo, wala haliwezi kutoa udhuru kwa mtu yeyote kuiheshimu.

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican aidha alisema hii inamaanisha pia kwamba kinachojulikana kama haki mpya hazipati uhalali kwa sababu tu watu wengi au Mataifa wanazidai. Mfano mbaya zaidi leo wa uelewa huu mbovu wa haki unawakilishwa na makadirio ya maisha ya binadamu milioni 73 yasiyo na hatia ambayo hukatizwa kila mwaka tumboni, kwa kisingizio cha mada ya  “haki ya kutoa mimba.” Mtazamo chanya unaweza kuona haki za binadamu kama seti ya uhuru inayotolewa kwa kila mtu na, kwa hivyo, seti inayolingana ya mipaka iliyowekwa kwa wengine ili kuheshimu haki hizo. Mtazamo kama huo, hata hivyo, ungepunguza mwingiliano wa kibinadamu kuwa aina ya ubinafsi, ambapo haki za mtu mmoja zinapingana na haki za wengine. Sifa ya Azimio la Kimataifa ni kwamba imewezesha tamaduni tofauti, misemo ya kisheria na mifano ya kitaasisi kuungana karibu na msingi wa maadili, na kwa hivyo haki.

Mwakilishi wa Vatican na utetezi wa haki za binadamu
15 September 2023, 16:38