Tafuta

Chuo Cha Kipapa cha Urbaniana, Roma Chuo Cha Kipapa cha Urbaniana, Roma 

Papa afanya teuzi katika nafasi za taasisi za Kipapa kuanzia na Urbaniana!

Baba Mtakatifu Francisko amefanya teuzi mbalimbali zikiwemo Mjumbe wa Kipapa kwa Urubaniana,Buonomo,Rais mpya wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi ya Kihistoria,Padre Marek Andrzej Inglot na Katibu Msaidizi mpya wa Baraza la Utamaduni na Elimu,Padre Antonio Spadaro.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko,tarehe 14 Septemba 2024 amefanya teuzi mbali mbali katika mabaraza na taasisi za kipapa.  Awali ya yote kwa kuteuliwa kwa Profesa Vincenzo Buonomo kuwa Mjumbe mpya wa Kipapa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma. Kwa uteuzi huo Papa ameambatanisha hata hati. Katika hati hiyo anaandika kuwa kwa kutambua hitaji la kurekebisha huduma na kazi ya Chuo Kikuu cha Urbaniana kulingana na mahitaji ya wakati wa sasa, anaitwa kuchangia utendaji wa kimisionari wa Kanisa unaohitaji kukua katika kutafsiri Neno lililofunuliwa na katika kuelewa ukweli pia kwa njia ya kitaaluma, kiutamaduni,  shughuli na kisayansi ili kuwafunza wale walioitwa kushirikiana katika utangazaji wa Injili, katika kukuza maisha ya imani na katika serikali katika maeneo ya uinjilishaji wa kwanza (Rej. Praedicate Evangelium, 61-63)”Kwa hiyo “Baada ya kuzingatia kile ambacho Kansela alinieleza kuhusu uharaka wa kupitia upya muundo wa Chuo Kikuu na kuafikiana na Katiba ya Veritatis Gaudium Sheria na masharti mengine ya udhibiti ambayo yanatawala maisha ya Vitivo na Taasisi, pamoja na kuhakikisha marekebisho ya shirika la kiutawala kwa sheria inayotumika kwa Miili ya Vatican.”

Profesa Vincenzo Buonomo
Profesa Vincenzo Buonomo

Kwa hiyo Profesa Buonomo, ambaye atachukua jukumu hilo kuanzia tarehe 1 Oktoba 2023, atatekeleza wajibu wake kwa makubaliano na Kansela Mkuu na Wasimamizi wa Kitengo cha Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya maalumu ya Uinjilishaji, “kuripoti kwangu moja kwa moja masuala ya umuhimu mkubwa zaidi na pia itapendelea kuingizwa kwa lazima kwa Chuo Kikuu cha Urbaniana katika mchakato ulioanzishwa unaotamaniwa na Papa na kuratibiwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu unaolenga kupanga upya Taasisi za Kipapa za Kitaaluma za Kirumi ambazo zinasimamiwa moja kwa moja kutoka Vatican.

Rais wa Taasisi ya Kipapa ya Kamati ya Kisayansi ya Historia

Baba Mtakatifu Francisko vile vile amemteua rais wa Taasisi ya Kipapa ya  Kamati ya Kisayansi ya kihistoria, Padre Marek Andrzej Inglot, S.I.,  Profesa wa kawaida katika Kitengo cha Historia na mali za utamaduni za Kanisa, katika Chuo Kikuu ca Kipapa Gregoriana, Roma (Italia). Padre  Marek Andrzej Inglot, S.I., alizaliwa tarehe 25 Machi 1961 huko Brzozów Poland. Alijiunga na Shirika la Kijesuit  mnamo 1980, na kupewa daraja la upandre mnamo tarehe 29 Juni 1988 alifunga nadhiri za daima mnamo tarehe 22 Agosti 1997.  Alipata shahada ya udaktari katika Historia ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma nel 1995.  Tangu 1993 anafundisha katika Kitivo cha Hisotria na Mali za utamaduni wa Kanisa , katika Chuo hicho ambapo alikuwa  hada Decano. Aidha ni mjumbe wa Kamati ya Kipapa ya Sayansi za Kihistoria tangu 17 Machi 20220.

Uteuzi wa Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 14 Septemba 2023 amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Elimu na Utamaduni, Mheshimiwa Padre Antonino Spadaro, S.I., ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mkurugeniz wa Gazeti la Civiltà Cattolica.  Atachukua nafasi hiyo kuanzia tarehe Mosi Januari 2024. Padre Antonino Spadaro, S.I.,  alizaliwa tarehe 6 Julai 1966 huko Messina (Italia). Baada ya shahada ya Falsafa katika Chuo Kikuu cha Mafunzo huko Messina mnamo 1988, alijiunga kwenye unovisi kwenye Shirika la Yesu( Wajesuit).

Kunako tarehe 21 Desemba 1996  alipewa dawaja la Upadea na 24 Mei 2007 akafunga nadhiri za daima katika shirika la Wajesuit. Kunako 2022 aliendelea na masomo ya shahada ya Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma. Alijumuishwa katika Bodi ya Waandishi la Gazeti 'La Civiltà Cattolica' mnamo 1998, akawa Mkurugenzi wake mnamo 6 Septemba 2011. Ni mshauri wa Baraza la kipapa la Utamaduni na Elimu na Mjumbe wa Kawaida wa Taasisi ya Kipapa la Elimu ya Uzuri wa sana ana Fasihi ya mafunzo ya  fadhili za  Pantheon.

Katibu Msaidizi wa kitengo cha kidiplomasia ya Vatican

Baba Mtakatifu Francisko  amemteua Katibu msaidizi kwa ajili ya kitengo cha  wafanyakazi wa kidiplomasia wa Vatican Monsinyo Joseph Murphy, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mkuu wa Protokali za Katibu wa Vatican.

Papa amefanya teuzi kadhaa katika taasisi za Vatican.
14 September 2023, 17:30