Tafuta

 Dk. Ruffini ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Sinodi kwa mawasiliano. Dk. Ruffini ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Sinodi kwa mawasiliano. 

Mafungo ya kiroho kwa washiriki wa Sinodi huko Sacrofano Roma hadi 3 Oktoba

Mafungo ya kiroho kwa wajumbe ndugu na wageni maalum watakaoshiriki Sinodi ya kisinodi kuanzia tarehe 4 Oktoba katika mkutano mkuu wa kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu yanaanza tarehe 30 Septemba hadi tarehe 3 Oktoba jioni.Mafungo hayo yanaongozwa na tafakari za Sr.Ignazia Angelini na Padre Tomothy Radcliffe.

Vatican News

Mafungo ya  kiroho yataanza tarehe 30 Septemba 2023 mara baada ya mkesha wa sala ya kiekumeni jioni kwa washiriki wa Sinodi ambao watafikia huko Domus ya Fraterna ya Sacrofano kwa Bus. Kuondoka kutoka mjini Vatican kumepangwa saa 2.30 Usiku. Mafungo yataisha siku ya Jumanne tarehe 3 Oktoba 2023 baada ya chakula cha jioni na tarehe 4 Oktoba 2023 itakuwa ni ufunguzi rasimi kwa misa takatifu itakayoongozwa na Baba Mtakatifu pamoja na makardinali wapya.

Katika Siku za  mafungo kuanzia Dominika, Jumatatu na Jumanne zitagawanywa kama ifuatavyo: saa 2.45 masifu ya Asubuhi pamoja na tafakari ya  Sr. Ignazia Angelini. Saa 3.30 - 5.30, tafakari za Padre Tomothy Radcliffe ikifuatiwa na ukimya na sala ya kibinafsi. Baada ya chakula cha mchana, alasiri, mikutano ya kikundi na  mazungumzo katika Roho imeratibiwa. Misa Takatifu itafuata ikitanguliwa na tafakari ya pili ya Sr Ignazia Angelini na hatimaye chakula cha jioni. Tafakari za Sr Angelini na Padre Radcliffe na Misa Takatifu zitakuwa zikitangazwa na Vyombo vya Habari vya Vatican na maandishi ya tafakari hiyo yatachapishwa na Ofisi ya Habari Vatican.

30 September 2023, 12:55