Tafuta

2023.09.08 Baselios Marthoma Mathews Mkuu Kanisa la Kiorthodox la Malankara. 2023.09.08 Baselios Marthoma Mathews Mkuu Kanisa la Kiorthodox la Malankara. 

Septemba 11,Papa atakutana na Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la Malankara

Baselios Marthoma Mathews III kwa mara ya kwanza katika ziara rasmi na Papa baada ya kuchaguliwa kwake 2021.Mkutano pia umepangwa kukutana na Baraza la Kipapa la KuhamasishaUmoja wa Wakristo na Ibada ya Ekaristi Takatifu,Septemba 10,katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta,Roma na waamini wa Jumuiya ya Kiorthodox ya Siria Malankara wanaoishi Roma.

Vatican News.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Vyombo vya habari Vatican kwa waandishi wa habari ni kwamba Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox wa Kisiria Malankara, Baselios Marhoma Mathews III atakutana na Baba Mtakatifu  Francisko tarehe 11 Septemba 2023 ambapo utakuwa  mkutano wa kwanza rasmi jijini Vatican, tangu alipochaguliwa kunako 2021 katika mwaka wa 10 wa ziara ya mtangulizi wake Baselios Marthoma Paulose II, ikiwa pia ni mwaka wa 14 wa ziara ya kwanza mjini Roma kwa Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox wa Siria Malankara.

Baada ya Mkutano huo wa faragha na Baba Mtakatifu Baselios Marthoma Mathews III atatembelea hata Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo. Dominika tarehe 10 Septemba 2023 , Mkuu huyo ataadhimisha Liturujia ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, Roma  kwa waamini wa Jumuiya ya Kirthodox wa Siria malakara wanaoishi Roma.

Papa atakutana na kiongozi wa kiorthodox wa malakara
08 September 2023, 16:38