Tafuta

2023.09.14 Papa amekutana na mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde 2023.09.14 Papa amekutana na mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde  (Vatican Media)

Papa Francisko amekutana na Mfalme wa Ubelgiji Philip na Malkia Mathilde

Papa Francisko amekutana na Mfalme Philip wa Ubelgiji na Malkia Mathilde katika Jumba la Kitume, mjini Vatican ambapo mara baada ya mazungumzo yao, amekutana na Askofu Mkuu Ghallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Alhamisi tarehe 14 Septemba 2023 asubuhi, Baba Mtakatifu Francisko aamekutana na Mfalme wa Ubelgiji na Philip na Mke wake Malkia Mathilde katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Mara baada ya Mkutano huo, alikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,  Katibu wa Vatican wa Masuala ya Mahusiano Na Nchi  na Mashirika ya Kimataifa.

Papa akisalimiana na Mfalme wa Ubelgiji
Papa akisalimiana na Mfalme wa Ubelgiji

Kwa mujibu wa habari kutoka Ofisi ya  habari mjini Vatican,  imebainisha kuwa, wakati wa mazungumzo yake na Katibu wa Vatican, wameonesha kuwa na  mahusiano mazuri kati ya Vatican na nchi ya Ubelgiji, kwa kusisitizia nafasi ya imani ya kikristo na Kanisa Katoliki.

Mfalme na Malkia wakiwa na Askofu Mkuu Gallagher
Mfalme na Malkia wakiwa na Askofu Mkuu Gallagher

Katika mchakato wa mazungumzo hayo pia wametazama masuala ya pamoja na baadhi ya matatizo yenye tabia ya kimataifa, kwa namna ya pekee kuhusiana na Afrika hadi vita nchini Ukraine na jitihada zao kwa ajili ya amani kati ya watu.

Zawadi

Kwa upande wa zawadi kati ya viongozi hao wakuu, kwa muda wa dakika hizo chache Baba Mtakatifu amempatia Mfalme Mchoro wa shaba unaoonesha maelezo ya mlango wa kati wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na  idadi za hati za upapa kuanzia na Ujumbe wa Amani kwa mwaka huu 2023. Kitabu kinachohusu katekesi za Kipapa zilizoandaliwa na Nyumba ya Kipapa na hatimaye kitabu cha Picha kuhusu Statio Orbis yaani Njia ya msalaba tarehe 27  Machi 2023, kilichoandaliwa na Nyumba ya Uchapishaji Vatican (LEV).

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi

Kutoka kwa Wafalme

Kazi ya udongo wa msanii wa Ubelgiji inayoonesha Mchungaji Mwema

Wakiwa wanasindikizwa wafalme  baada ya kukutana na Papa
Wakiwa wanasindikizwa wafalme baada ya kukutana na Papa
Papa akutana na wafalme wa Ubelgiji
14 September 2023, 17:13