Tafuta

2023.09.14 Papa akutana na wahusika wa Filamu ya 'Mimi Kapteni.' 2023.09.14 Papa akutana na wahusika wa Filamu ya 'Mimi Kapteni.'  (Vatican Media)

Papa ampokea mkurugenzi Garrone na baadhi ya wahamiaji kutoka katika filamu Mimi Kapteni

Katika Maktaba ya Filamu ya Vatican tarehe 14 Septemba kuna kuonyeshwa kwa filamu inayoelezea janga la wahamiaji wa Kiafrika wanaojaribu kufika Ulaya.Papa Francisko amekutana na mkurugenzi na wachezaji wa filamu hiyo.

Vatican News

Mapema alasiri tarehe 14 Septemba 2023 katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, Baba Mtakatifu  Francisko alimpokea mkurugenzi Matteo Garrone, akiambatana na baadhi ya waigizaji wa filamu yenye kichwa: “Mimi Kapteni”, ambayo ilishinda  tuzo ya 'Simba ya Shaba' kwenye Tamasha la Filamu la Venezia Italia.

Papa Francisko amekutana na wahusika wakuu wa Filamu "Mimi ni Kapteni" inaeleza janga la uhamiaji
Papa Francisko amekutana na wahusika wakuu wa Filamu "Mimi ni Kapteni" inaeleza janga la uhamiaji

Hayo yameripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican na kufahamisha kuwa imepangwa kufanyika onesho maalum la filamu hiyo, lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano saa kumi na mbili jioni katika chumba cha Maktaba ya Filamu ya Vatican, mbele ya mkurugenzi na baadhi ya wahusika wakuu na Mamadou Kouassi, ambaye kutokana na uzoefu wake wa maisha, njama ya filamu ilihusika moja kwa moja.

Papa akutana na wahsika wa filamu iitwayo mimi kapteni

 

14 September 2023, 18:02