Tafuta

2023.09.15Askofu Raymond Tapiwa Mupa, ameteuliwa kuwa askofu wa Jimbo la  Masvingo Nchini Zimbabwe. 2023.09.15Askofu Raymond Tapiwa Mupa, ameteuliwa kuwa askofu wa Jimbo la Masvingo Nchini Zimbabwe. 

Papa amemteua Askofu Tapiwa Mupa kuwa Askofu wa Masvingo

Baba Mtakatifu Francisko,tarehe 15 Septemba 2023 amemteua Askofu wa Jimbo Masvingo nchini Zimbabwe Askofu Raymond Tapiwa Mupa, C.Ss.Na katika ujumbe wake mfupi Papa anasema "kutoka kwa Maria wa Mateso tunajifunza kuwa ikiwa tunabaki na uhusiano na Mungu,hatuendolewi mateso ya maisha."

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Mnamo tarehe 15 Septemba 2023 Baba Mtakatifu Francisko, amemteua Askofu wa Jimbo Masvingo nchini Zimbabwe, Askofu  Raymond Tapiwa Mupa, C.Ss.R.,  ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Chinhoyi nchini Zimbabwe.   Askofu Raymond Tapiwa Mupandasekwa alizaliwa tarehe 28 Aprili 1970 na alikuwa Askofu wa Jimbo  Katoliki la Chinhoyi tangu tarehe 7 Aprili 2018. Na  alikuwa ni askofu wa kwanza mweusi wa Jimbo la  Chinhoyi. Na Askofu wa kwanza mweusi wa Shirika la Mkombozi kwa Kiafrika huko Zimbabwe, lakini pia kwa shirika zimakwa upande wa Afrika Mkombozi(Congregation of the Redemptorists),lambalo limeena sehemu mbali mbali za dunia iloanzishwa na Mtakatifu anayejulikana sana Alfonsi Maria de Liguori.

Maadhimisho ya Siku Kuu ya Mama Maria wa mateso saba

Kila tarehe 15 Septemba ya kila mwaka, Mama Kanisa anakumbuka Mama Maria wa Mateso saba, siku moja baada ya Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba. Katika furaha hiyo, Baba Mtakatifu, ameandika ujumbe wake kupitia mitandao ya kijamii kuwa: “Kutoka kwa Maria wa Mateso tunajifunza kuwa ikiwa tunabaki na uhusiano na Mungu, hatuendolewi mateso ya maisha lakini unafunguliwa upeo mpana wa mema na kutembea ndani mwake kuelekea utimilifu.” Asili ya siku kuu hii ilikuwa ni mnamo tarehe 9 Juni 1668, Baraza la Kipapa la wakati ule la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti liliruhusu kuadinisha Misa kwa heshimia ya huzuni saba za  Mwenyeheri Bikira likitaja katika katika Hati hiyo kwamba Wanashirika wa Watumishi wa Maria waweze kuvaa  mavazi meusi  kwa ajili ya  kumbukumbu ya ibada ya Maria na huzuni ambayo yeye alifanya uzoefu katika mateso ya Mwanawe.

Ibada ya Mater Dolorosa

Na ibada hiyo kwa ajili ya Mater Dolorosa, Mama wa Mateso  iliyoenea sana hasa katika nchi za Mediterania, iliendelezwa tangu  mwisho wa karne ya XI. Ilikuwa ni Papa Pio VII aliyeiingiza katika kalenda ya kiliturujia ya Kirumi mnamo mwaka 1814, akiiweka  kuadhimisha kila tarehe 15 Septemba. Picha ya Mama wa Huzuni ambaye anaonesha Mateso ya Mwanawe imekuwa uwakilishi maarufu katika sanaa, muziki mtakatifu na uchaji wa Mungu. Kwa hiyo Heshima  ya watu wa Mungu kwa ibada ya Mateso ya Maria  imekuwa ikifanyika kwa karne nyingi. Nyimbo zimeandikwa kwa heshima ya Mama Yetu wa Huzuni: alikuwa chini ya msalaba na wanamtafakari pale, akiteseka. Ucha Mungu wa Kikristo umekusanya huzuni za Maria na unazungumza juu ya ‘huzuni saba.’ Mateso ya  kwanza,  tayari ni katika siku 40 tu baada ya kuzaliwa kwa Yesu, unabii wa Simeoni ambaye alizungumza juu ya upanga ambao utachoma moyo wake (taz. Lk. 2:35).

Mateso ya Mama Yesu Maria akimsindikiza mwanae Yesu

Mateso ya pili, yanafikiri juu ya kukimbilia Misri kuokoa maisha ya Mwana (rej. Mt. 2,13-23). Mateso ya tatu ni  siku tatu za uchungu wakati mtoto alibaki hekaluni (taz. Lk. 2:41-50). Mateso ya nne, Mama Yetu anapokutana na Yesu njiani kuelekea Kalvari (taz. Yoh. 19:25). Maumivu ya tano ya Mama Yetu akiona  kifo cha Yesu, na kumwona Mwanae pale, amesulubiwa, uchi, akifa. Mateso ya sita, akishuka Yesu kutoka msalabani, mekufa, na anamchukua mikononi mwake kama vile alivyokuwa amemchukua mikononi mwake zaidi ya miaka 30 mapema huko Bethlehemu. Mateso  ya saba ni kuzikwa kwa Yesu. Na kwa hivyo, uchamungu wa Kikristo unafuatilia njia hii ya Mama Maria  anayefuatana na Yesu. “Ndugu wapenda leo hii basi nasi tuombe maumivu hayo saba kama kumbukumbu ya Mama wa Kanisa, kama Mama wa Kanisa aliyetuzaa sisi sote kwa uchungu mwingi.” Alisema hivyo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Mahubiri ya Ijumaa Kuu tarehe  3 Aprili 2020 kwa kujikita na mada ya Mwenye uchungu na Mama.

Uteuzi wa Askofu wa Masvingo na mateso ya Maria
15 September 2023, 16:15