Tafuta

2023.09.16 Card. Konrad Krajewski na Askofu Mkuu Pietro Marini katika misa ya mazishi ya mtu hasiye na makazi 2023.09.16 Card. Konrad Krajewski na Askofu Mkuu Pietro Marini katika misa ya mazishi ya mtu hasiye na makazi 

Mirko hasiye na makazi bila uso amezikwa kwa hadhi

Katika Kanisa la Mtakatifu Monica,Kardinali Krajewski aliongoza mazishi ya Mslovakia asiye na makazi ambaye alikufa akiwa na umri wa miaka 60 kutokana na saratani iliyomeza 90% ya uso wake.Hii ndiyo sababu kila mara alitembea na leso juu ya uso wake. Akiwa ametelekezwa kwenye bustani moja huko Roma.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Miroslaw Mirko kwa urafiki wake hakuwa na uso tena bali uso wa Kristo tu anayeteseka. Mslovakia, mwenye umri wa miaka 60 hivi, akiwa na saratani ilimfanya kubaki na mdomo wake tu ukiwa mzima, akimmeza macho, pua na sehemu nzuri ya uso wake. Walimwita mtu mwenye pazia,​​kwa sababu ya kitambaa alichotumia kujifunika; hakuweza kugugumia maneno machache, kupiga kelele alipoona mtu anajaribu kumsaidia na kumeza chakula. Kisha, baada ya mwaka aliotunzwa katika Jumba la Migliori, jengo lililo umbali  kidogo kutoka Nguzo ya Mtakatifu Petro, ambalo kwa matashi ya Papa kwa ajili ya maskini wote katika eneo hilo alianza kutabasamu.

Mirko alifariki tangu mwezi Agosti 2023 lakini kutokana na taratibu mbalimbali za ukiritimba  kwa wageni, mazishi hayo yameadhimishwa tarehe 16 Septemba 2023 katika Kanisa la Mtakatifu  Monica lililopo Katika Uwanja wa Maeneo Matakatifu na Ni kikanisa cha Waagostiniani. Misa hiyo iliongozwa na Kadinali Konrad Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo na kusindikizwa na umati wa watu wapatao mia moja, wakiwemo mapadre, watawa, watu wa kujitolea , wawakilishi wa Ubalozi wa Slovakia na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ambayo inasimamia Jengo hilo na huduma  na watu maskini wapatao hamsini ambao mtu huyu amekuwa rafiki kwao. Ishara kwamba Mirko hakufa peke yake, katika eneo la kutojali na uharibifu ambao alikuwa ameishi kwa miaka, ambapo mara moja alikuja Italia kutoka Austria, katika bustani ya Aventine Hill kati ya nzi na mchwa.

Kukaa karibu naye wakati huu ilikuwa ni kama kutufanyia mazoezi ya kiroho, hakuwahi kulalamika, hajawahi kufanya maombi, aliridhika na tulichomletea na alisema asante kila wakati, alisisitiza, kwa ishara ya hisia, Kardinali Krajewski. Ni yeye alionywa na ripoti kuhusu mwanamume mwenye leso usoni akilala kwenye bustani  ambaye alimshawishi Mirco kupata kimbilio katika Jumba lililozinduliwa mnamo 2019. “Nilienda huko kumtembelea, lakini hakupenda kuhamishwa, kwa sababu alisema kwamba alitaka kufa huko, akiwa amezungukwa na wadudu. Nikamwambia: tazama, tunaweza kutengeneza nafasi katika bustani ya Vatican. Halafu unajua jinsi alivyosadiki? Nilipomwambia: Papa Francisko anakualika kwenye bweni jipya. Akajibu: nenda vizuri, lakini nitakwambia baada ya siku tatu. Na baada ya siku tatu, alisema ndio.”

Mazishi mjini Vatican kwa mtu hasiye na makazi

 

18 September 2023, 18:19