Tafuta

Shoah: Zimepatikana hati zenye orodha ya Wayahudi waliokolewa kwenye komventi za watawa jijini Roma. Shoah: Zimepatikana hati zenye orodha ya Wayahudi waliokolewa kwenye komventi za watawa jijini Roma.  (ANSA)

Majina ya Wayahudi yaliyolindwa na taasisi za kidini huko Roma yamepatikana

Nyaraka zilizopatikana katika kumbukumbu za Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia na ambayo inajumuisha orodha ya wale waliolindwa dhidi ya wanazi na mashirika ya kike na kiume ya watawa zilizowapatia hifadhi zimewasilishwa tarehe 7 Septemba,kwenye Jumba la Makumbusho la Kumbu kumbu ya Wayahudi Jijini Roma.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Hati ambayo haijachapishwa ambayo inaorodhesha watu wengi wa Kiyahudi waliohifadhiwa na kulinwa katika  makao ya taasisi za Kikatoliki jijini Roma walipokuwa wakikimbia mateso ya Wanazi zimegunduliwa tena katika jumba la kumbukumbu ya Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia huko Roma. Orodha ya wanawake 100 na wanaume 55 watawa wa mashirika ya kitawa, kike na kiume yaliyotoa ukarimu, pamoja na idadi ya watu waliohudhuria iliyoshughulikiwa nao,ilikuwa tayari imechapishwa na mwanahistoria Renzo de Felice mnamo 1961, lakini hati kamili ilikuwa imepotea. Orodha mpya zilizogunduliwa upya zinarejea zaidi ya watu 4,300 kati yao 3,600 wametambuliwa kwa majina.

Ulinganisho na hati hizo zilizowekwa kwenye kumbukumbu ya Jumuiya ya Wayahudi wa Roma inaonesha kwamba 3,200 hakika walikuwa Wayahudi. Ya mwisho inajulikana  hata ni wapi walikuwa wamefichwa na katika hali fulani waliishi kabla ya mateso. Nyaraka hivyo kwa kiasi kikubwa inaongeza taarifa juu ya historia ya uokoaji wa Wayahudi katika muktadha wa taasisi za Kikatoliki za Roma. Kwa sababu za ulinzi wa faragha, ufikiaji wa hati kwa sasa imezuiwa. Hati hiyo iliwasilishwa katika warsha iliyofanyika katika Jumba la Makusho ya kiyahudi tarehe 7 Septemba 2023.

Nyaraka zilizogunduliwa upya zilikusanywa na Mjesuit wa Italia Padre  Gozzolino Birolo kati ya Juni 1944 na masika ya 1945, mara baada ya ukombozi wa Roma na Washirika. Birolo alikuwa bursar wa Taasisi ya Kipapa ya Biblia kuanzia 1930 hadi kifo chake kutokana na saratani mnamo Juni 1945. Mkuu wa Taasisi katika kipindi hicho alikuwa Mjesuit wa Ujerumani Padre Augustin Bea, ambaye aliundwa kuwa Kadinali mnamo mwaka wa 1959 na kujulikana kwa kujitolea kwake kwa mazungumzo ya Kiyahudi-Katoliki, inaonekana hasa katika hati ya Nostra Aetate ya Mtaguso wa Pili wa Vatican  

Wanahistoria waliohusika katika utafiti wa nyaraka mpya ni Claudio Procaccia, Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni ya Jumuiya ya Wayahudi ya Roma; Grazia Loparco wa Kitivo cha Kipapa cha Sayansi ya Elimu Auxilium; Paul Oberholzer wa Chuo Kikuu cha Gregorian na Iael Nidam-Orvieto, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Holocaust huko Yad Vashem. Utafiti huo umeratibiwa na Dominik Markl (Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia na Chuo Kikuu cha Innsbruck) pamoja na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia, Mjesuti wa Kanada Michael Kolarcik. Roma ilitawaliwa na Wanazi kwa muda wa miezi tisa, kuanzia Septemba 10, 1943 hadi majeshi ya Muungano yalipokomboa mji huo mnamo Juni 4, 1944. Wakati huo, mateso ya Wayahudi yalisababisha, miongoni mwa mambo mengine, kufukuzwa na kuuawa kwa karibu watu 2,000, kutia ndani mamia ya watoto na vijana, kutoka katika jumuiya ya Wayahudi takriban 10,000 hadi 15,000 huko Roma.

Kupatikana kwa orodha ya majina ya wayahudi waliopata hifadhi katika nyumba za watawa wa kike na kiume jijini Roma
07 September 2023, 16:38