Kard.Zuppi,China kwa mazungumzo na Li Hui:njia za amani na usalama wa chakula
Vatican News
Kardinali Matteo Maria Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) alianza ziara yake huko Beijing Nchini China, kama mjumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya utume wa amani ya Ukraine inayoteswa ambayo ilimwona akitembelea Kyiv, Ukraine, Moscow, Urussi na Washington, Marekani kati ya mwezi Juni na Julai 2023. Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Vatican ililipoti kwamba Kardinali huyo alipokelewa katika mji mkuu wa China katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Watu wa China na Li Hui, na mwakilishi maalum wa Masuala ya Ulaya na Asia.
Kutafuta suluhishi hata za nafaka kwa walio hatarini
Mkutano huo kwa mujibu wa taarifa ya Vatican iliarifu kuwa ulifanyika katika mazingira ya wazi na ya kirafiki na ulijitolea kwa kutazama vita vya Ukraine na matokeo yake makubwa, ukisisitiza haja ya kuunganisha juhudi za kuhimiza mazungumzo na kutafuta njia zinazoongoza kwa amani. Tatizo la usalama wa chakula pia lilishughulikiwa, kukiwa na matumaini kwamba uuzaji wa nafaka nje ya nchi unaweza kuhakikishwa hivi karibuni, hasa kwa nchi zilizo katika hatari zaidi.