Tafuta

2023.09.09  Mabalozi wa Vatican waliwekwa wakfu wa kiaskofu na Kardinali Parolin watakaokwenda nchin,Ivory Coast na Kazakhstan,Kyrgyzstan na Tajikistan. 2023.09.09 Mabalozi wa Vatican waliwekwa wakfu wa kiaskofu na Kardinali Parolin watakaokwenda nchin,Ivory Coast na Kazakhstan,Kyrgyzstan na Tajikistan.  (Vatican Media)

Kard.Parolin awaweka wakfu wa kiaskofu mabalozi wawili

Jumamosi 9 Septemba katika altare ya Kanisa kuu la Vatican,Katibu wa Vatican aliongoza ibada ya kuwekwa wakfu kwa Maaskofu wakuu 2:Mauricio Rueda Beltz,aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Ivory Coast na George George Panamthundi, atakayekuwa balozi wa Vatican huko Kazakhstan,Kyrgyzstan na Tajikistan.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika utume mabalozi wa Vatican Mtakuwa ni wajibu wenu kuendeleza majadiliano ya kweli ya kiekumeni na ya kidini yanayopendelea kupiga marufuku unyonyaji wowote wa dini”. Ni moja ya ushauri kwa wawakilishi wapya wa Papa kwa mabalozi wapya wa nchini Ivory Cost na Kazakhstan, Kyrgyzstan na Tajikistan, aliyosema Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Jumamosi tarehe 9 Septemba 2023 katika mahubiri ya Misa ya kuwekwa wakfu kwao. Hawa ni  Monsinyo Mauricio Rueda Beltz, mwenye umri wa miaka 53, Mkolombia, aliyekuwa katibu msaidizi katika  Kitengo cha Wanadiplomasia Vatican na hapo awali pia  alikuwa ni mratibu wa safari za upapa, na kwa Monsinyo George Panamthundil, mwenye umri wa miaka 51 kutoka India, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa mshauri wa ubalozu huko Cyprus.

Kardinali Parolin wakati wa mahubiri
Kardinali Parolin wakati wa mahubiri

Kwa hiyo Kardinali Parolin, akizungumzia Masomo ya siku, yaliyosomwa aliomba  juu ya yote kuwa walinzi wanaochunguza alama za nyakati na mafundi wa upatanisho, ili watoto wa Mungu waliofanywa wabaki katika urafiki na Bwana na kupata neema yake. Kwa kuwa sehemu ya Baraza la Maaskofu, hasa kwa kuwekwa wakfu wa kiaskofu, Katibu wa Vatican alisisitiza kuwa itabidi kutathmini alama za nyakati na kubaini ni kiasi gani kizuri, kinachokaribia upeo wa mtazamo na kwamba ni kiasi gani badala yake inakuwa ni hatari ambayo, ikiwa haitambuliwa na kusimamishwa, inaweza kufanya uharibifu mwingi, na kuhatarisha maisha ya waamini. Kwa kukumbuka mahitaji ya maisha ya Kikristo yenye ustawi Kardinali Parolin alisisitiza kuwa watawasaidia wote waliobatizwa kuweka daima katika kuhifadhi urafiki na Bwana.

Ibada ya kuwaweka wakfu wa kiaskofu mabalozi wapya wa Vatican
Ibada ya kuwaweka wakfu wa kiaskofu mabalozi wapya wa Vatican

Akirejea ukurasa wa Injili ya Mathayo uliosomwa siku hiyo, Kardinali Parolin alikumbusha mwaliko wa kuwa mafundi wa upatanisho na kusambaza zawadi za kimungu, msamaha, amani ya ndani, uwepo wa Mwana wa Mungu katika Ekaristi, ili kuamsha upendo kwa Kanisa. Zaidi ya hayo, kama mabalozi watashika daima mawazo na maneno ya Papa ambaye kwa karama ya ukweli iliyopokelewa, wanaweza kuendeleza Kanisa vizuri zaidi katika uaminifu kwa mapokeo ya kweli, si kuchukuliwa kama majivu ya kuhifadhiwa, lakini kama moto wa kuweza kuchochewa.

Kwa mamlaka ya Vatican basi, Kardinali Parolin, alisisitiza kwamba watashuhudia jinsi Papa anavyojali sana amani na maendeleo yenye upatanisho, ambayo hatoi mifuko inayoongezeka ya watu waliotengwa walioachwa pembezoni katika hali ya umaskini na bila ulinzi au ambayo inazidisha usawa wa tabianchi. Kardinali Parolin alikumbuka uwepo wao katika huduma ya mema isiyokadirika ya ushirika na umoja, ambayo haibatilishi tofauti halali, lakini inapatanisha, inasafisha na kuunga mkono ili Makanisa mahalia yapate msaada kutoka katika Kanisa la ulimwengu wote umuhimu na kufurahiya uhuru sahihi kutoka kwa mamlaka ya kiraia.

Maaskofu wakuu  mabalozi wawili wakiwa tayari wamewekwa wakfu wa kiaskofu
Maaskofu wakuu mabalozi wawili wakiwa tayari wamewekwa wakfu wa kiaskofu

Kardinali Parolin vile vile alisema kuwa  huo ndio uzuri mkubwa na upendeleo wa kuwa Mkatoliki ambao licha ya kutoka katika tamaduni, lugha na tamaduni mbalimbali, wanajikuta wameunganishwa katika mambo ya msingi, katika sala, katika sherehe, katika majisterio katika ibada ya yote. Mwili uliounganika kwa uthabiti lakini hautoi usawa wa kuchosha na wa kutosheleza.  Katika Maandiko ya “Unitate Trinitatis”  ni kauli mbiu ya kiaskofu ya Monsinyo Panamthundil, ambayo kardinali Parolin alikumbusha kuwa  “umoja wa furaha na wa pande nyingi”.

Kwa hiyo basi pia akinukuu Azimio la Abu Dhabi kuhusu Udugu wa Kibinadamu  wa mkataba uliotiwa saini mnamo Februari 2019, mkuu wa diplomasia yaani Kardinali Parolin hatimaye alisisitiza kwamba “Dini hazichochei vita na kamwe haziongezi hisia za chuki, uhasama au itikadi kali. Neema na iwe kwa Mungu nchini Ivory Coast na Kazakhstan, nchi zenye sifa ya tamaduni nyingi na imani nyingi, imani hizi zimepata ardhi yenye rutuba na jumuiya mbalimbali za kidini zinaishi kwa kuheshimiana na kuishi pamoja kwa amani. Ikiwa kila mtu atafuata mfano wake, basi sura mpya itafunguka katika mahusiano ya pande zote, yenye nafasi ya kutosha ya ujuzi wa kina wa pamoja na ushirikiano mkubwa ambao utathibitisha kuwa dawa bora dhidi ya itikadi kali na ushupavu wote.

Mabalozi wapya kuwekwa wakfu wa kiaskofu
10 September 2023, 10:00