Tafuta

2023.09.24 Kardinali Czerny aliadhimisha misa katika Siku ya 109 ya wahamiaji na wakimbizi katika Kanisa la Mama Yeru wa Ulinzi huko Marsiglia. 2023.09.24 Kardinali Czerny aliadhimisha misa katika Siku ya 109 ya wahamiaji na wakimbizi katika Kanisa la Mama Yeru wa Ulinzi huko Marsiglia. 

Kard.Czerny:Wakimbizi wote wanatumaini moja la Maisha bora!

Kuwawezesha watu kuwa raia kamili na wito wa kushinda chuki na hofu ndiyo maneno yalisikika katika Madhabahu ya Mama Yetu wa Ulinzi huko Marsiglia,katika fursa ya maadhimisho ya Siku ya 109 ya Uhamiaji na Ukimbizi duniani Dominika 24 Septemba 2023 aliyosema Kard.Czerny.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Huduma Fungamani ya Binadamu, Kardinali Michael Czerny aliongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ajili ya Siku 109 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani, Dominika tarehe 24 Septemba 2023 katika Kanisa Kuu la Notre Dame de la Garde yaani Mama Yetu wa Ulinzi, huko Marsiglia, Kusini mwa Ufaransa. Katika mahubiri yake alisema katika somo la siku, Mtakatifu Paulo anatupatia onyo, yaani kama ombi ambalo linaweza kuonekana kama nia yake ya mwisho kwa jumuiya ya Wafilipi asemapo: “Ishi maisha yenu kama inavyostahili Injili ya Kristo!”( Fl 1:27). Wakati Mtume anapokaribia lengo kuu la maisha yake mwenyewe, kilio hiki kinatoka moyoni mwake. Ana shauku ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wake watairejea Injili daima, ili wastahili wito walioitiwa, wa ubatizo ambao wamepokea, na kuhakikisha furaha yao kuu. Katika Injili, tunapata mwongozo wote tunaohitaji ili kuwa wanafunzi wa Kristo. Na tunapoadhimisha Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani, Kardinali alisema tutazame  mfano huu wa maisha ya kila siku unatufundisha nini kuhusu hali halisi ya masumbuko ya  matukio ya uhamaji, ambao unatualika, kama Papa Francisko alivyotuhimiza  katika hitimisho la Mikkutano ya Bahari ya Mediterania. Mikutano, ya "kusikiliza historia za Maisha ya watu hawa.

Mkuu wa Baraza la kipapa la kuhamasisha huduma ya maendeleo Fungamani ya binadamu alisema kama ilivyokuwa mara nyingi katika siku za Yesu, kikundi cha wafanyakazi kilikwendakwenye uwanja wa jiji na kungoja nafasi ya kuajiriwa kwa siku hiyo. Mwenye shamba la mizabibu, baada ya kufikia makubaliano na wafanyakazi, aliwatuma kufanya kazi katika shamba lake. Kisha wafanyakazi hao wakaanza safari kuelekea shamba la mizabibu, ambako kazi inawangojea. Kwa muda wa siku, mmiliki aliendelea kurudi kwenye uwanja na kila wakati alijiri kikundi kipya cha wafanyakazi, kwa sababu hakutana wakae bila kufanya chochote. Vikundi tofauti vya wafanyakazi  walikwenda kwenye shamba la mizabibu kwa saa tofauti na matokeo yake, waliishia kufanya kazi kwa urefu tofauti wa wakati. Hata hivyo, wakati wa malipo ulipotimia  bwana aliamuru kwamba kila mtu apewe mshahara uleule, na hivyo kuzua malalamiko kutoka kwa wale walioanza siku ya kazi mapema. Jibu la mmiliki badala yake linasema “Rafiki, sikukosea; hukukubaliana nami kwa malipo ya kawaida ya kila siku? […] Ninachagua kumpa huyu wa mwisho kama vile ninavyokupa wewe. Je, siruhusiwi kufanya nipendavyo na mali yangu?” ( Mt 20:13-15 ). Mfano huo una mafundisho mawili.

Kwanza, kabisa Bwana, Mmiliki wa kweli wa shamba la mizabibu, ni mwema na mkarimu kwa wale ambao hawajapata nafasi ya kuanza kufanya kazi mapema. Na katika zaburi kulikuwa na maombi kwamba, “Bwana ndiye mwenye haki katika njia zake zote na ni mwema katika kazi zake zote” (Zab. 144). Pili, Yesu alitanguliza mantiki mpya isiyotulia, akichanganya haki na mshikamano na kugeuza utaratibu wa mambo unaokubalika katika jamii. Ni mantiki ambayo inakwenda mbali zaidi ya uwezo wetu wa kuelewa mahusiano ya kibinadamu. Kwa wafanyakazi wa siku hizi, mara nyingi safari ya kwenda kwenye shamba la mizabibu ni ngumu na yenye hatari zaidi kuliko wale walio katika mfano huo. Zile zinazoitwa "safari za matumaini" zinajumuisha kila aina ya matatizo: mitego, unyonyaji, unyanyasaji, vurugu ... Na watu wengine hata kupoteza maisha yao! Hata hivyo, hata katikati ya jangwa au katikati ya mawimbi ya kutisha, umuhimu wa lengo lao huwapatia nguvu ya kuendelea. Kwa sababu wote wana tumaini moja: kuwa na uwezo wa kuhakikisha maisha yenye heshima kwao na familia zao. Katika muktadha wa uhamiaji leo, hii kuwaweka wale walio wa mwisho kwanza kunamaanisha kufanya ahadi fulani za haraka, kibinafsi na kwa pamoja.

Na kwa kufanya hivyo kwanza kabisa ni lazima tujitolee katika kuhakikisha kwamba njia ya kuelekea “shamba la mizabibu” ni ya utaratibu na salama, tukihakikisha kwamba haki na utu wa kila mtu vinaheshimiwa. Hii inahitaji kubisha hodi, kupanua njia za uhamiaji za kawaida, na nafasi ya kuwa "raia kamili". Hilo lingechukua nafasi ya njia za bei ghali na hatari ambazo watu wengi leo hii wanaona kuwa chaguo lao pekee. Kwa kuongeza, hilo Kardinali alisema  ingekuza harakati kubwa zaidi za mtiririko wa uhamiaji, kwa manufaa ya wote. Kwa hakika, kama Papa Francisko alivyodokeza katika hotuba yake ya hitimisho la Mkutano kuwa  "jambo la uhamaji si jambo la dharura la muda, daima ni nzuri kwa ajili ya kuzalisha propaganda za kutisha, lakini ukweli wa wakati wetu, mchakato ... ambao lazima utawaliwe kwa busara ya busara".

Kardinali Czerny aliendelea kusisitiza kuwa ni lazima tujifunze kutoka katika mfano katika Injili hiyo  ili kuoanisha haki na mshikamano, tukichukua roho hiyo ya ushiriki wa kidugu ambayo inavuka mipaka yote. Kushiriki ambako Injili inatuita kunahitaji kujitoa sadaka, kwa maana lazima tuweke mipaka ya kile tunachochukua kwa ajili yetu wenyewe ili kila mtu apate kile anachohitaji, kwa uhakika kwamba Bwana hatatunyima kile tunachohitaji kweli. Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani mwaka huu umetolewa kwa uhuru wa kuchagua kuhama au kukaa. Kuanzia ukweli wa kusikitisha kwamba uhuru huo hauhakikishiwa mara kwa mara, Baba Mtakatifu anaangazia uharaka wa kujitolea kwa pamoja, ili kila mtu ahakikishwe kuwa ni "shamba la mizabibu" ambalo atafanya kazi kwa heshima katika nchi yake ya asili, bila kulazimishwa kuhama. .

Uhamiaji, ambao unakusudiwa kuendelea baada ya muda, husaidia kujenga "mizabibu ya rangi nyingi", jamii za kiutamaduni ambapo utofauti huwa fursa kwa kila mtu kutajirika. Cha kusikitisha, chuki na hofu hutuzuia kuchukua fursa hii, na kusababisha kutengwa na kubaguliwa. Kardinali Czerny alisisitiza: ni lazima tuitikie utamaduni unaowakutanisha wengine wenye utamaduni wa kukutana, chanzo cha furaha. Kwa kukabiliwa na changamoto hizi zote, Jumuiya za Kikristo zimetakiwa kuonesha mfano mzuri, kwa njia ya “njia hii ya maisha ya kiinjili yenye kashfa”, lakini ambayo Baba Mtakatifu alihimiza katika mkutano wa hitimisho la mikutano ya Mediteranea. Hivyo ndiyo, tuitikie wito uliozinduliwa na Mtakatifu Paulo wa kuwa nuru ya ulimwengu na chumvi ya dunia: basi, tuishi kwa namna inayostahili injili ya Kristo!" Alihitimisha.

25 September 2023, 15:18