Tafuta

2023.08.25 Bi Katalin Novak, Rais wa Jamhuri ya Hungaria amekutana na Papa Francisko mjini Vatican. 2023.08.25 Bi Katalin Novak, Rais wa Jamhuri ya Hungaria amekutana na Papa Francisko mjini Vatican.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Hungaria

Baada ya mkutano na Papa, Bi Katalin Novàk alizungumza na Katibu wa Vatican,Kardinali Pietro Parolin na Monsinyo Mirosław Wachowski,Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa na mashirika ya Kimataifa.Miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni kuhusu mzozo wa Ukraine na hali ya Wakristo wanaoteswa duniani.

Vatican News.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 25 Agosti 2023 amekutana na Rais wa Jamhuri ya Hungaria, Bi Katalin Novàk, ambaye baadaye alikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akiambatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa na amshirika ya Kimataifa

Mzozo wa Ukraine na kuteswa Wakristo duniani kote

Wakati wa mkutano wao katika Sekretarieti ya Vatican,  kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican inasomeka kuwa: “ mara baada ya kutaja ziara ya Kitume kwenda Budapest, ambayo ilifanyika tangu tarehe 28 hadi 30 Aprili 2023, baadhi ya mada ya maslahi ya kawaida ilijadiliwa, kama vile familia na maadili ya Kikristo”. Katika muendelezo wa mazungumzo “tulijikita na  vita vya Ukraine, tukiwa na kumbukumbu maalum ya hali ya kibinadamu, pamoja na juhudi za kumaliza mzozo. Hatimaye, ilitajwa mada ya uhuru wa kidini na hali ya Wakristo wanaoteswa duniani.”

Zawadi kutoka kwa Baba Mtakatifu:

Katika kukutana na Baba Mtakatifu kama kawaida wamebadilishana zawadi ambapo Papa Francisko amemzawadia Rais wa Jamhuri ya Hungaria: Ujumbe wa Amani wa 2023; Nyaraka za Upapa, kama vile Kitabu cha Njia ya Msalaba (Statio Orbis cha Machi 27, 2020), kilichohaririwa na LEV; na Sanamu ya shaba  iliyo na maneno: “Kuweni Wajumbe wa Amani.”

Zawadi kutoka kwa Rais wa Hungaria:

Bi Katalin amembaptia Papa “Sanduku lenye zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na divai na vitu vitakatifu. Picha  kutoka Transcarpathia, eneo la watu walio wachache wa Hungaria nchini Ukraine. Albamu ya picha ya Ziara ya Kitume ya  Baba Mtakatifu nchini Hungary Aprili iliyopita.

Na katika nakala ya pili ya albamu, ambayo Rais anairudisha nchini Hungaria, Papa amenadika maneno yanayosomeka hivi: “Ninamshukuru Rais Katalin Novak kwa kitabu hiki kinachokumbusha ziara yangu nchini Hungaria. Katika nchi yako, acha ujumbe wa amani uenee kwa ajili ya Ulaya iliyojeruhiwa na vita. Kwa baraka zangu, ninapyaisha matashi yangu mema ya umoja na udugu.

Kindugu

Francisko.”

Papa amekutana na Rais wa Hungaria Bi Katalin Novak
25 August 2023, 16:34