Papa ameteua Jimbo Kuu jipya la Osaka-Takamatsu,Japan
Vatican News.
Dominika tarehe 15 Agosti 203, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Mkuu Thomas Aquino Manyo Maeda, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni askofu mkuu wa Jimbo kuu la Osaka, kuwa Askofu mkuu wa kwanza waJimbo kuu jipya lililounganishwa la OSAKA na Takamatsu.
Kardinali Thomas Aquino Manyo Maeda alizaliwa tarehe 3 Machi 1949 huko Tsuwasaki, Kami Goto, Jimbo kuu la Nagasaki, nchini Japan. Baada ya kumaliza masomo yake katika Shule ya Sekondati ya Nanzan huko Nagasaki, alijiunga na Seminari Kuu ya Mtakatifu Sulpice huko Fukuoka. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadre mnamo tarehe 19 Machi 1975 na kuandikishwa katika Jimbo kuu la Nagasaki.
Tarehe 13 Juni 2011 aliteuliwa kuwa askofu wa jimbo la Hiroshima na kupokea wakfu wa kiaskofu tarehe 23 Septemba 2011. Amekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Osaka tangu 2014 na aliteuliwa kuwa Kardinali mnamo tarehe 28 Juni 2018 kwa kupewa Kanisa la Pudenziana, Roma.