Tafuta

2023.08.14 Kardinali Parolin amefika Sudan Kusini na kulakiwa na baadhi ya waamini na viongozi wa Kanisa na serikali. 2023.08.14 Kardinali Parolin amefika Sudan Kusini na kulakiwa na baadhi ya waamini na viongozi wa Kanisa na serikali. 

Kard.Parolin amefika Sudan Kusini kwa ziara ya siku nne

Katibu wa Vatican ameanza ziara ya siku 4 nchini Sudan Kusini ili kuonesha mshikamano wa Kanisa na eneo lililokumbwa na maafa la Malakal na juhudi za taifa hilo katika kuelekea amani na mshikamano wa kweli tangu kutoka kwa Baba Mtakatifu.Askofu Mkuu Ameyu alielezea ratiba ya ziara hiyo.Anatarajiwa kurudi Roma tarehe 17 Agosti 2023.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Katika ziara yake Kardinali Parolin kuelekea Nchi ya Sudan Kusini, baada ya kufika Juba asubuhi ya tarehe 14 Agosti 2023 amekutana na Kardinal Zubeir na kuzindua bango la kumbukumbu ya kukaa kwa Baba Mtakatifu katika Ubalozi  wakati wa ziara yake ya kitume ya hivi karibuni, kama ilivyoelezwa kwa waandishi wa Habari. Kwa mujibu wa  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Juba, Kardinali mteule Stephen Ameyu Martin Mulla, katika Mkutano na waandishi wa Habari kupitia ukurasa wa Facebook wa Radio Bakhita, Jumamosi jioni tarehe 12 Agosti 2023, alibainisha juu ya ziara ya Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican kwa mara ya pili kuanzia Jumatatu tarehe 14-17 Agosti 2023; na kwamba lengo lake ni mwendelezo wa ziara ya hivi karibuni ya Papa Francisko nchini Sudan Kusini, na ambapo atakutana na Rais Salva Kiir na naibu wake kwa  kutaka kutekelezwa kwa makubaliano ya amani. Kardinali Parolin pia anatarajiwa kutembelea majimbo katoliki ya Malakal na Rumbek.

Kardinali Parolin amefika Sudan Kusini kwa ziara ya siku nne kuanzia 14-17 Agosti
Kardinali Parolin amefika Sudan Kusini kwa ziara ya siku nne kuanzia 14-17 Agosti

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ameyu, alisema: “Anakuja kufuatilia baadhi ya kazi ambazo alipewa na kazi hizo ziko wazi katika akili zetu kama serikali na Kanisa. Tuko hapa tukisisitiza suala la amani ya kina miongoni mwa watu, amani ambayo ilitiwa saini mjini Addis Ababa, Mkataba Uliohuishwa wa Amani. Kufikia sasa bado haujatekelezwa kwa utaratibu na kuna dosari kuhusu mkataba huu na kwa hivyo lazima ufuatwe,” alisisitiza Askofu Mkuu Ameyu. Kwa kuongezea: “Baba Mtakatifu alipokuja, alituambia, hasa serikali kwamba watu wa Sudan Kusini wanapaswa kuwa pamoja, wafanye kazi pamoja. Na alisisitiza kuwa: “Umoja ndio utakaoweza kutuletea amani na Papa alirudia neno ‘pamoja’ mara tatu kwa sababu  ameongeza Ameyu "umoja maana yake ni umoja, umoja maana yake tunaweza kupata amani kati yetu na umoja maana yake kuna aina ya mazingira ya kirafiki miongoni mwetu,” alisisitiza Askofu Mkuu Ameyu

Kardinali Parolin amefika Sudan Kusini
Kardinali Parolin amefika Sudan Kusini

Kulingana na ratiba ya Kardinali, baada ya kukutana na Rais Kiir na viongozi wakuu wa serikali, Kardinali Parolin atawatembelea baadhi ya viongozi  wakuu akiwemo Kadinali Gabriel Zubeir, na kupanda miti katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa. Askofu Mkuu Ameyu alisema kuwa Katibu wa Vatican alitaka ziara yake ishughulikiwe kwa faragha na mapadre, watawa na waamin wachache sana wa kumpokea katika uwanja wa ndege siku ya Jumatatu karibu saa 4.00 asubuhi. Kwa mujibu wa Kardinali Ameyu alisema: “Kadinali Parolin angependa ziara hii ishughulikiwe zaidi faraghani na hapendi mapokezi makubwa. Hata hivyo, kutakuwa na baadhi ya viongozi wa dini, watawa wachache na ndugu wa kwenda kumlaki katika uwanja wa ndege akifika, kisha atapelekwa Ubalozi wa Vatican na taratibu nyingine zitafuata."  Aidha alisema kuwa "Ziara hii ni maalum kwa Jimbo la Malakal ambapo amealikwa na Askofu Stephen Nyodo Ador wa Malakal, kwenda kujionea hali ya Malakal. Sisi sote tunaifahamu hali ya Malakal, mikasa ya asili, mafuriko na mambo mengine mengi na mikasa  inayosababishwa na wanadamu,” Alikiri Askofu Mkuu Ameyu. “Pia, kuna fursa ya amani kwa hivyo atapenda kwenda kuona Malakal na kutoka hapo ataelekea Rumbek na atarudi hapa na kuruka mara moja  tarehe 17 Agosti hadi Roma, "alihitimisha maelezo yake Askofu Mkuu Ameyu.

Ziara ya Pili ya Katibu wa Vatican Kusini Sudan
14 August 2023, 13:35