Sudan Kusini:Kard.Parolin akaribishwa jimbo Rumbek na kuadhimisha Misa
Na Angella Rwezaula, - Vatican,
Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin tangu tarehe 14 Agosti 2023 alisafiri kwenda Nchini Sudan Kusini ambapo siku yake ya nne na ya mwisho, tarehe 17 Agosti 2023 ilimpeleka katika Jimbo la Rumbek asibuhi, baada ya kutembelea Jimbo la Malakal lenye wakimbizi wengi kutoka Sudan, na ambao wamejaribiwa na mikasa kadhaa ya vita ikiwemo hata mikasa ya asili kama mafuriko.
Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akiwa huko ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika mji wa Rumbek, Sudan Kusini ikiwa ni kuhitimisha ziara yake nchini Sudan Kusini, ambapo Kardinali ametoa mwaliko kwa watu wote kutembea katika njia za amani na upatanisho kwa manufaa ya nchi.
Hata hivyo Kardinali Parolin baada ya kupokelewa aliwasalimia wote na kushukuru sana mkuu wa mkoa kwa maneno ambayo aliyasema mara alipofika hapo Rumbek. Kwa njia hiyo alieleza furaha yake kuwa hapo na wao. Kama wanavyojua, hiyo ilikuwa ni ziara ya tatu nchini Sudan. Na hivyo Kardinali aliongeza kusema: “Ninakuwa sasa raia wa Sudan Kusini, ziara ya nne. Lakini daima ni furaha kuwa hapa.” Akiendelea ameeleza lengo lake la kufuata njia ya Papa Francisko ambaye alikwenda jijini Juba, Sudan Kusini, mwezi Februari uliopita kama wanavyokumbuka vizuri.
Kardinali alisema: “Ilikuwa ni ziara ya kiekumeni na askofu mkuu wa Canterbury na Msimamizi wa Kanisa la Presbyterian la Scotland ili tu kukuza, kuimarisha, mchakato wa amani, upatanisho na amani nchini Sudan Kusini.” Amesema. Kwa kuongeza: “Basi na hilo pia ndilo dhumuni la ziara yangu hapa kufuatia maelekezo ya Baba Mtakatifu”.
Aidha Kardinali alieleza alivyokuwa huko Malakal, ambao ulikuwa mwaliko wa Askofu kwa “sababu ya shida ya watu waliohamishwa na wakimbizi ni muhimu sana huko. Binafsi ameona kinachoendelea huko”. “Lakini bila shaka, Askofu Christian alipojua kuhusu kuja kwangu Sudan, alisema: “mbona ni safari fupi kufika Rumbek?” na kwa hiyo anikasema basi, ninafuraha hata mwaliko wako. Na hii ndiyo sababu niko hapa ili kushiriki nanyi wakati huu wa imani, wa sala, wa ushirika katika Kanisa Asante sana .” Alihitimisha kwa kuwatakia kila la heri.