Chad:Papa amemteua Mhs,Padre Tibinger kuwa askofu wa kwanza wa Koumra
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amechagua Jimbo jipya la Koumra, lenye eneo lililotengwa na jimbo la Sarh, na kulifanya kuwa jimbo kutoka katika Jimbo kuu la N'Djaména na wakati huo huo Jumamosi tarehe 12 Agosti 2023, Baba Mtakatifu amemteua askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Koumra, Mhashamiwa Samuel Mbairabé Tibingar, wa N'Djaména, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni makamu jimbo hilo hilo. Askofu mteule Samuel Mbairabé Tibingar alizaliwa huko Sarh tarehe 27 Julai 1972 na akapewa daraja la Upadre mnamo tarehe 26 Novemba 2005. Baada ya masomo yake ya Sekondari alijunga na Seminari Kuu Shirikishi ya Mtakatifu Luc de Bakara huko N'Djaména (1997-2004).
Masomo ya juu
Alipata leseni ya Maandiko Matakatifu katika Taasisi ya Kipapa ya Kibiblia huko Roma (2007-2011) na udaktari katika Kitivo cha Taalimungu nchini Italia ya Kati huko Firenze kati ya(2011-2016). Aidha ameshika nyadhifa zifuatazo: Paroko msaidizi wa Kanisa Kuu la N'Djaména (2005-2006), Paroko wa Mtakatifu Paul de Kabalaye huko N'Djaména (2006-2007); Mshiriki wa Parokia ya Watakatifu Martinona Giusto huko Lucardo Alto, huko Flirenze; Mkufunzi katika Seminari Kuu Shirikishi ya Sarh na kisha Gambera (2017). Tangu 2021 amekuwa Makamu wa Jimbo Kuu la N'Djaména.
Takwimu za Jimbo jipua la Koumara
Jimbo jipya la Koumra nchini Chad linaendana na Wiklya ya kiraia ya Mandoul, ambalo jiji la Koumra ni mji mkuu wake. Mkowa una wilaya 6, zilizogawanywa katika tarafa 15, na inashughulikia eneo la kilomita za mraba 17,330, na idadi ya watu wapatao 900,000. Jiji lilikuwa kituo cha utume na parokia zote zinazozunguka zilikua nje yake. Kwa kugawanya Jimbo kuu la N'Djaména, makao ya jimbo jipya ni mji wa Koumra. Kanisa kuu la Mzunguko mpya wa Kikanisa ni Kanisa la sasa la Parokia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, huko Koumra.