Tafuta

2023.07.12 SIGNIS Afrika huko Africa Kampala, Uganda. Baadhi ya washiriki wa Warsha. 2023.07.12 SIGNIS Afrika huko Africa Kampala, Uganda. Baadhi ya washiriki wa Warsha. 

Warsha ya SIGNIS Afrika:Waandishi katoliki wawe na huruma zaidi kwa wahamiaji

Warsha ya SIGNIS Afrika kwa wahusika wa vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika mjini Kampala,Uganda imemalizika kwa kutoa wito wa kutoa ripoti zenye huruma zaidi kuhusu wakimbizi ambazo hazivunji maadili ya uandishi wa habari.Washiriki kukutana na wakimbizi huko Kyangwali takriban Kilomita 300 kutoka mji mkuu Kampala,Uganda.

Na Padre  Paul Samasumo - Kampala

Warsga la SIGNIS  Afrika kuhusu wahamiaji na wakimbizi limemalizika mjini Kampala, Uganda kwa kutayarisha rasimu ya kile ambacho hatimaye kinapaswa kutambulika kama miongozo ya kitaalamu ya kutumiwa na vyombo vya habari vya Kikatoliki barani Afrika wakati wa kuripoti kuhusu wahamiaji na wakimbizi. Hata hivyo Kamati itaundwa kwa kazi zaidi ya rasimu hiyo.


Katika siku ya mwisho ya sehemu ya warsha hiyo iliyaonza tarehe 11 Julai 2023, wahusika wa vyombo vya habari kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda walishirikiana na washiriki katika majadiliano juu ya nini kifanyike ili kuhimiza ripoti za kitaalamu na za huruma ambazo bado ni za kweli na zenye lengo kuu. Swali la ni nini kinachomtofautisha mwanahabari Mkatoliki wa Kiafrika lilijadiliwa kwa kwa kirefu zaidi.


Katika siku ya Ijumaa tarehe 15 Julai 2023,  vile vile washiriki wa Warsha hiyo  kuhusu Wakimbizi na wahamiaji watasafiri hadi Makazi ya Wakimbizi huko Kyangwali takriban Kilomita 300 kutoka mji mkuu Kampala, Uganda. Kwa hiyo hii itakuwa siku ya kuzamishwa  kwa undani ili kuona jinsi gani wakimbizi na wahamiaji wanavyoishi katika makazi hayo. Wazo  hilo sio tu kuzungumza juu ya wahamiaji na wakimbizi katika vyumba vya mikutano lakini pia kuwa na fursa ya kufanya uozefu wa mkutano wa siku nzima wa kukutana na kuwasikiliza wakimbizi.

Rais wa Ulimwengu wa Signis Bi Helen akihutubia katika Warsha ya Signis Afrika huko Kampala Uganda.
Rais wa Ulimwengu wa Signis Bi Helen akihutubia katika Warsha ya Signis Afrika huko Kampala Uganda.

Ikumbukwe kwamba Warsha ya SIGNIS Afrika kwa ajili ya mashirika ya vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika ilifunguliwa rasmini Jumanne asubuhi tarehe 11 Julai 2023. Warsha hiyo inafanyika katika seminari Kuu ya kitaifa ya Ggaba, ambayo ipo kilomita 9, kutoka mjini Kampala nchini Uganda na inawakutanisha waandishi wa habari wapatao 50 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Warsha hiyo iliandaliwa na Signs Afrika kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, ambayo imetaka kutafuta njia za kipekee za Kiafrika za kuweza kuzungumzia juu ya wahamiaji katika vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika kutoka katika dhana hadi ripoti za huruma zaidi zinazohifadhi heshima ya wahamiaji na wakimbizi.

 

14 July 2023, 16:40